Skip navigation.
Home kabah

Kusoma Majina Ya Allaah Kwa Idadi Maalum

SWALI:

Nimeona kitabu kimeandikwa majina ya M/mungu na maana yake kwa kiswahili, na baadhi ya majina yameelezwa kwamba kama ukiyataja mara kadhaa 70 au 100-nk, basi unaweza kupata jambo fulani, jee nikweli mambo haya?

 


JIBU:

Vitabu kama hivyo vipo vingi vinavyoelezea mambo haya ya kutaja majina ya Allaah سبحانه وتعالى  kwa idadi maalumu nawe utapata thawabu kadhaa. Kwa hakika ukiangalia vitabu hivyo hutapata kukuta maelezo hayo ni Hadithi na ikiwa imesemekana kuwa ni Hadithi basi aghalu za ni Hadiythi zisizotegemewa.  Kumkumbuka Allaah سبحانه وتعالى  kwa kutumia Majina Yake au aina yoyote ya Tasbiyh kwa kutaja idadi ma'aluum bila kuweko dalili katika Qur'aan au Sunnah ni jambo la uzushi (Bid'ah) na linapaswa kuachwa kwani mtu atahangaika bure na kitendo hakitokubaliwa kutokana na dalili za Hadiythi nyingine kuhusu mambo ya Bid'ah, mojawapo wapo ni hii:

((من عمل عملا ليس عليه أمرنا فهو رد    ((خرجه مسلم في صحيحه

 ((Atakayefanya kitendo kisichokuwa katika amri yetu basi kitarudishwa (hakitokubaliwa) )) Imesimuliwa na Muslim

Jambo ambalo lipo wazi kuhusu majina ya Allaah سبحانه وتعالى  ni kama inavyotueleza Qur’ani kuwa Allaah سبحانه وتعالى  ana majina mazuri hivyo tumuombe kupitia majina hayo yake. Allaah سبحانه وتعالى   Anasema:

}}وَلِلّهِ الأَسْمَاء الْحُسْنَى فَادْعُوهُ بِهَا{{



{{Na Mwenyezi Mungu ana majina mazuri kabisa, basi muombeni kwa hayo}} Al-A'araaf 7: 180 

Na Amesema tena:

}}قُلِ ادْعُواْ اللّهَ أَوِ ادْعُواْ الرَّحْمَنَ أَيًّا مَّا تَدْعُواْ فَلَهُ الأَسْمَاء الْحُسْنَى{{

{{Sema: Mwombeni Allah (Mwenyezi Mungu), au mwombeni Rahman (Mwingi wa Rehema), kwa jina lolote mnalo mwita. Kwani Yeye ana majina mazuri mazuri}}

 Israa 17: 110 .

Kwa hiyo unaweza kuomba mfano unataka Allaah سبحانه وتعالى ِ Akughufurie dhambi zako, ukamwita kwa Jina Lake Tukufu 'Yaa Ghaffaaru' au 'Ya 'Afuwwu'  kama mfano unataka Akuruzuku kitu ukamwita 'Ya Razzaaq' au mfano unamuomba kitu na unataka Akutakabalie dua yako, ukamwita 'Ya Sami'u', 'Ya Qariybu', 'Ya Mujiybu' na kadhalika.  Hivi unaweza kumwita kwa mara unazotaka bila ya kuweka idadi ma'aluum.  

Katika vitu vyenye idadi maalumu ni dhikri (kumtaja Allah) kwa kusema: Subhanallah, Alhamdullillah, Allahu Akbar na adhkari nyingine za baada ya Swalah, au za mchana na usiku. Tazama Kitabu cha 'Hiswnul-Muslim' kilichokuweko katika kiungo hiki cha Alhidaaya humo utapata dalili ya Tasbiyh na Adhkaara ambazo zimetajwa idadi ma'aluum kuzisoma.

HISWNUL MUSLIM- Du'aa katika Qur-aan Na Sunnah

Khaswa katika kiungo hiki kumetajwa idadi ma'aluum.

Fadhila za Tasbiih, Tahmiid, Tahliil, na Takbii

 

Wa Allaahu A'alam