23-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Ndoa: Wanawake Walioharamika Kwa Muda: vi-Mwanamke Mzinifu Mpaka Atubie

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الزَّوَاجِ

 

Kitabu Cha Ndoa

  

Alhidaaya.com 

 

 

 

23-Wanawake Walioharamika Kwa Muda: vi-Mwanamke Mzinifu Mpaka Atubie:

 

 

Mwanamke huyu hedhi moja inatosha kujua kama ana kitu tumboni au la.  Allaah Ta’aalaa Amesema:

 

"الزَّانِي لَا يَنكِحُ إِلَّا زَانِيَةً أَوْ مُشْرِكَةً وَالزَّانِيَةُ لَا يَنكِحُهَا إِلَّا زَانٍ أَوْ مُشْرِكٌ ۚ وَحُرِّمَ ذَٰلِكَ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ"

 

Mwanamme mzinifu hafungi nikaah isipokuwa na mwanamke mzinifu au mwanamke mshirikina, na mwanamke mzinifu haolewi isipokuwa na mwanamme mzinifu au mshirikina.  Na imeharamishwa hivyo kwa Waumini”.   [An-Nuwr: 03]

 

‘Ulamaa wamekhitilafiana katika ufahamu wa aayah hii tukufu.  Ni kwamba je, aayah inabeba dhana ya kwamba jambo hili ni baya na si zuri, au inabeba dhana ya kuharamisha?  Na je neno “hivyo” katika aayah linarejea kwenye zinaa au ndoa?

 

Jumhuwr kinyume na Ahmad bin Hanbali wanaona kwamba dhana ya aayah inabeba ashirio la kwamba jambo hilo si zuri  na ni baya, lakini si kuliharamisha. Na kwa msingi huu, wamejuzisha mtu kumwoa mwanamke mzinifu kwa sababu hizi zifuatazo walizozitaja:

 

1-  Mwonekano wa aayah sio unaokusudiwa, kwa kuwa kama utachukuliwa kama ulivyo, basi italazimu kusema kwamba mwanaume mzinifu wa Kiislamu anafaa kumwoa mwanamke mpagani, na mwanamke mzinifu wa Kiislamu anafaa kuolewa na mwanaume wa kipagani, na haya mawili hayaruhusiwi kama ilivyotangulia nyuma.

 

 

2-  Wametolea dalili Hadiyth ya mtu ambaye alimweleza Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusu tabia ya mkewe akimwambia:

 

" إِنَّهَا لاَ تَرُدُّ يَدَ لاَمِسٍ، فقَالَ له: طَلِّقْهَا‏.‏ فقَالَ: إِنِّي لاَ أَصْبِرُ عَنْهَا، ‏فَقَالَ: ‏فَأَمْسِكْهَا"

 

“Yeye hamkatai mtu yeyote anayemgusa.  Rasuli akamwambia:  Mwache.  Akasema: Siwezi kuishi bila kuwa naye.  Akamwambia:  Basi endelea kuishi naye”.  [Hasanun Bitwuruqihi.  Imekharijiwa na Abu Daawuwd (2049), An-Nasaaiy (6/170) na Al-Bayhaqiy (7/154-155)]

 

Ninasema:  “Aayah kubeba dhana ya kuharamisha kumwoa mwanamke mzinifu (kahaba) kunatiliwa nguvu na sababu ya kuteremka aayah yenyewe.  Sababu yenyewe ni hii:

 

