003 - Aal-'Imraan

 

آل عِمْران

003-Aal-‘Imraan

 

003-Aal-'Imraan: Utangulizi Wa Suwrah

 

Alhidaaya.com

 

 

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

الم ﴿١﴾

 

1. Alif Laam Miym.[1]

 

 

 

اللَّـهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْحَيُّ الْقَيُّومُ ﴿٢﴾

2. Allaah, hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye, Al-Hayyu (Aliye Hai daima) Al-Qayyuwm (Msimamia kila kitu).[2]

 

 

 نَزَّلَ عَلَيْكَ الْكِتَابَ بِالْحَقِّ مُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ وَأَنزَلَ التَّوْرَاةَ وَالْإِنجِيلَ ﴿٣﴾

3. Amekuteremshia Kitabu (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) kwa haki kinachosadikisha yaliyo kabla yake na Akateremsha Tawraat na Injiyl.

 

 

مِن قَبْلُ هُدًى لِّلنَّاسِ وَأَنزَلَ الْفُرْقَانَ ۗ إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا بِآيَاتِ اللَّـهِ لَهُمْ عَذَابٌ شَدِيدٌ ۗ وَاللَّـهُ عَزِيزٌ ذُو انتِقَامٍ ﴿٤﴾

4. Kabla (ya kuteremshwa Qur-aan), iwe ni mwongozo kwa watu na Akateremsha pambanuo (la haki na baatwil). Hakika wale waliokufuru Aayaat (na Ishara, Hoja, Dalili) za Allaah watapata adhabu kali. Na Allaah Ni Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Kulipiza.

 

 

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَخْفَىٰ عَلَيْهِ شَيْءٌ فِي الْأَرْضِ وَلَا فِي السَّمَاءِ ﴿٥﴾

5. Hakika Allaah Hakifichiki Kwake chochote katika ardhi wala katika mbingu. 

 

 

 هُوَ الَّذِي يُصَوِّرُكُمْ فِي الْأَرْحَامِ كَيْفَ يَشَاءُ ۚ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿٦﴾

6. Yeye Ndiye Anayekusawirini umbo katika matumbo ya uzazi vile Atakavyo. Hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye, Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.

 

 

 

هُوَ الَّذِي أَنزَلَ عَلَيْكَ الْكِتَابَ مِنْهُ آيَاتٌ مُّحْكَمَاتٌ هُنَّ أُمُّ الْكِتَابِ وَأُخَرُ مُتَشَابِهَاتٌ ۖ فَأَمَّا الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِمْ زَيْغٌ فَيَتَّبِعُونَ مَا تَشَابَهَ مِنْهُ ابْتِغَاءَ الْفِتْنَةِ وَابْتِغَاءَ تَأْوِيلِهِ ۗ وَمَا يَعْلَمُ تَأْوِيلَهُ إِلَّا اللَّـهُ ۗ وَالرَّاسِخُونَ فِي الْعِلْمِ يَقُولُونَ آمَنَّا بِهِ كُلٌّ مِّنْ عِندِ رَبِّنَا ۗ وَمَا يَذَّكَّرُ إِلَّا أُولُو الْأَلْبَابِ ﴿٧

7. Yeye Ndiye Aliyekuteremshia Kitabu. Humo mna Aayaat zenye maana wazi, hizo ndio msingi wa Kitabu, na nyinginezo zisizokuwa wazi maana zake. Basi wale ambao katika nyoyo zao mna upotovu hufuata zile zisizokuwa wazi maana zake kutafuta fitnah (upotofu)[3] na kutafuta maana zake zilizofichika, na hakuna ajuae maana zake isipokuwa Allaah. Na wenye msingi madhubuti katika ilimu husema: Tumeziamini, zote ni kutoka kwa Rabb wetu. Na hawakumbuki ila wenye akili.[4]

 

 

رَبَّنَا لَا تُزِغْ قُلُوبَنَا بَعْدَ إِذْ هَدَيْتَنَا وَهَبْ لَنَا مِن لَّدُنكَ رَحْمَةً ۚ إِنَّكَ أَنتَ الْوَهَّابُ ﴿٨﴾

8. (Husema): Rabb wetu!  Usizipotoe nyoyo zetu baada ya kuwa Umetuhidi na Tutunukie kutoka Kwako Rehma. Hakika Wewe Ni Mwingi wa Kutunuku na Kuneemesha.

 

 

رَبَّنَا إِنَّكَ جَامِعُ النَّاسِ لِيَوْمٍ لَّا رَيْبَ فِيهِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ لَا يُخْلِفُ الْمِيعَادَ ﴿٩﴾ 

9. Rabb wetu! Hakika Wewe Ni Mkusanyaji watu Siku isiyo na shaka ndani yake. Hakika Allaah Havunji miadi.

 

 

 إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا لَن تُغْنِيَ عَنْهُمْ أَمْوَالُهُمْ وَلَا أَوْلَادُهُم مِّنَ اللَّـهِ شَيْئًا ۖ وَأُولَـٰئِكَ هُمْ وَقُودُ النَّارِ ﴿١٠﴾

10. Hakika wale waliokufuru hazitowafaa kitu mali zao wala watoto wao mbele ya Allaah, na hao ndio kuni za moto.

 

 

كَدَأْبِ آلِ فِرْعَوْنَ وَالَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۚ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا فَأَخَذَهُمُ اللَّـهُ بِذُنُوبِهِمْ ۗ وَاللَّـهُ شَدِيدُ الْعِقَابِ ﴿١١﴾

