Usharifu
SW
Assalaam Alaykum
Ya Maalim, Hua tunasikia kua kuna Koo (family) za MASHARIFU ktk baadbi ya Vijiij vyetu Vya E.Afrika je hii ni kweli na
Na vipi CHEO hichi hupatikana mbele ya Allah?
JIBU:
Neno Sharifu limetokana na neno la Kiarabu Sharaf lenye maana ya honour, dignity, distinction, high rank, nobility (Dkt. Rohi Baalbaki, Al-Mawrid: A Modern Arabic - English Dictionary, uk. 667). Haya maneno ya maana ifuatayo kwa Kiswahili honour (utukufu, adhama), dignity (heshima, hadhi), distinction (heshima, sifa), high rank (cheo kikuu), nobility (ulodi, usharifu, uungwana).
Hili ni neno kama maneno mengine ya Kiswahili ambayo yemetoka nje ya maana ile halisi ya Kiarabu na mara nyingi tunaifasiri
}} وَلَقَدْ كَرَّمْنَا بَنِي آدَمَ وَحَمَلْنَاهُمْ فِي الْبَرِّ وَالْبَحْرِ وَرَزَقْنَاهُم مِّنَ الطَّيِّبَاتِ وَفَضَّلْنَاهُمْ عَلَى كَثِيرٍ مِّمَّنْ خَلَقْنَا تَفْضِيلا{{ً
{{Na hakika tumewatukuza wanaadamu, na tumewapa vya kupanda nchi kavu na baharini, na tumewaruzuku vitu vizuri vizuri, na tumewafadhilisha kwa fadhila kubwa kuliko wengi miongoni mwa tulio waumba}} (Israa 17: 70).
Na Allah Anasema ubora upo katika uchaji Mngu:
}}إِنَّ أَكْرَمَكُمْ عِندَ اللَّهِ أَتْقَاكُمْ إِنَّ اللَّهَ عَلِيمٌ خَبِيرٌ{{
{{Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliye mchamngu zaidi katika nyinyi}} (AL-Hujuraalt 49: 13).
Na Mtume wa Allah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika Hijjatul Wida'a alisema kwamba hakuna tofauti wala ubora kwa Mwarabu juu ya asiyekuwa Mwarabu, wala mweupe na mweusi isipokuwa kwa uchaji Mungu.
Swali ambalo tunaweza kujiuliza ni kuwa: Sharifu ni nani? Kwa huku kwetu na Waislamu ulimwengu mzima ni yule mwenye kizazi cha Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) isipokuwa katika nchi ya
Wengine wanaweza kusema ni Bani Hashim na kutaka kutukuzwa na kupata fursa ya kuwatawala watu. Nchi ya
Na tufahamu ya kwamba katika mas-ala haya mafungamano halisi si ya kidamu kwani mahusiano ya ki-Imani ndio yaliyo halisi. Ndio Nabii Nuh (‘alayhis-salaam.) akaambiwa kuwa mtoto wake si wake japokuwa walikuwa na unasaba wa kidamu. Allah Anasema:
}}وَنَادَى نُوحٌ رَّبَّهُ فَقَالَ رَبِّ إِنَّ ابُنِي مِنْ أَهْلِي وَإِنَّ وَعْدَكَ الْحَقُّ وَأَنتَ أَحْكَمُ الْحَاكِمِينَ{{
}} قَالَ يَا نُوحُ إِنَّهُ لَيْسَ مِنْ أَهْلِكَ إِنَّهُ عَمَلٌ غَيْرُ صَالِحٍ فَلاَ تَسْأَلْنِ مَا لَيْسَ لَكَ بِهِ عِلْمٌ إِنِّي أَعِظُكَ أَن تَكُونَ مِنَ الْجَاهِلِينَ{{
{{Na Nuhu alimwomba Mola wake Mlezi: Ee Mola Mlezi wangu! Hakika mwanangu ni katika ahali zangu, na hakika ahadi yako ni haki. Na Wewe ni Mwenye haki kuliko mahakimu wote. Akasema: Ewe Nuhu! Huyu si katika ahali zako. Mwendo wake si mwema. Basi usiniombe jambo usio na ujuzi nalo}} (Huud: 11: 45 - 46).
Tukichukulia mambo ya kinasaba tunajikuta tuna maswali mengi na utata mkubwa, kwani huku kwetu inachukuliwa kuwa ni wale waliozalikana na 'Aliy na Faatimah bint Rasuul (Radhiya Allaahu ‘anha) Je, nasaba Kiislamu inachukuliwa upande gani? Upande wa mama au wa baba? Jawabu ni kuwa nasaba inachukuliwa kwa upande wa baba.
Ikiwa ni kutoka kwa baba, kwa nini watoto wa nduguze 'Aliy (Radhiya Allaahu ‘anhu)
Ikiwa tutasema ya kuwa watoto wa 'Ali na Faatimah (Radhiya Allaahu ‘anha) wote walikuwa ni Bani Haashim, hivyo kuingia katika usharifu. Je, kwa nini tunabagua baina ya watoto wao? Inafahamika kuwa wao walikuwa na watoto kadhaa miongoni mwao ni Hasan, Husayn, Muhsin, na kadhalika mbali na kuwa 'Ali (Radhiya Allaahu ‘anhu) alikuwa na watoto wengine wa kiume kwa wake wengine. Swali ni kuwa ni kwa nini masharifu wanachukuliwa kuwa ni wale wazawa wa Husayn (Radhiya Allaahu ‘anhu) na ilhali Hasan (Radhiya Allaahu ‘anhu) ndiye aliyekuwa mkubwa (mtoto wa kwanza) naye alizaa watoto kadhaa wa kiume?