أَنَّ مَرْثَدَ بْنَ أَبِي مَرْثَدٍ وَكَانَ رَجُلاً يَحْمِلُ الأَسْرَى مِنْ مَكَّةَ حَتَّى يَأْتِيَ بِهِمُ الْمَدِينَةَ، قَالَ: وَكَانَتِ امْرَأَةٌ بَغِيٌّ بِمَكَّةَ يُقَالُ لَهَا عَنَاقُ وَكَانَتْ صَدِيقَةً لَهُ وَإِنَّهُ كَانَ وَعَدَ رَجُلاً مِنْ أُسَارَى مَكَّةَ يَحْمِلُهُ قَالَ : فَجِئْتُ حَتَّى انْتَهَيْتُ إِلَى ظِلِّ حَائِطٍ مِنْ حَوَائِطِ مَكَّةَ فِي لَيْلَةٍ مُقْمِرَةٍ ‏.‏ قَالَ: فَجَاءَتْ عَنَاقُ فَأَبْصَرَتْ سَوَادَ ظِلِّي بِجَنْبِ الْحَائِطِ، فَلَمَّا انْتَهَتْ إِلَىَّ عَرَفَتْهُ فَقَالَتْ: مَرْثَدُ فَقُلْتُ مَرْثَدُ ‏.‏ فَقَالَتْ: مَرْحَبًا وَأَهْلاً هَلُمَّ فَبِتْ عِنْدَنَا اللَّيْلَةَ ‏.‏ قَالَ قُلْتُ: يَا عَنَاقُ حَرَّمَ اللَّهُ الزِّنَا ‏.‏ قَالَتْ: يَا أَهْلَ الْخِيَامِ هَذَا الرَّجُلُ يَحْمِلُ أَسْرَاكُمْ ‏.‏ قَالَ: فَتَبِعَنِي ثَمَانِيَةٌ، وَسَلَكْتُ الْخَنْدَمَةَ، فَانْتَهَيْتُ إِلَى كَهْفٍ أَوْ غَارٍ فَدَخَلْتُ، فَجَاءُوا حَتَّى قَامُوا عَلَى رَأْسِي فَبَالُوا فَطَلَّ بَوْلُهُمْ عَلَى رَأْسِي وَأَعْمَاهُمُ اللَّهُ عَنِّي ‏.‏ قَالَ: ثُمَّ رَجَعُوا وَرَجَعْتُ إِلَى صَاحِبِي فَحَمَلْتُهُ وَكَانَ رَجُلاً ثَقِيلاً حَتَّى انْتَهَيْتُ إِلَى الإِذْخِرِ فَفَكَكْتُ عَنْهُ كَبْلَهُ فَجَعَلْتُ أَحْمِلُهُ وَيُعِينُنِي حَتَّى قَدِمْتُ الْمَدِينَةَ، فَأَتَيْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ  فَقُلْتُ: يَا رَسُولَ اللَّهِ! أَنْكِحُ عَنَاقًا مَرَّتَيْنِ، فَأَمْسَكَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ  وَلَمْ يَرُدَّ عَلَىَّ شَيْئًا حَتَّى نَزَلَتِ ‏:‏ الزَّانِي لاَ يَنْكِحُ إِلاَّ زَانِيَةً أَوْ مُشْرِكَةً وَالزَّانِيَةُ لاَ يَنْكِحُهَا إِلاَّ زَانٍ أَوْ مُشْرِكٌ وَحُرِّمَ ذَلِكَ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ ،  فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ  : ‏يَا مَرْثَدُ الزَّانِي لاَ يَنْكِحُ إِلاَّ زَانِيَةً أَوْ مُشْرِكَةً وَالزَّانِيَةُ لاَ يَنْكِحُهَا إِلاَّ زَانٍ أَوْ مُشْرِكٌ فَلاَ تَنْكِحْهَا". هَذَا حَدِيثٌ حَسَنٌ غَرِيبٌ لاَ نَعْرِفُهُ إِلاَّ مِنْ هَذَا الْوَجْهِ.‏

 