11. Kama mwenendo wa watu wa Firawni na wale waliokuwa kabla yao. Walikadhibisha Aayaat (Ishara, Dalili) Zetu na Allaah Akawaadhibu kwa madhambi yao, na Allaah Ni Mkali wa Kuakibu.[5]

 

 

قُل لِّلَّذِينَ كَفَرُوا سَتُغْلَبُونَ وَتُحْشَرُونَ إِلَىٰ جَهَنَّمَ ۚ وَبِئْسَ الْمِهَادُ ﴿١٢

12. Waambie waliokufuru: Mtashindwa na mtakusanywa katika Jahannam, na ni pabaya mno mahala hapo pa kupumzika.

 

 

 قَدْ كَانَ لَكُمْ آيَةٌ فِي فِئَتَيْنِ الْتَقَتَا ۖ فِئَةٌ تُقَاتِلُ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَأُخْرَىٰ كَافِرَةٌ يَرَوْنَهُم مِّثْلَيْهِمْ رَأْيَ الْعَيْنِ ۚ وَاللَّـهُ يُؤَيِّدُ بِنَصْرِهِ مَن يَشَاءُ ۗ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَعِبْرَةً لِّأُولِي الْأَبْصَارِ ﴿١٣﴾

13. Kwa hakika ilikuwa ni Aayah (Dalili, Funzo na Zingatio) kwenu katika makundi mawili yalipokutana (Vita vya Badr). Kundi linapigana katika Njia ya Allaah na jingine la makafiri. Wanawaona (Waislamu) mara mbili yao kwa mtazamo wa macho. Na Allaah Humsaidia kwa Nusura Yake Amtakaye. Hakika katika hayo bila shaka kuna mazingatio kwa wenye utambuzi.

 

 

زُيِّنَ لِلنَّاسِ حُبُّ الشَّهَوَاتِ مِنَ النِّسَاءِ وَالْبَنِينَ وَالْقَنَاطِيرِ الْمُقَنطَرَةِ مِنَ الذَّهَبِ وَالْفِضَّةِ وَالْخَيْلِ الْمُسَوَّمَةِ وَالْأَنْعَامِ وَالْحَرْثِ ۗ ذَٰلِكَ مَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا ۖ وَاللَّـهُ عِندَهُ حُسْنُ الْمَآبِ ﴿١٤﴾

14. Watu wamepambiwa huba ya matamanio ya kupenda wanawake na watoto, mirundi ya mali iliyolimbikizwa ya dhahabu na fedha, farasi wenye chapa ya aina bora, wanyama wa mifugo na mashamba. Hayo ni starehe za uhai wa dunia, na marejeo mazuri yako Kwake Allaah.

 

 

 قُلْ أَؤُنَبِّئُكُم بِخَيْرٍ مِّن ذَٰلِكُمْ ۚ لِلَّذِينَ اتَّقَوْا عِندَ رَبِّهِمْ جَنَّاتٌ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا وَأَزْوَاجٌ مُّطَهَّرَةٌ وَرِضْوَانٌ مِّنَ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ بَصِيرٌ بِالْعِبَادِ ﴿١٥﴾

15. Sema: Je, nikujulisheni yaliyo bora kuliko hayo? Kwa wale waliokuwa na taqwa, watapata kwa Rabb wao Jannaat zipitazo chini yake mito, wadumu humo, pamoja na wake waliotakasika na Radhi kutoka kwa Allaah. Na Allaah Ni Mwenye Kuwaona vyema waja.

 

 

الَّذِينَ يَقُولُونَ رَبَّنَا إِنَّنَا آمَنَّا فَاغْفِرْ لَنَا ذُنُوبَنَا وَقِنَا عَذَابَ النَّارِ﴿١٦﴾ 

16. Wale wasemao: Rabb wetu! Hakika sisi tumeamini, basi Tughufurie madhambi yetu na Tukinge na adhabu ya moto.

 

 

 الصَّابِرِينَ وَالصَّادِقِينَ وَالْقَانِتِينَ وَالْمُنفِقِينَ وَالْمُسْتَغْفِرِينَ بِالْأَسْحَارِ﴿١٧﴾

17. Wenye kuvuta subira, wasemao kweli, watiifu, watoaji mali katika Njia ya Allaah na waombao maghfirah kabla ya Alfajiri.[6]

 

 

شَهِدَ اللَّـهُ أَنَّهُ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ وَالْمَلَائِكَةُ وَأُولُو الْعِلْمِ قَائِمًا بِالْقِسْطِ ۚ لَا إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿١٨﴾

18. Allaah Ameshuhudia kwamba hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye, na (pia) Malaika na wenye ilimu wameshuhudia hilo. Na Yeye mbali ya hilo, Anasifika kwa uadilifu. Hapana mwabudiwa wa haki ila Yeye Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.

 

 

إِنَّ الدِّينَ عِندَ اللَّـهِ الْإِسْلَامُ ۗ وَمَا اخْتَلَفَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ إِلَّا مِن بَعْدِ مَا جَاءَهُمُ الْعِلْمُ بَغْيًا بَيْنَهُمْ ۗ وَمَن يَكْفُرْ بِآيَاتِ اللَّـهِ فَإِنَّ اللَّـهَ سَرِيعُ الْحِسَابِ ﴿١٩﴾

19. Hakika Dini mbele ya Allaah ni Uislamu.[7] Na hawakukhitilafiana wale waliopewa Kitabu ila baada ya kuwajia ilimu kutokana na baghi[8] (chuki na hasadi) iliyotamalaki baina yao. Na atakayekanusha Aayaat (na Ishara, Dalili) za Allaah basi hakika Allaah Ni Mwepesi wa Kuhesabu.

