Ahli Bait Wa Mtume wapo? Na Nani Masharifu?

 

SWALI:

 

Ningependa kutatukiwa kuhusu akhlul bait ya Mtume kama wapo na ikiwa hawapo masharifu ni kina nani? kulingana na quraan na sunnah ya mtume.

 


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani kwa swali lako kuhusu kuwepo kwa Ahlul Bayt ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).

Hakika ni kuwa masharifu kwa huku kwetu Afrika Mashariki ni Ahlul Bayt wa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).

 

Je, ni wao wanaojiita masharifu kuwa ni Ahlul Bayt au wengine? Hayo yanaeleweka mbele ya Allaah Aliyetukuka tu.

 

Sisi Waislamu tunachukulia kila kitu kwa wenzetu kwa dhana nzuri. Ikiwa mtu amesema kuwa yeye ni katika kizazi cha Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) nasi tunachukulia hivyo hivyo.

 

Hilo ni kuwa kizazi chake bado kipo na kitaendelea kuwepo. Kuwepo huko ni kuwa yeye mwenyewe, Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ametueleza kuwa katika mwisho wa zama kabla ya Qiyaamah atakuja Mahdi anayetarajiwa kutoka katika kizazi chake. Hivyo, kizazi chake kipo na kitaendelea kuwepo.

 

 

Tafadhali bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo kamili:

 

 

Ufafanuzi Wa Ahlul Bayt (Masharifu) Na Kizazi Chake

 

Vizazi Vya Mtume Vipo Bado Na Je Ni Kweli Kuwa Hawatawakiwi Kupokea Sadaka?

 

Usharifu Nini Maana Yake? Je Ukoo Wa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) Uko Kweli?

 

Kizazi Cha Mtume (Swalla Allaahu ‘Alayhi Wa Aalihi Wa Sallam) Bado Kinaendelea?

 

Masharifu Wasioswali Wana Maovu Na Maasi Watukuzwe? Je, Wao Bora Kuliko Mja Anayefuata Sheria?

 

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share