Surat Yaasiyn, Je, Inafaa Kumsomea Mtu Anayekata Roho?

 

Suwrah Yaasiyn, Je, Inafaa Kumsomea Mtu Anayekata Roho?

 

Alhidaaya.com

 

SWALI:

 

Assalam aleykum, natumaini hamjambo  kwa hiyo tunashukuru Allaah anasaidia.

Napenda kuuliza swali, Suwrah-Yaasiyn inafaa kumsomea mtu akiwa anataka kukata roho (yaani sakarat mauti) au kama mtu amekufa kumsomea pia inafaa, au kama wewe mwenyewe unayekata roho pia inafaa,naomba jibu inshaalah mungu atakuwezesha.

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Tunakushukuru kwa kuuliza swali hili muhimu kuhusu Suwrah Yaasiyn ambayo imeenea katika mujtama'a wetu kuitumia na kuitukuza suwrah hii pekee kuliko suwrah zingine katika Qur'aan au kuitumia mahali pasipofaa.

 

Hadiyth inayosema, "Wasomeeni maiti wenu (wanaokata roho) Yaasiyn" ni Hadiyth dhaifu haina mashiko yoyote.

 
Hivyo, hakuna uthibitisho wa Hadiythi yoyote iliyo sahihi kuwa zimetajwa fadhila za Suwrah hii.  Na kwa kupata maelezo zaidi tafadhali ingia katika kiungo kifuatacho upate ushahidi wa hizo Hadiyth zilizokuwa dhaifu kuhusu Suwrah hii
.

 

Surat Yaasiyn Na Al-An'aam Zina Fadhila?

 

 

Na Allaah Anajua Zaidi

 

 

Share