 

 

 فَإِنْ حَاجُّوكَ فَقُلْ أَسْلَمْتُ وَجْهِيَ لِلَّـهِ وَمَنِ اتَّبَعَنِ ۗ وَقُل لِّلَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ وَالْأُمِّيِّينَ أَأَسْلَمْتُمْ ۚ فَإِنْ أَسْلَمُوا فَقَدِ اهْتَدَوا ۖ وَّإِن تَوَلَّوْا فَإِنَّمَا عَلَيْكَ الْبَلَاغُ ۗ وَاللَّـهُ بَصِيرٌ بِالْعِبَادِ ﴿٢٠﴾

20. Na wakikuhoji, basi sema: Nimejisalimisha kwa Allaah mimi pamoja na walionifuata. Na waambie waliopewa Kitabu na wasiojua kusoma na kuandika: Je, mmesilimu? Wakisilimu basi wamehidika, na wakikengeuka basi hakika juu yako ni kubalighisha tu. Na Allaah Ni Mwenye Kuwaona waja.[9]

 

 

إِنَّ الَّذِينَ يَكْفُرُونَ بِآيَاتِ اللَّـهِ وَيَقْتُلُونَ النَّبِيِّينَ بِغَيْرِ حَقٍّ وَيَقْتُلُونَ الَّذِينَ يَأْمُرُونَ بِالْقِسْطِ مِنَ النَّاسِ فَبَشِّرْهُم بِعَذَابٍ أَلِيمٍ ﴿٢١﴾ 

21. Hakika wanaokanusha Aayaat (na Ishara, Dalili) za Allaah na wakaua Manabii bila ya haki, na wakaua wale wanaoamrisha haki miongoni mwa watu, basi wabashirie adhabu iumizayo.

 

 

أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ حَبِطَتْ أَعْمَالُهُمْ فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ وَمَا لَهُم مِّن نَّاصِرِينَ ﴿٢٢﴾

22. Hao ndio ambao amali zao zimeporomoka katika dunia na Aakhirah na hawatopata watu wa kuwasaidia.

 

 

أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ أُوتُوا نَصِيبًا مِّنَ الْكِتَابِ يُدْعَوْنَ إِلَىٰ كِتَابِ اللَّـهِ لِيَحْكُمَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ يَتَوَلَّىٰ فَرِيقٌ مِّنْهُمْ وَهُم مُّعْرِضُونَ ﴿٢٣﴾ 

23. Je, hukuzingatia wale waliopewa sehemu katika Kitabu wanaitwa katika Kitabu cha Allaah ili kiwahukumu baina yao, kisha kundi miongoni mwao linageuka na huku wanapuuza.

 

 

 ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ قَالُوا لَن تَمَسَّنَا النَّارُ إِلَّا أَيَّامًا مَّعْدُودَاتٍ ۖ وَغَرَّهُمْ فِي دِينِهِم مَّا كَانُوا يَفْتَرُونَ ﴿٢٤﴾

24. Hivyo ni kwa sababu wamesema: Hautotugusa moto isipokuwa siku chache za kuhesabika. Na yakawadanganya katika dini yao yale waliyokuwa wakiyatunga (ya uongo).

 

 

فَكَيْفَ إِذَا جَمَعْنَاهُمْ لِيَوْمٍ لَّا رَيْبَ فِيهِ وَوُفِّيَتْ كُلُّ نَفْسٍ مَّا كَسَبَتْ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ ﴿٢٥﴾

25. Basi itakuwa vipi Tutakapowakusanya katika Siku ambayo haina shaka ndani yake, na kila nafsi italipwa kikamilifu yale iliyochuma, nao hawatodhulumiwa.

 

 

قُلِ اللَّـهُمَّ مَالِكَ الْمُلْكِ تُؤْتِي الْمُلْكَ مَن تَشَاءُ وَتَنزِعُ الْمُلْكَ مِمَّن تَشَاءُ وَتُعِزُّ مَن تَشَاءُ وَتُذِلُّ مَن تَشَاءُ ۖ بِيَدِكَ الْخَيْرُ ۖ إِنَّكَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿٢٦﴾

26. Sema: Ee Allaah Mfalme Uliyemiliki ufalme wote, Unampa ufalme Umtakaye, na Unamuondoshea ufalme Umtakaye, na Unamtukuza Umtakaye, na Unamdhalilisha Umtakaye, kheri imo Mkononi Mwako.  Hakika Wewe Ni Muweza wa kila kitu.

 

 

 تُولِجُ اللَّيْلَ فِي النَّهَارِ وَتُولِجُ النَّهَارَ فِي اللَّيْلِ ۖ وَتُخْرِجُ الْحَيَّ مِنَ الْمَيِّتِ وَتُخْرِجُ الْمَيِّتَ مِنَ الْحَيِّ ۖ وَتَرْزُقُ مَن تَشَاءُ بِغَيْرِ حِسَابٍ ﴿٢٧﴾

27. Unauingiza usiku katika mchana na Unauingiza mchana katika usiku, na Unatoa kilicho hai kutokana na kilicho mfu na Unatoa kilicho mfu kutokana na kilicho hai[10], na Unamruzuku Umtakaye bila ya hesabu.

 

 

لَّا يَتَّخِذِ الْمُؤْمِنُونَ الْكَافِرِينَ أَوْلِيَاءَ مِن دُونِ الْمُؤْمِنِينَ ۖ وَمَن يَفْعَلْ ذَٰلِكَ فَلَيْسَ مِنَ اللَّـهِ فِي شَيْءٍ إِلَّا أَن تَتَّقُوا مِنْهُمْ تُقَاةً ۗ وَيُحَذِّرُكُمُ اللَّـهُ نَفْسَهُ ۗ وَإِلَى اللَّـهِ الْمَصِيرُ ﴿٢٨﴾ 

28. Waumini wasiwafanye makafiri kuwa marafiki wandani na walinzi badala ya Waumini. Na atakayefanya hivyo, basi hatokua na chochote mbele ya Allaah, isipokuwa ikiwa kwa ajili ya kujilinda hatari kutoka kwao. Na Allaah Anakutahadharisheni na Nafsi Yake.[11] Na kwa Allaah ni mahali pa kuishia.

