Kufunga Mikono Katika Swalaah
Kufunga mikono katika Swalaah ni Sunnah iliyothibiti kutoka kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na ni jambo alilolisisitiza sana katika Swalaah na hata kuwasahihisha wale waliokuwa wakikosea kufunga mikono yao ndani ya Swalaah. Isitoshe ni Sunnah sahihi iliyothibiti hata kwa Manabii waliotangulia kama anavyotujulisha mwenyewe Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) katika Hadiyth zifuatazo.