Ametuhadithia ‘Abdu bin Humayd, ametuhadithia Rawh bin ‘Ubaadah toka kwa ‘Ubaydullaa bin Al-Akhnas amesema:  Amenieleza ‘Amri bin Shu’ayb akipokea toka kwa baba yake toka kwa babu yake aliyesema:  Kulikuwa na mtu ajulikanaye kama Marthad.  Kazi yake ilikuwa ni kuwabeba na kuwatorosha mateka toka Makkah kuwaleta Madiynah.  Na hapo Makkah alikuwepo mwanamke kahaba aitwaye ‘Anaaq ambaye alikuwa ni hawara yake Marthad (kabla hajasilimu). Marthad alikuwa amemwahidi mtu mmoja katika mateka wa Makkah kuwa atambeba (kumtorosha).  [Marthad anasema]:  Nikaja hadi nikaishilia katika kivuli cha kuta kati ya kuta za Makkah katika usiku angavu wa nuru ya mwezi.  ‘Anaaq akaja, akaona weusi wa kivuli changu pembeni ya ukuta.  Aliponifikia, alinitambua akasema:  Ni Marthad!  Nami nikasema ni (mimi) Marthad.  Akasema:  Karibu sana, njoo basi ulale kwetu usiku huu.  Nikamwambia:  Ee ‘Anaaq!  Allaah Ameharamisha zinaa!  (Hapo hapo) akapiga ukelele na kusema: Enyi watu wa makhema!  Huyu hapa mtu anayewatorosha mateka wenu.  Watu wanane wakaniandama, nikapita Al-Khandamah, nikakimbilia pangoni na kuingia.  Wakaja mpaka wakasimama juu ya kichwa changu (mdomo wa pango) lakini Allaah Aliwaziba macho wasiweze kuniona. Kisha wakaondoka, nami nikarudi kwa mwenzangu, nikambeba, naye alikuwa mzito.  Nikamfuata mwingine, nikamfungua minyonyoro yake, nikaanza kumbeba huku akinilemea na kunichosha mpaka nikawasili Madiynah.  Nikamwendea Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)   nikamwambia:  Ee Rasuli wa Allaah!  Je, naweza kumwoa ‘Anaaq?  Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  akanyamaza, hakujibu kitu mpaka iliposhuka:

 

"الزَّانِي لَا يَنكِحُ إِلَّا زَانِيَةً أَوْ مُشْرِكَةً وَالزَّانِيَةُ لَا يَنكِحُهَا إِلَّا زَانٍ أَوْ مُشْرِكٌ ۚ وَحُرِّمَ ذَٰلِكَ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ"

 

“Mwanamme mzinifu hafungi nikaah isipokuwa na mwanamke mzinifu au mwanamke mshirikina, na mwanamke mzinifu haolewi isipokuwa na mwanamme mzinifu au mshirikina.  Na imeharamishwa hivyo kwa Waumini”.  [An Nuwr (24:3)]

 

Na hapo Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  akamwambia:  Ee Marthad!  Mwanamme mzinifu hafungi nikaah isipokuwa na mwanamke mzinifu au mwanamke mshirikina; na mwanamke mzinifu haolewi isipokuwa na mwanamme mzinifu au mshirikina, basi usimwoe:.  [At-Tirmidhiy Mujallad Wa Ukurasa wa 152]

 

Hadiyth hii ni Hasan Ghariyb, haijulikani isipokuwa kwa picha hii.

 

Toka kwa Abu Hurayrah:  “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

"لَا يَنْكِحُ اَلزَّانِي اَلْمَجْلُودُ إِلَّا مِثْلَهُ "

 

“Mzinifu aliyepatikana na kosa la zinaa na akachapwa viboko, haoi isipokuwa mfano wake”.  [Hadiyth Hasan.  Imekharijiwa na Abu Daawuwd (2052), Al-Haakim (2/193) na Al-Bayhaqiy (7/156)]

 

Hata yule pia mwenye sifa ya mwenendo huu mchafu mitaani, asiruhusiwe kuoa binti anayejiheshimu.

 

Na haya ni madhehebu ya Qataadah, Is-Haaq, Ibn ‘Ubayd, na Ahmad, na Sheikh wa Uislamu ameyakhitari.

 

 

Share