 

 

 قُلْ إِن تُخْفُوا مَا فِي صُدُورِكُمْ أَوْ تُبْدُوهُ يَعْلَمْهُ اللَّـهُ ۗ وَيَعْلَمُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۗ وَاللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿٢٩﴾

29. Sema: Mkificha yale yaliyomo katika vifua vyenu au mkiyafichua, Allaah Anayajua. Na Anajua yale yaliyomo katika mbingu na yale yaliyomo katika ardhi. Na Allaah Ni Muweza wa kila kitu.

 

 

يَوْمَ تَجِدُ كُلُّ نَفْسٍ مَّا عَمِلَتْ مِنْ خَيْرٍ مُّحْضَرًا وَمَا عَمِلَتْ مِن سُوءٍ تَوَدُّ لَوْ أَنَّ بَيْنَهَا وَبَيْنَهُ أَمَدًا بَعِيدًا ۗ وَيُحَذِّرُكُمُ اللَّـهُ نَفْسَهُ ۗ وَاللَّـهُ رَءُوفٌ بِالْعِبَادِ ﴿٣٠﴾

30. Siku itayokuta kila nafsi yale iliyoyatenda katika kheri yamehudhurishwa, na yale iliyoyatenda katika maovu, itatamani nafsi lau kama ingelikuwa baina yake na baina ya (maovu) hayo masafa ya mbali. Na Allaah Anakutahadharisheni na Nafsi Yake Na Allaah Ni Mwenye Huruma mno kwa waja.

 

 

 قُلْ إِن كُنتُمْ تُحِبُّونَ اللَّـهَ فَاتَّبِعُونِي يُحْبِبْكُمُ اللَّـهُ وَيَغْفِرْ لَكُمْ ذُنُوبَكُمْ ۗ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٣١﴾

31. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Mkiwa mnampenda Allaah, basi nifuateni mimi, Allaah Atakupendeni na Atakughufurieni dhambi zenu. Na Allaah Ni Mwingi wa Kughufiria, Mwenye Kurehemu.[12]

 

 

قُلْ أَطِيعُوا اللَّـهَ وَالرَّسُولَ ۖ فَإِن تَوَلَّوْا فَإِنَّ اللَّـهَ لَا يُحِبُّ الْكَافِرِينَ ﴿٣٢﴾

32. Sema: Mtiini Allaah na Rasuli, lakini mkikengeuka basi hakika Allaah Hapendi makafiri.

 

 

إِنَّ اللَّـهَ اصْطَفَىٰ آدَمَ وَنُوحًا وَآلَ إِبْرَاهِيمَ وَآلَ عِمْرَانَ عَلَى الْعَالَمِينَ ﴿٣٣﴾

33. Hakika Allaah Amemkhitari Aadam na Nuwh na kizazi cha Ibraahiym na kizazi cha ‘Imraan juu ya walimwengu.

 

 

 ذُرِّيَّةً بَعْضُهَا مِن بَعْضٍ ۗ وَاللَّـهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ ﴿٣٤﴾

34. Kizazi cha wao kwa wao, na Allaah Ni Mwenye Kusikia yote, Mjuzi wa yote.

 

 

إِذْ قَالَتِ امْرَأَتُ عِمْرَانَ رَبِّ إِنِّي نَذَرْتُ لَكَ مَا فِي بَطْنِي مُحَرَّرًا فَتَقَبَّلْ مِنِّي ۖ إِنَّكَ أَنتَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ ﴿٣٥﴾ 

35. Pale aliposema mke wa ‘Imraan: Rabb wangu! Hakika mimi nimeweka nadhiri Kwako kilichomo katika tumbo langu kuwa ni wakfu kukutumikia, basi Nitakabalie. Hakika Wewe Ni Mwenye Kusikia yote, Mjuzi wa yote[13].

 

 

 فَلَمَّا وَضَعَتْهَا قَالَتْ رَبِّ إِنِّي وَضَعْتُهَا أُنثَىٰ وَاللَّـهُ أَعْلَمُ بِمَا وَضَعَتْ وَلَيْسَ الذَّكَرُ كَالْأُنثَىٰ ۖ وَإِنِّي سَمَّيْتُهَا مَرْيَمَ وَإِنِّي أُعِيذُهَا بِكَ وَذُرِّيَّتَهَا مِنَ الشَّيْطَانِ الرَّجِيمِ ﴿٣٦﴾

36. Basi alipomzaa akasema: Rabb wangu! Hakika mimi nimezaa mwanamke, na Allaah Anajua zaidi alichokizaa. Na mwanamme si kama mwanamke. Nami nimemwita Maryam, nami namkinga Kwako na dhuria wake kutokana na shaytwaan aliyetokomezwa mbali na kulaaniwa.