Labda tukiafikiana katika maana ya Sharifu kinasaba huenda tukapata ufumbuzi madhubuti kuhusu familia hiyo. Ajabu ni kuwa tunapata masharifu wa makabila yote ya kilimwengu kwa mfano Tanzania wapo Masharifu wa Kiarabu, Kihindi, Kidigo, Kizaramo, Kirangi n.k. na Kenya vilevile wapo Masharifu wa Kiluhya, Kiswahili, Kikikuyu, Kibajuni, wa Kiarabu, wa Kisomali, wa Kiborana na wengine. Na ukienda nchi nyengine utapata wapo wengi zaidi ya hao. Na ili kupata jaha na utukufu wameleta hekaya chungu nzima ambazo zinamuingiza mtu katika kufuru. Wangapi wanaodai ni Masharifu huko Afrika ya Mashariki tunaowajua na kuwasikia wana matendo yasiyokuwa ya Kiislam? Wangapi wana wanawake zaidi ya kumi na watoto hata wenyewe hawawajui!! Kila wakienda kijiji fulani wanapewa mwanamke na hata ilifika baadhi ya sehemu, baadhi ya hao wanaojidai ni Ma-Sharifu anapewa mke wa mtu alale naye
Tukumbuke kuwa yale madai wanayosema Masharifu kuwa wao wataingia Peponi bila ya hesabu ni uongo na tujihadhari
Kadhalika Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipoteremshiwa aya isemayo:
}}وَأَنذِرْ عَشِيرَتَكَ الْأَقْرَبِينَ {{
{{Na uwaonye jamaa zako walio karibu nawe} (Ash-Shu'araa 26: 214),
alisema: "Enyi Maquraysh! Jinunulieni nafsi zenu kutoka kwa Allah, kwani mimi sitowafaa kitu kwa Allah. enyi Bani 'Abdi Manaf! Sitowafaa kitu kwa Allah. Ewe Swafiya (shangazi yake), sitokufaa kitu kwa Allah. Ewe Faatimah (bint Muhammad) niombe utakalo, lakini sitokufaa kitu kwa Allah" (Ahmad).
Na miongoni mwa kauli zilizotangaa
{{Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliye mchamngu zaidi katika nyinyi}} (49: 13).
Hivyo, yeyote mwenye kufanya matendo mema na kuacha maovu na akamcha Allah basi anakuwa katika cheo kitukufu mbele ya Allah kuliko yule mwenye nasaba nzuri lakini matendo mabaya.
wa Allaahu A'alam
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha



Assalaam aleykum, Sina nia
Assalaam aleykum,
Sina nia ya kukukosoa, ila nakumbusha tu kwani ni wajibu wetu kukumbushana. Tunaambiwa na maulamaa kua ni bora zaidi kuandika SWALLA LLAAHU ALAYHI WA SALLAM badala ya "S.A.W" SUBHAANAHU WATAALA badala ya "S.W" na mengineo yalofanana na hayo. Kwa kuona kua maulamaa wetu wa kitengo hichi wanatumia hayo yaliyokatazwa, kuacha itakua nzito. Kwahiyo tujitahidi tukumbuke kuandika kirefu maneno haya ili tuwe mfano wa kuigwa. Allaah atupunguzie sahau inshallah.
Samahani kama ntakua nimekosea au metumia lugha mbaya.
Wa Billahit-tawfiyq.
Assalaamu 'alaykum wa
Assalaamu 'alaykum wa Rahmatullaah wa Barakaatuh,
Tunamshukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) kwa neema zote. Na tunakushukuru na we kwa hima yako na ari ya kusimamisha mafunzo sahihi ya dini yetu jambo ambalo ndilo tunalipigana nalo usiku na mchana.
Mawazo yako mazuri na hakika hujakosea kabisa na tunakushukuru kwa maoni yako hayo.
Ukitazama vizuri kwenye tovuti, na haswa kwenye majibu mengi ya maswali yetu siku za karibuni, utakuta kwamba tunayazingatia sana hayo na tunawarekebisha wengi wenye kufupisha utukufu wa Allaah, na kumswalia Mtume wetu (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).
Hapo ulipoandika chini ya hilo jibu, hilo ni miongoni mwa majibu ya zamani ambayo tulikuwa tukiandika hivyo kabla ya kupata fatwa za Maulamaa kuhusiana na hayo. Baada tu kujua hayo, basi tuliacha mara moja kufanya hivyo na tukawa hadi leo AlhamduliLlaah tunakamilisha. Lakini ni vigumu kwa kuwa ni watu wachache sana wanaoshughulika na kazi hii kubwa na nzito, kuweza kupitia makosa hayo yote na kuyarekebisha kwa mara moja. Kila mara tunajitahidi kurekebisha hayo na kwa kuwa majukumu ni mengi na uchache wetu, basi hadi sasa tunajisukuma kuimaliza kazi hiyo.
Tunakushukuru tena na tunakuomba pindi utakapoliona jingine lenye kuhitaji kutanabahishwa sisi ili iweze hii tovuti yenu ya ALHIDAAYA kuwa katika njia sahihi na mwelekeo ulionyooka utakaomridhisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) na kuwenda sambamba kabisa na mafunzo mazuri kabisa ya Mtume wetu kipenzi, Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).
Jazaaka Allaahu khayra
Ndugu zako,
ALHIDAAYA