Skip to main content

11B-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: كِتَابُ الفَرْق بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ Kitabu Cha Kutengana Mke Na Mume: Talaka Rejea02-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Kutengana Mke Na Mume: Talaka Rejea: Mume Akimtaliki Mkewe Talaka Ya Tatu

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

كِتَابُ الفَرْق بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ

Kitabu Cha Kutengana Mke Na Mume 

طَلَاقٌ رَجْعِي

Talaka Rejea 

Alhidaaya.com

18-Mume Akimtaliki Mkewe Talaka Ya Tatu:

Mtu akimtaliki mkewe talaka ya tatu, basi mkewe anakuwa ameachika talaka mtengano, utengano mkubwa "طَلَاقٌ بَائِنٌ بَيْنُونَةٌ كُبْرَى", na anakuwa ni haramu kwake.  Kadhalika, haruhusiki kumrejea mpaka aolewe na mume mwingine ndoa iliyo sahihi.  Allaah Ta'aalaa Amesema:

 "فَإِن طَلَّقَهَا فَلَا تَحِلُّ لَهُ مِن بَعْدُ حَتَّىٰ تَنكِحَ زَوْجًا غَيْرَهُ"

"Na akimtaliki (mara ya tatu), basi hatokuwa halali kwake baada ya hapo mpaka aolewe na mume mwengine".  [Al-Baqarah: 230]

Na kama hiyo haitoshi, ni lazima pia mume huyo mpya amuingilie jimai sahihi ya kushibisha (jimai halisi) kutokana na Hadiyth ya 'Aaishah (Radhwiya Allaah 'anhaa) kwamba:

 "أنَّ امْرَأَةَ رِفَاعَةَ الْقُرَظِيِّ جَاءَتْ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَتْ: يَا رَسُولَ اللَّهِ، إِنَّ رِفَاعَةَ طَلَّقَنِي فَبَتَّ طَلاَقِي، وَإِنِّي نَكَحْتُ بَعْدَهُ عَبْدَ الرَّحْمَنِ بْنَ الزَّبِيرِ الْقُرَظِيَّ، وَإِنَّمَا مَعَهُ مِثْلُ الْهُدْبَةِ‏.‏ فقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ‏لَعَلَّكِ تُرِيدِينَ أَنْ تَرْجِعِي إِلَى رِفَاعَةَ؟ لاَ، حَتَّى يَذُوقَ عُسَيْلَتَكِ وَتَذُوقِي عُسَيْلَتَهُ ‏"

“Mke wa Rifa-'at Al-Quradhwiy alikuja kwa Rasuli (Swalla Allaah 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia:  Ewe Rasuli wa Allaah!  Rifa-'at ameniacha talaka tatu mpigo, nami baada ya kuniacha, nimeolewa na 'Abdulrahmaan bin Az-Zubayr Al-Quradhwiy, naye ana mfano wa ncha ya nguo (dhakari yake imelegea, haisimami vizuri).  Rasuli (Swalla Allaah 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia:  Inaonyesha unataka kurudi kwa Rifa-'at.  Hapana, huwezi kurudi, mpaka ('Abdulrahmaan) aonje asali yako (akuingilie kisawasawa) na wewe uonje asali yake (akufikishe kileleni)".  [Hadiyth Swahiyh.  Imechakatwa na Al-Bukhaariy (21639) na Muslim (1433)