 

 

فَتَقَبَّلَهَا رَبُّهَا بِقَبُولٍ حَسَنٍ وَأَنبَتَهَا نَبَاتًا حَسَنًا وَكَفَّلَهَا زَكَرِيَّا ۖ كُلَّمَا دَخَلَ عَلَيْهَا زَكَرِيَّا الْمِحْرَابَ وَجَدَ عِندَهَا رِزْقًا ۖ قَالَ يَا مَرْيَمُ أَنَّىٰ لَكِ هَـٰذَا ۖ قَالَتْ هُوَ مِنْ عِندِ اللَّـهِ ۖ إِنَّ اللَّـهَ يَرْزُقُ مَن يَشَاءُ بِغَيْرِ حِسَابٍ ﴿٣٧﴾ 

37. Basi Rabb wake Akampokea kwa kabuli njema, na Akamkuza mkuzo mwema, na Akamfanya Zakariyyaa kuwa mlezi wake. Kila Zakariyyaa alipoingia kwake katika chumba cha kuswalia alikuta kwake vyakula. Akasema: Ee Maryam! Umepata wapi hivi? Akasema: Hivi ni kutoka kwa Allaah. Hakika Allaah Anamruzuku Amtakaye bila ya hesabu.[14]   

 

 

 هُنَالِكَ دَعَا زَكَرِيَّا رَبَّهُ ۖ قَالَ رَبِّ هَبْ لِي مِن لَّدُنكَ ذُرِّيَّةً طَيِّبَةً ۖ إِنَّكَ سَمِيعُ الدُّعَاءِ ﴿٣٨﴾

38. Hapo hapo Zakariyyaa akamwomba Rabb wake, akasema: Rabb wangu! Nitunukie kutoka Kwako kizazi chema, hakika Wewe Ni Mwenye Kusikia duaa yangu.

 

 

فَنَادَتْهُ الْمَلَائِكَةُ وَهُوَ قَائِمٌ يُصَلِّي فِي الْمِحْرَابِ أَنَّ اللَّـهَ يُبَشِّرُكَ بِيَحْيَىٰ مُصَدِّقًا بِكَلِمَةٍ مِّنَ اللَّـهِ وَسَيِّدًا وَحَصُورًا وَنَبِيًّا مِّنَ الصَّالِحِينَ ﴿٣٩﴾

39. Malaika wakamwita (Zakariyyaa) naye akiwa amesimama anaswali katika chumba chake cha ibaada wakamwambia: Hakika Allaah Anakubashiria Yahyaa atakayesadikisha Neno (la Kun!) kutoka kwa Allaah. Atakuwa mtu wa kuheshimika, mtawa anayejitenga mbali na matamanio, na Nabiy miongoni mwa Swalihina.[15]

 

 

قَالَ رَبِّ أَنَّىٰ يَكُونُ لِي غُلَامٌ وَقَدْ بَلَغَنِيَ الْكِبَرُ وَامْرَأَتِي عَاقِرٌ ۖ قَالَ كَذَٰلِكَ اللَّـهُ يَفْعَلُ مَا يَشَاءُ ﴿٤٠﴾

40. (Zakariyyaa) akasema: Nitapataje ghulamu (mwana) na hali uzee umeshanifikia na mke wangu ni tasa?! Akasema: Hivyo ndivyo Allaah Anafanya Atakavyo.  

 

 

قَالَ رَبِّ اجْعَل لِّي آيَةً ۖ قَالَ آيَتُكَ أَلَّا تُكَلِّمَ النَّاسَ ثَلَاثَةَ أَيَّامٍ إِلَّا رَمْزًا ۗ وَاذْكُر رَّبَّكَ كَثِيرًا وَسَبِّحْ بِالْعَشِيِّ وَالْإِبْكَارِ ﴿٤١﴾ 

41. (Zakariyyaa) akasema: Rabb wangu! Niwekee Aayah (Ishara). Akasema: Aayah (Ishara) yako ni kwamba hutoweza kuwasemesha watu siku tatu ila kwa kuashiria tu. Na mdhukuru Rabb wako kwa wingi na msabihi jioni na asubuhi.

 

 

وَإِذْ قَالَتِ الْمَلَائِكَةُ يَا مَرْيَمُ إِنَّ اللَّـهَ اصْطَفَاكِ وَطَهَّرَكِ وَاصْطَفَاكِ عَلَىٰ نِسَاءِ الْعَالَمِينَ ﴿٤٢

42. Na pale Malaika (Jibriyl) aliposema:[16] Ee Maryam! Hakika Allaah Amekuteua na Amekutakasa na Amekukhitari juu ya wanawake wa walimwengu.[17]

 

 

 يَا مَرْيَمُ اقْنُتِي لِرَبِّكِ وَاسْجُدِي وَارْكَعِي مَعَ الرَّاكِعِينَ ﴿٤٣﴾

43. Ee Maryam!  Kuwa mtiifu kwa Rabb wako, na sujudu, na rukuu pamoja na wanaorukuu.

 

 

ذَٰلِكَ مِنْ أَنبَاءِ الْغَيْبِ نُوحِيهِ إِلَيْكَ ۚ وَمَا كُنتَ لَدَيْهِمْ إِذْ يُلْقُونَ أَقْلَامَهُمْ أَيُّهُمْ يَكْفُلُ مَرْيَمَ وَمَا كُنتَ لَدَيْهِمْ إِذْ يَخْتَصِمُونَ ﴿٤٤﴾ 

44. Hizo ni khabari za ghaibu Tunakufunulia Wahy (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم).  Na hukuwa pamoja nao walipotupa kalamu zao[18], ili nani kati yao amlee Maryam. Na hukuwa pamoja nao waliposhindana.

 

 

 إِذْ قَالَتِ الْمَلَائِكَةُ يَا مَرْيَمُ إِنَّ اللَّـهَ يُبَشِّرُكِ بِكَلِمَةٍ مِّنْهُ اسْمُهُ الْمَسِيحُ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ وَجِيهًا فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ وَمِنَ الْمُقَرَّبِينَ ﴿٤٥﴾

45. Na pale Malaika waliposema: Ee Maryam! Hakika Allaah Anakubashiria Neno (la Kun!) kutoka Kwake (umzae mtoto), jina lake ni Al-Masiyhu ‘Iysaa mwana wa Maryam, mwenye taadhima katika dunia na Aakhirah, na ni miongoni mwa waliokurubishwa (kwa Allaah).

