Skip to main content

10A-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: كتاب الزواج Kitabu Cha Ndoa22-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Mwanamke Wa Kiislamu Ni Haramu Kuolewa Na Kafiri

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

كِتَابُ الزَّوَاجِ

Kitabu Cha Ndoa

Alhidaaya.com 

22-Mwanamke Wa Kiislamu Ni Haramu Kuolewa Na Kafiri:

Hii ni sawa ikiwa mwanaume ni katika Ahlul Kitaab au dini nyingine kutokana na Neno Lake Ta’aalaa:

"وَلَا تَنكِحُوا الْمُشْرِكَاتِ حَتَّىٰ يُؤْمِنَّ ۚ وَلَأَمَةٌ مُّؤْمِنَةٌ خَيْرٌ مِّن مُّشْرِكَةٍ وَلَوْ أَعْجَبَتْكُمْ ۗ وَلَا تُنكِحُوا الْمُشْرِكِينَ حَتَّىٰ يُؤْمِنُوا ۚ وَلَعَبْدٌ مُّؤْمِنٌ خَيْرٌ مِّن مُّشْرِكٍ وَلَوْ أَعْجَبَكُمْ ۗ أُولَـٰئِكَ يَدْعُونَ إِلَى النَّارِ ۖ وَاللَّـهُ يَدْعُو إِلَى الْجَنَّةِ وَالْمَغْفِرَةِ بِإِذْنِهِ"

“Na wala msiwaoe wanawake washirikina mpaka waamini.  Na mjakazi Muumini ni bora kuliko mshirikina japo akikupendezeni.  Na wala msiwaozeshe (wanawake wa Kiislamu) wanaume washirikina mpaka waamini.  Na mtumwa Muumini ni bora kuliko mshirikina japo akikupendezeni.  Hao wanaitia katika moto na Allaah Anaitia katika Jannah na maghfirah kwa Idhini Yake”.  [Al-Baqarah: 221]