093 - Adh-Dhuhaa

 

   الضُّحى

 

093-Adh-Dhuhaa

 

093-Adhw-Dhwuhaa: Utangulizi Wa Suwrah

 

 Alhidaaya.com

 

 

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

 

 

وَالضُّحَىٰ ﴿١﴾

1. Naapa kwa dhuha (jua linapopanda).[1]

   

 

 

وَاللَّيْلِ إِذَا سَجَىٰ ﴿٢﴾

2. Na Naapa kwa usiku unapotanda kiza na kutulia.

 

 

مَا وَدَّعَكَ رَبُّكَ وَمَا قَلَىٰ ﴿٣﴾

3. Rabb wako Hakukutelekeza na wala Hakukuchukia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم).

 

 

وَلَلْآخِرَةُ خَيْرٌ لَّكَ مِنَ الْأُولَىٰ ﴿٤﴾

4. Na bila shaka Aakhirah ni kheri zaidi kwako kuliko ya awali (dunia).

 

 

وَلَسَوْفَ يُعْطِيكَ رَبُّكَ فَتَرْضَىٰ ﴿٥﴾

5. Na bila shaka Rabb wako Atakupa na utaridhika.

 

 

أَلَمْ يَجِدْكَ يَتِيمًا فَآوَىٰ ﴿٦﴾

6. Je, kwani Hakukukuta yatima, Akakupa makazi?

 

 

وَوَجَدَكَ ضَالًّا فَهَدَىٰ ﴿٧﴾

7. Na Akakukuta hujui lolote (kuhusu Kitabu wala Iymaan), kisha Akakuongoza?

 

 

 

وَوَجَدَكَ عَائِلًا فَأَغْنَىٰ ﴿٨﴾

8. Na Akakukuta mhitaji, Akakutosheleza?

 

 

فَأَمَّا الْيَتِيمَ فَلَا تَقْهَرْ ﴿٩﴾

9. Kwa hivyo basi yatima usimuonee.

 

 

وَأَمَّا السَّائِلَ فَلَا تَنْهَرْ ﴿١٠﴾

10. Na ama mwombaji, basi usimkaripie.

 

 

وَأَمَّا بِنِعْمَةِ رَبِّكَ فَحَدِّثْ ﴿١١﴾

11. Na ama Neema ya Rabb wako, basi ihadithie.

 

 

 

 

Share