 

 

وَيُكَلِّمُ النَّاسَ فِي الْمَهْدِ وَكَهْلًا وَمِنَ الصَّالِحِينَ ﴿٤٦﴾

46. Na Atawasemesha watu utotoni mwake na katika utu uzima wake, na ni miongoni mwa Swalihina.

 

 

قَالَتْ رَبِّ أَنَّىٰ يَكُونُ لِي وَلَدٌ وَلَمْ يَمْسَسْنِي بَشَرٌ ۖ قَالَ كَذَٰلِكِ اللَّـهُ يَخْلُقُ مَا يَشَاءُ ۚ إِذَا قَضَىٰ أَمْرًا فَإِنَّمَا يَقُولُ لَهُ كُن فَيَكُونُ ﴿٤٧﴾

47. (Maryam) Akasema: Itakuwaje nipate mtoto na hali hakunigusa mtu? (Malaika) Akasema: Hivyo ndivyo Allaah Huumba Akitakacho. Anapohukumu jambo basi huliambia: Kun! (Kuwa!) Basi nalo huwa.

 

 

 وَيُعَلِّمُهُ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَالتَّوْرَاةَ وَالْإِنجِيلَ ﴿٤٨﴾

48. Na Atamfunza Kitabu na Hikmah na Tawraat na Injiyl.

 

 

 

 وَرَسُولًا إِلَىٰ بَنِي إِسْرَائِيلَ أَنِّي قَدْ جِئْتُكُم بِآيَةٍ مِّن رَّبِّكُمْ ۖ أَنِّي أَخْلُقُ لَكُم مِّنَ الطِّينِ كَهَيْئَةِ الطَّيْرِ فَأَنفُخُ فِيهِ فَيَكُونُ طَيْرًا بِإِذْنِ اللَّـهِ ۖ وَأُبْرِئُ الْأَكْمَهَ وَالْأَبْرَصَ وَأُحْيِي الْمَوْتَىٰ بِإِذْنِ اللَّـهِ ۖ وَأُنَبِّئُكُم بِمَا تَأْكُلُونَ وَمَا تَدَّخِرُونَ فِي بُيُوتِكُمْ ۚ إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَةً لَّكُمْ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ﴿٤٩﴾

49. Na ni Rasuli kwa wana wa Israaiyl (atakayewaambia): Hakika mimi nimekujieni na Aayah (Dalili, Muujiza) kutoka kwa Rabb wenu, kwamba mimi nakuundieni kutokana na udongo, mfano wa umbo la ndege, kisha napuliza humo na anakuwa ndege kwa Idhini ya Allaah. Na naponyesha vipofu na wenye ubarasi, na nahuisha wafu kwa Idhini ya Allaah. Isitoshe, nakujulisheni pia mtakavyokula na mtakavyoweka akiba majumbani mwenu. Hakika katika hayo bila shaka kuna Aayah (Ishara, Dalili) kwenu mkiwa Waumini.[19]

 

 

 وَمُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيَّ مِنَ التَّوْرَاةِ وَلِأُحِلَّ لَكُم بَعْضَ الَّذِي حُرِّمَ عَلَيْكُمْ ۚ وَجِئْتُكُم بِآيَةٍ مِّن رَّبِّكُمْ فَاتَّقُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُونِ ﴿٥٠﴾

50. Na mwenye kusadikisha yaliyo kabla yangu katika Tawraat, na ili nikuhalalishieni baadhi ya yale yaliyoharamishwa kwenu. Na nimekujieni na Aayah (Ishara, Dalili, Hoja) kutoka kwa Rabb wenu. Basi mcheni Allaah na nitiini.

 

 

 إِنَّ اللَّـهَ رَبِّي وَرَبُّكُمْ فَاعْبُدُوهُ ۗ هَـٰذَا صِرَاطٌ مُّسْتَقِيمٌ ﴿٥١﴾

51. Hakika Allaah ni Rabb wangu na Rabb wenu basi mwabuduni. Hii ndio njia iliyonyooka.

 

 

 فَلَمَّا أَحَسَّ عِيسَىٰ مِنْهُمُ الْكُفْرَ قَالَ مَنْ أَنصَارِي إِلَى اللَّـهِ ۖ قَالَ الْحَوَارِيُّونَ نَحْنُ أَنصَارُ اللَّـهِ آمَنَّا بِاللَّـهِ وَاشْهَدْ بِأَنَّا مُسْلِمُونَ ﴿٥٢﴾

52. Basi ‘Iysaa alipohisi ukafiri kutoka kwao alisema: Nani watakaokuwa wasaidizi wangu kwa ajili ya Allaah? Wakasema wafuasi watiifu:  Sisi ni wasaidizi wa Allaah. Tumemwamini Allaah, na shuhudia kwamba sisi ni Waislamu (wenye kujisalimisha Kwake).

