Kauli Za Salaf
Kauli Za Salaf Na 'Ulamaa
Kauli Za Salaf
Shujaa Ni Yule Anayejizuia Na Hawaa (Matamanio Ya Nafsi)
Imaam Sufyaan Ath-Thawriy (Rahimahu Allaah) amesema:
"Shujaa zaidi katika watu, ni yule mkakamavu zaidi katika kujizuia na Hawaa (matamanio ya nafsi)."
[Bahjatu Al-Majaalis, mj.1, uk. 808]
Kauli Za Salaf
Msiambatane Na Watu Wa Bid'ah Na Msijadiliane Nao
Imaam Abu Qilaabah (Rahimahu Allaah) amesema:
"Msikae na watu wa Matamanio (watu wa bid'ah), na wala msijadiliane nao, hakika mimi sijiaminishi juu yenu kuwa watashindwa kuwazamisha katika upotevu wao au kuwafunika kwa hadaa kwa yale mnayoyajua (mkavurugukiwa)."
[Ad-Daarimiy, Al-Aajuriy na wengineo]
Kauli Za Salaf
Msikae Na Watu Wa Bid'ah Wala Kushirikiana Nao
Amesema 'Abdullaah bin 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa):
"Msikae na watu wa Matamanio ya nafsi, hakika kukaa nao kunasababisha maradhi (kunaharibu Dini)."
[Isnaad yake ni sahihi kama ilivyo katika Utangulizi wa Sunan Ad-Daarimiy]
Kauli Za Salaf
Wafundisheni Watoto Wenu Mapenzi Kwa Maswahaba (Ridhw-waanu Allaah 'Alayhim)
Imaam Maalik (Rahimahu Allaah) amesema:
"Walikuwa Salaf wakiwafundisha watoto wao mapenzi kwa Abu Bakr na 'Umar, kama wanavyofundisha Suwrah katika Qur-aan."
Kauli Za Salaf
Anayetafuta Kuifahamu Dini Bila Isnaad
Imaam Ibn Mubaarak (Rahimahu Allaah) amesema:
"Mfano wa yule anayeitafuta (kuifahamu) Dini bila Isnaad (maagemezi ya dalili) ni mfano wa yule anayepanda darini bila ngazi."
Kauli Za Salaf
Watu Wa Bid'ah Ni Khawaarij
Imaam Ayyuwb As-Sakhtiyaan (Rahimahu Allaah) alikuwa akiwaita watu wa bid'ah kuwa ni Khawaarij na akisema:
"Hakika Khawaarij wametofautiana kuhusiana na majina yao, lakini wamekubaliana kuhusiana na upanga (kumuasi Mtawala)."
Kauli Za Salaf
Nasiha Zenye Kima Kwa Watafutaji Elimu
Shaykh Sulaymaan Ar-Ruhayliy (Hafidhwahu Allaah) amesema: