Kusoma Tawassul Kwa Kutaja Majina Ya Allaah 99 Inafaa?

 

Kusoma Tawassul Kwa Kutaja Majina Ya Allaah 99 Inafaa? 

 

Alhidaaya.com

 

SWALI:

 

Asalam Aleikum, shukran sana kwa hii nakala ya Al-hidaya, Inshallah Mungu Atawapa jaza yenu. Swali langu ni hii, hii kusoma tawasulli ambayo watu wanataja majina 99 ya Allaah Subhanna WaaTalla ni vizuri?

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho

 

Tufahamu kuwa hakuna mas-ala ya Muislamu kusoma Tawassul, linahitajika ni wewe kumuomba Allaah Aliyetukuka kwa kuyatumia majina hayo kwa mahitaji yako unayotaka. Kwa minajili hiyo, Allaah aliyetukuka Anasema:

قُلِ ادْعُوا اللَّـهَ أَوِ ادْعُوا الرَّحْمَـٰنَ ۖ أَيًّا مَّا تَدْعُوا فَلَهُ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ ۚ 

Sema; Muiteni Allaah au muiteni Ar-Rahmaan, vyovyote mtakavyomwita basi Yeye Ana Majina Mazuri kabisa. [Al-Israa: 110]

 

Na Anasema tena Aliyetukuka:

وَلِلَّـهِ الْأَسْمَاءُ الْحُسْنَىٰ فَادْعُوهُ بِهَا ۖ وَذَرُوا الَّذِينَ يُلْحِدُونَ فِي أَسْمَائِهِ ۚ سَيُجْزَوْنَ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ ﴿١٨٠﴾

Na Allaah Ana Majina Mazuri kabisa, basi muombeni kwayo. Na waacheni wale wanamili katika kukadhibisha Majina Yake, watalipwa yale waliyokuwa wakiyatenda. [Al-A‘raaf: 180].

 

Kwa njia hiyo, Muislamu anatakiwa anapomuomba Allaah Aliyetukuka aanze kwa kumsifu na kisha kutaja Majina Yake mazuri kama Ee Allaah, Ee Rahman, Rahiym na majina mengine kabla ya kutaja haja yake.

 

Kwa hiyo, ni juu yetu kama Waislamu kumuomba Allaah Aliyetukuka kwa kuyataja majina yake Mazuri kabla ya kumtaka tunayotaka. Wala si sawa kuyaimba Majina Yake kwa njia ya pamoja au kwa mtu mmoja mmoja kwani hilo sio lengo la Majina hayo.

 

Bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo zaidi:

 

Kusoma Majina Ya Allaah Kwa Idadi Maalum

 

Je, Majina 99 Ya Allaah Kazi Yake Ndio Hii?

 

Du'aa Gani Asome Mkewe Apate Kizazi? Je, Kusoma Majina Allaah Mara Kadhaa na kupuliza Katika Maji Inafaa?

 

 

Na Allaah Anajua zaidi.

 

 

Share