 

 

رَبَّنَا آمَنَّا بِمَا أَنزَلْتَ وَاتَّبَعْنَا الرَّسُولَ فَاكْتُبْنَا مَعَ الشَّاهِدِينَ ﴿٥٣﴾

53. Rabb wetu! Tumeamini Uliyoyateremsha na tumemfuata Rasuli, basi Tuandike pamoja na wanaoshuhudia (haki).

 

 

وَمَكَرُوا وَمَكَرَ اللَّـهُ ۖ وَاللَّـهُ خَيْرُ الْمَاكِرِينَ ﴿٥٤﴾

54.  Wakapanga makri (njama) na Allaah Akapanga makri. Na Allaah Ni Mbora wa wenye kupanga makri.[20] 

 

 

إِذْ قَالَ اللَّـهُ يَا عِيسَىٰ إِنِّي مُتَوَفِّيكَ وَرَافِعُكَ إِلَيَّ وَمُطَهِّرُكَ مِنَ الَّذِينَ كَفَرُوا وَجَاعِلُ الَّذِينَ اتَّبَعُوكَ فَوْقَ الَّذِينَ كَفَرُوا إِلَىٰ يَوْمِ الْقِيَامَةِ ۖ ثُمَّ إِلَيَّ مَرْجِعُكُمْ فَأَحْكُمُ بَيْنَكُمْ فِيمَا كُنتُمْ فِيهِ تَخْتَلِفُونَ ﴿٥٥﴾ 

55.  Pale Allaah Aliposema: Ee ‘Iysaa! Hakika Mimi Nitakuchukua na Nitakupandisha Kwangu na Nitakutakasa na wale waliokufuru na Nitawafanya wale waliokufuata (kujisalimisha kwa Allaah) kuwa juu ya wale waliokufuru mpaka Siku ya Qiyaamah, kisha Kwangu ndio marejeo yenu na Nitahukumu baina yenu katika yale mliyokuwa mkikhitilafiana.[21]

 

 

فَأَمَّا الَّذِينَ كَفَرُوا فَأُعَذِّبُهُمْ عَذَابًا شَدِيدًا فِي الدُّنْيَا وَالْآخِرَةِ وَمَا لَهُم مِّن نَّاصِرِينَ ﴿٥٦﴾

56. Ama wale waliokufuru, Nitawaadhibu adhabu kali katika dunia na Aakhirah, na hawatopata wa kuwasaidia.

 

 

وَأَمَّا الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ فَيُوَفِّيهِمْ أُجُورَهُمْ ۗ وَاللَّـهُ لَا يُحِبُّ الظَّالِمِينَ ﴿٥٧﴾

57. Na ama wale waliomini na wakatenda mema, basi hao Atawalipa ujira wao kikamilifu. Na Allaah Hapendi madhalimu.

 

 

ذَٰلِكَ نَتْلُوهُ عَلَيْكَ مِنَ الْآيَاتِ وَالذِّكْرِ الْحَكِيمِ ﴿٥٨﴾

58. Hizi Tunazokusomea (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) ni katika Aayaat na ukumbusho wenye hikmah.

 

 

 

إِنَّ مَثَلَ عِيسَىٰ عِندَ اللَّـهِ كَمَثَلِ آدَمَ ۖ خَلَقَهُ مِن تُرَابٍ ثُمَّ قَالَ لَهُ كُن فَيَكُونُ ﴿٥٩﴾

59. Hakika mfano wa ‘Iysaa kwa Allaah ni kama mfano wa Aadam. Amemuumba kutokana na udongo kisha Akamwambia: Kun! Basi akawa.[22]

 

 

الْحَقُّ مِن رَّبِّكَ فَلَا تَكُن مِّنَ الْمُمْتَرِينَ ﴿٦٠﴾

60. Ni Haki kutoka kwa Rabb wako, basi usiwe miongoni mwa wanaotia shaka.

 

 

فَمَنْ حَاجَّكَ فِيهِ مِن بَعْدِ مَا جَاءَكَ مِنَ الْعِلْمِ فَقُلْ تَعَالَوْا نَدْعُ أَبْنَاءَنَا وَأَبْنَاءَكُمْ وَنِسَاءَنَا وَنِسَاءَكُمْ وَأَنفُسَنَا وَأَنفُسَكُمْ ثُمَّ نَبْتَهِلْ فَنَجْعَل لَّعْنَتَ اللَّـهِ عَلَى الْكَاذِبِينَ ﴿٦١﴾

61. Basi yeyote atakayekuhoji kwayo baada ya kukujia ilimu, sema: Njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu, na wanawake wetu na wanawake wenu, na sisi wenyewe na nyinyi wenyewe, kisha tuombe mubaahalah,[23] tuifanye Laana ya Allaah iwe juu ya waongo.

 

 

 إِنَّ هَـٰذَا لَهُوَ الْقَصَصُ الْحَقُّ ۚ وَمَا مِنْ إِلَـٰهٍ إِلَّا اللَّـهُ ۚ وَإِنَّ اللَّـهَ لَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿٦٢﴾

62. Kwa hakika haya ni masimulizi ya haki. Na hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah. Na hakika Allaah Yeye Ndiye Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.

 

 

 

فَإِن تَوَلَّوْا فَإِنَّ اللَّـهَ عَلِيمٌ بِالْمُفْسِدِينَ ﴿٦٣﴾

63. Wakikengeuka, basi hakika Allaah ni Mjuzi wa mafisadi.

 

 

 قُلْ يَا أَهْلَ الْكِتَابِ تَعَالَوْا إِلَىٰ كَلِمَةٍ سَوَاءٍ بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمْ أَلَّا نَعْبُدَ إِلَّا اللَّـهَ وَلَا نُشْرِكَ بِهِ شَيْئًا وَلَا يَتَّخِذَ بَعْضُنَا بَعْضًا أَرْبَابًا مِّن دُونِ اللَّـهِ ۚ فَإِن تَوَلَّوْا فَقُولُوا اشْهَدُوا بِأَنَّا مُسْلِمُونَ ﴿٦٤﴾

64. Sema: Enyi Watu wa Kitabu!  Njooni katika neno lililo sawa baina yetu na baina yenu, kwamba tusiabudu isipokuwa Allaah Pekee, na wala tusimshirikishe na chochote, na wala wasichukue baadhi yetu wengine kuwa miola badala ya Allaah. Wakikengeuka, basi semeni: Shuhudieni kwamba sisi ni Waislamu.

