Skip to main content

11B-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: كِتَابُ الفَرْق بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ Kitabu Cha Kutengana Mke Na Mume: Talaka Rejea11-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Kutengana Mke Na Mume: Talaka Rejea: Talaka Rejea Inapunguza Idadi Ya Talaka

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

كِتَابُ الفَرْق بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ

Kitabu Cha Kutengana Mke Na Mume 

طَلَاقٌ رَجْعِي

Talaka Rejea 

Alhidaaya.com 

27: Talaka Rejea Inapunguza Idadi Ya Talaka:

Mume kama tujuavyo anamiliki talaka tatu tu kwa mkewe.  Talaka hizi zinapungua kwa kila talaka anayoitoa, ni sawa iwe talaka rejea "طَلَاقٌ رَجْعِيْ", au talaka mtengano "طَلَاقٌ بَائِنٌ", hata kama mume atamrejea mkewe akiwa ndani ya eda, itahesabika tu.  Hivyo basi, ikiwa amempa talaka moja kisha akamrejea, basi zitakuwa zimebakia mbili.  Na ikiwa amempa ya pili kisha akamrejea, basi itakuwa imebakia moja.  Haya ndiyo waliyoitafikiana kwayo 'Ulamaa kutokana na Kauli Yake Ta'aalaa: 

"الطَّلَاقُ مَرَّتَانِ ۖ فَإِمْسَاكٌ بِمَعْرُوفٍ أَوْ تَسْرِيحٌ بِإِحْسَانٍ"

"Talaka ni mara mbili. Hivyo kuzuia kwa mujibu wa shariy’ah au kuachia kwa ihsaan".  [Al-Baqarah: 229]