094 - Ash-Sharh
الشَّرْح
094-Ash-Sharh
094-Ash-Sharh: Utangulizi Wa Suwrah
بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ
أَلَمْ نَشْرَحْ لَكَ صَدْرَكَ ﴿١﴾
1. Je, kwani Hatukukunjulia kifua chako kukubainishia (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم)?[1]
وَوَضَعْنَا عَنكَ وِزْرَكَ ﴿٢﴾
2. Na Tukakuondolea mzigo wako (wa dhambi)?[2]
الَّذِي أَنقَضَ ظَهْرَكَ ﴿٣﴾
3. Ambao ulielemea mgongo wako?
وَرَفَعْنَا لَكَ ذِكْرَكَ ﴿٤﴾
4. Na Tukakutukuzia kutajwa kwako?[3]
فَإِنَّ مَعَ الْعُسْرِ يُسْرًا ﴿٥﴾
5. Basi hakika pamoja na kila ugumu kuna wepesi.[4]
إِنَّ مَعَ الْعُسْرِ يُسْرًا ﴿٦﴾
6. Hakika pamoja na kila ugumu kuna wepesi.
فَإِذَا فَرَغْتَ فَانصَبْ ﴿٧﴾
7. Basi utakapopata faragha fanya juhudi katika ibaada.
وَإِلَىٰ رَبِّكَ فَارْغَب ﴿٨﴾
8. Na kwa ajili ya Rabb wako, ongeza utashi zaidi (wa ibaada).
[1] Kisa Cha Kupasuliwa Kifua Chake Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):
Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alibaki katika kijiji cha Bani Sa’ad mpaka alipotimia umri wa miaka mine au mitano wakati kilipotokea kisa cha kupasuliwa kifua. Hadiyth ifuatayo inaelezea:
عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم أَتَاهُ جِبْرِيلُ صلى الله عليه وسلم وَهُوَ يَلْعَبُ مَعَ الْغِلْمَانِ فَأَخَذَهُ فَصَرَعَهُ فَشَقَّ عَنْ قَلْبِهِ فَاسْتَخْرَجَ الْقَلْبَ فَاسْتَخْرَجَ مِنْهُ عَلَقَةً فَقَالَ هَذَا حَظُّ الشَّيْطَانِ مِنْكَ . ثُمَّ غَسَلَهُ فِي طَسْتٍ مِنْ ذَهَبٍ بِمَاءِ زَمْزَمَ ثُمَّ لأَمَهُ ثُمَّ أَعَادَهُ فِي مَكَانِهِ وَجَاءَ الْغِلْمَانُ يَسْعَوْنَ إِلَى أُمِّهِ - يَعْنِي ظِئْرَهُ - فَقَالُوا إِنَّ مُحَمَّدًا قَدْ قُتِلَ . فَاسْتَقْبَلُوهُ وَهُوَ مُنْتَقَعُ اللَّوْنِ . قَالَ أَنَسٌ وَقَدْ كُنْتُ أَرَى أَثَرَ ذَلِكَ الْمِخْيَطِ فِي صَدْرِهِ .
Amesimulia Anas Bin Maalik (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alipokuwa akicheza na watoto wenzake alijiwa na Jibriyl (عليه السّلام), akamchukua na kumlaza chini, kisha akampasua kifua chake na kuutoa nje moyo wake na kutoa kutoka ndani ya moyo huo kipande cha damu iliyoganda. Akamwambia: Hii ni sehemu ya shaytwaan kwako. Kisha akauosha kwa maji ya Zamzam yaliyokuwemo ndani ya chombo cha dhahabu, akauunganisha, kisha akaurudisha moyo mahali pake. Watoto waliokuwa wakicheza pamoja naye walikimbia mpaka nyumbani kwa mnyonyeshaji wake Bibi Haliymah (رضي الله عنها) wakamwambia: “Muhammad kesha uliwa!” Walipomrudia walimkuta amekaa, mzima hana chochote isipokuwa rangi ya uso wake ilikuwa imebadilika na kugeuka nyeupe.” [Muslim]
[2] Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Kufutiwa Madhambi Yake:
Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):
لِّيَغْفِرَ لَكَ اللَّـهُ مَا تَقَدَّمَ مِن ذَنبِكَ وَمَا تَأَخَّرَ
Ili Allaah Akughufurie yale yaliyotangulia katika madhambi yako na yale yanayofuatia. [Al-Fat-h (48:2)]
Bonyeza pia kiungo kifuatacho:
Lakini juu ya hivyo, Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa akiomba maghfirah kwa Allaah (سبحانه وتعالى) zaidi ya mara sabiini kila siku kama ilivyothibiti yeye kusema hivyo katika Hadiyth ifuatayo:
عن أبي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه : سَمِعْتُ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ يَقُولُ : ((وَاللَّهِ إِنِّي لاَسْتَغْفِرُ اللَّهَ وَأَتُوبُ إِلَيْهِ فِي الْيَوْمِ أَكْثَرَ مِنْ سَبْعِينَ مَرَّةً)) رواه البخاري (6307)
Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Nimemsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: “Wa-Allaahi mimi naomba maghfirah kwa Allaah na kutubia Kwake zaidi ya mara sabiini kwa siku.” [Al-Bukhaariy]
[3] Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) Anatajwa Kila Mara:
Bonyeza viungo vifuatavyo kupata faida:
32-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Hatajwi Ila Anaswaliwa (Anaombewa Rahmah Na Amani)
33-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Ana Ujira Usiokatika Anasifika Na Maarufu Mno
Rejea pia Al-Qalam (68:3).
[4] Katika Kila Gumu Allaah Anajalia Wepesi:
Kauli yake Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kumwambia ‘Abdullaah bin ‘Abbaas (رضي الله عنهما) katika Hadiyth ifuatayo:
((احْفَظِ الله تَجِدْهُ أَمَامَكَ، تَعرَّفْ إِلَى اللهِ في الرَّخَاءِ يَعْرِفكَ في الشِّدَّةِ، وَاعْلَمْ: أنَّ مَا أَخْطَأكَ لَمْ يَكُنْ لِيُصِيبكَ، وَمَا أصَابَكَ لَمْ يَكُنْ لِيُخْطِئَكَ، وَاعْلَمْ: أنَّ النَّصْرَ مَعَ الصَّبْرِ، وَأَنَّ الفَرَجَ مَعَ الكَرْبِ، وَأَنَّ مَعَ العُسْرِ يُسْرًا))
“Mhifadhi Allaah utamkuta Yupo mbele yako. Mjue Allaah katika raha Naye Atakujua katika shida. Ujue kuwa, lililokukosa halikuwa ni lenye kukupata, na lililokusibu halikuwa ni lenye kukukosa. Ujue kuwa nusura ipo pamoja na subira, faraja ipo pamoja na dhiki, na kwenye uzito kuna wepesi.” [At-Tirmidhiy]