 

 

يَا أَهْلَ الْكِتَابِ لِمَ تُحَاجُّونَ فِي إِبْرَاهِيمَ وَمَا أُنزِلَتِ التَّوْرَاةُ وَالْإِنجِيلُ إِلَّا مِن بَعْدِهِ ۚ أَفَلَا تَعْقِلُونَ ﴿٦٥﴾

65. Enyi Watu wa Kitabu!  Kwa nini mnahojiana kuhusu Ibraahiym na hali haikuteremshwa Tawraat na Injiyl isipokuwa baada yake? Je, hamtii akilini?

 

 

هَا أَنتُمْ هَـٰؤُلَاءِ حَاجَجْتُمْ فِيمَا لَكُم بِهِ عِلْمٌ فَلِمَ تُحَاجُّونَ فِيمَا لَيْسَ لَكُم بِهِ عِلْمٌ ۚ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ وَأَنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ ﴿٦٦﴾

66. Ha! Nyinyi ndio hawa mliohojiana katika yale ambayo mnayo ilimu nayo, basi kwa nini mnahojiana katika yale msiyokuwa na ilimu nayo? Na Allaah Anajua na nyinyi hamjui.

 

 

مَا كَانَ إِبْرَاهِيمُ يَهُودِيًّا وَلَا نَصْرَانِيًّا وَلَـٰكِن كَانَ حَنِيفًا مُّسْلِمًا وَمَا كَانَ مِنَ الْمُشْرِكِينَ ﴿٦٧﴾

67. Ibraahiym hakuwa Yahudi wala Naswara, lakini alikuwa mwenye kujiengua na upotofu akaelemea Dini ya haki, Muislamu na hakuwa miongoni mwa washirikina.[24]

 

 

إِنَّ أَوْلَى النَّاسِ بِإِبْرَاهِيمَ لَلَّذِينَ اتَّبَعُوهُ وَهَـٰذَا النَّبِيُّ وَالَّذِينَ آمَنُوا ۗ وَاللَّـهُ وَلِيُّ الْمُؤْمِنِينَ ﴿٦٨﴾

68. Hakika watu walio karibu zaidi kwa Ibraahiym ni wale waliomfuata na huyu Nabiy (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) na wale walioamini. Na Allaah Ni Rafiki Mlinzi wa Waumini.

 

 

 

وَدَّت طَّائِفَةٌ مِّنْ أَهْلِ الْكِتَابِ لَوْ يُضِلُّونَكُمْ وَمَا يُضِلُّونَ إِلَّا أَنفُسَهُمْ وَمَا يَشْعُرُونَ ﴿٦٩﴾ 

69. Linatamani kundi katika Watu wa Kitabu kama wangelikupotezeni, lakini hawapotezi ila nafsi zao na wao hawahisi.

 

 

يَا أَهْلَ الْكِتَابِ لِمَ تَكْفُرُونَ بِآيَاتِ اللَّـهِ وَأَنتُمْ تَشْهَدُونَ ﴿٧٠﴾

70. Enyi Watu wa Kitabu! Kwa nini mnakanusha Aayaat (na Ishara, Miujiza, Dalili) za Allaah na hali nyinyi mnashuhudia?

 

 

 يَا أَهْلَ الْكِتَابِ لِمَ تَلْبِسُونَ الْحَقَّ بِالْبَاطِلِ وَتَكْتُمُونَ الْحَقَّ وَأَنتُمْ تَعْلَمُونَ ﴿٧١﴾

71. Enyi Watu wa Kitabu!  Kwa nini mnachanganya haki na baatwil na mnaficha haki na hali nyinyi mnajua?

 

 

وَقَالَت طَّائِفَةٌ مِّنْ أَهْلِ الْكِتَابِ آمِنُوا بِالَّذِي أُنزِلَ عَلَى الَّذِينَ آمَنُوا وَجْهَ النَّهَارِ وَاكْفُرُوا آخِرَهُ لَعَلَّهُمْ يَرْجِعُونَ ﴿٧٢﴾

72. Na kundi miongoni mwa Watu wa Kitabu likasema (kuambiana): Aminini yale ambayo yameteremshwa kwa wale walioamini mwanzo wa mchana na kanusheni mwisho wake, wapate kurejea (waache dini yao).

 

 

وَلَا تُؤْمِنُوا إِلَّا لِمَن تَبِعَ دِينَكُمْ قُلْ إِنَّ الْهُدَىٰ هُدَى اللَّـهِ أَن يُؤْتَىٰ أَحَدٌ مِّثْلَ مَا أُوتِيتُمْ أَوْ يُحَاجُّوكُمْ عِندَ رَبِّكُمْ ۗ قُلْ إِنَّ الْفَضْلَ بِيَدِ اللَّـهِ يُؤْتِيهِ مَن يَشَاءُ ۗ وَاللَّـهُ وَاسِعٌ عَلِيمٌ ﴿٧٣﴾ 

73. Na wala msimwamini isipokuwa yule anayefuata dini yenu. Sema: Hakika mwongozo wa kweli ni Mwongozo wa Allaah, (mnakhofu) kwamba atapewa mmoja (ilimu) mfano wa yale mliyopewa au wakuhojini mbele ya Rabb wenu. Sema: Hakika fadhila zi Mkononi mwa Allaah, Humpa Amtakaye. