Skip to main content

11C-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: كِتَابُ الفَرْق بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ Kitabu Cha Kutengana Mke Na Mume: الطَّلَاقُ السُّنِّيُّ والبِدعِيُّ Talaka Ya Kisunnah Na Kibid'ah03-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: كِتَابُ الفَرْق بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ Kitabu Cha Kutengana Mke Na Mume: Talaka Ya Kisunnah: Idadi Ya Talaka

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

كِتَابُ الفَرْق بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ

Kitabu Cha Kutengana Mke Na Mume 

الطَّلَاقُ السُّنِّيُّ والبِدعِيُّ

Talaka Ya Kisunnah Na Kibid'ah

Alhidaaya.com 

03: Talaka Ya Kisunnah: Idadi Ya Talaka:

Kwanza:  Kwa Mwenye Kupata Hedhi Aliyeingiliwa: 

Talaka ya Kisunnah inapatikana kwa huyu kwa kumpa talaka moja tu akiwa katika hali ya utwahara bila mumewe kumuingilia, kisha amsubirie mpaka eda yake imalizike (twahara tatu), na wala asiandamize talaka nyingine kabla ya kumalizika eda yake.  Na ikiwa ataandamiza, basi inakuwa ni talaka ya kibid'-ah kwa mujibu wa kauli ya Jumhuwr kinyume na Ash-Shaafi'iy na Ibn Hazm.  Dalili kuhusiana na suala hili zimeelezwa kwenye suala la kutoa talaka tatu kwa mpigo. 

Na kama atampa talaka moja kila baada ya kutwaharika na hedhi, hukmu yake itakuwa ni sawa na hukmu ya kumpa talaka tatu kwa mpigo akiwa katika hali ya utwahara.  Hii ni kauli ya Ahmad, Maalik, Al-Awzaa'iy na Abu 'Ubayd. 

Pili:  Kwa Ambaye Hakuingiliwa:

Huyu anakuwa ni kama aliyeingiliwa.  Ikiwa atamtaliki mkewe ambaye hakumuingilia talaka tatu, basi talaka zake zinakuwa ni kinyume na talaka ya Kisunnah. 

Tatu:  Kwa Ambaye Hapati Hedhi Kutokana Na Umri Mdogo Au Mkubwa:

Huyu eda yake inakuwa ni kwa miezi kama Alivyosema Allaah Ta'aalaa: 

"وَاللَّائِي يَئِسْنَ مِنَ الْمَحِيضِ مِن نِّسَائِكُمْ إِنِ ارْتَبْتُمْ فَعِدَّتُهُنَّ ثَلَاثَةُ أَشْهُرٍ وَاللَّائِي لَمْ يَحِضْنَ"

“Na wale wanawake wanaokoma hedhi miongoni mwa wanawake wenu, mkiwa mna shaka, basi eda yao ni miezi mitatu, pamoja na wale wanawake wasiopata hedhi”. [At-Twalaaq: 04]