Skip to main content

11B-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: كِتَابُ الفَرْق بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ Kitabu Cha Kutengana Mke Na Mume: طَلَاقٌ رَجْعِي Talaka Rejea14-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Kutengana Mke Na Mume: Talaka Rejea: Ni Wakati Gani Talaka Mtengano, Utengano Mdogo Inatokea?

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

كِتَابُ الفَرْق بَيْنَ الزَّوْجَيْنِ

Kitabu Cha Kutengana Mke Na Mume 

طَلَاقٌ رَجْعِي

Talaka Rejea 

Alhidaaya.com 

30:  Ni Wakati Gani Talaka Mtengano, Utengano Mdogo  "بَائِنٌ بَيْنُونَةٌ صُغْرَى" Inatokea? 

Talaka hii inatokea katika hali zifuatazo:

1-  Mume akimtaliki mkewe kabla hajamuingilia.  Allaah Ta'aalaa Anasema: 

"يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا نَكَحْتُمُ الْمُؤْمِنَاتِ ثُمَّ طَلَّقْتُمُوهُنَّ مِن قَبْلِ أَن تَمَسُّوهُنَّ فَمَا لَكُمْ عَلَيْهِنَّ مِنْ عِدَّةٍ تَعْتَدُّونَهَا"

"Enyi walioamini!  Mnapofunga nikaah na Waumini wa kike, kisha mkawataliki kabla ya kujimai nao, basi hamna juu yao eda yoyote mtakayohesabu".  [Al-Ahzaab: 49]

Aayah hapa inaashiria kwamba mwanamke aliyetalikiwa kabla hajaingiliwa, basi hana eda, na mume aliyemtaliki hana mamlaka ya kumrejea, na talaka hiyo haiwi talaka rejea"رَجْعِي" , bali ni talaka mtengano "بَائِنٌ".  Hii ni itifaki ya 'Ulamaa wote. 

2-  Mke akitaka mwenyewe kujivua na ndoa (kufanya khulu "خُلْعٌ")

Jumhuwr ya ‘Ulamaa wanasema kwamba talaka hii ambayo mke humlipa mumewe pesa ili amwache, inakuwa ni talaka mtengano "بَائِنٌ"

Ninasema:  Khulu  "خُلْعٌ"inazingatiwa kuwa talaka mtengano "بَائِنٌ" kwa maana kwamba mume anaweza kumrejesha tena mkewe baadaye kwenye fungamano la ndoa ikiwa mke ataridhia, kwa ndoa mpya na kwa mahari mapya.  Hili ni sahihi kabisa na hakuna tatizo lolote. 

Ama ikiwa kwa maana ya talaka moja anayohesabiwa mume katika tatu, hili si sahihi, bali lililo sahihi ni kwamba khulu ni mke mwenyewe kuomba kufuta ndoa yake (toka kwa mume), na si talaka, hivyo basi haihesabiwi kuwa ni moja katika talaka tatu kwa mujibu wa kauli ya Jumhuwr.  Allaah Ndiye Ajuaye zaidi". 

3-  Baadhi ya hali maalum za kumfanya mke na mume kuachana:

Ni kama kuwepo kasoro (za kimwili, kisaikolojia, kimaumbile) au madhara, au mume kumuapia mkewe kwamba hatomuingilia kwa muda wa miezi minne ("Iylaa" "إِيْلاءُ"[hadi muda huo ukapita bila kumuingilia].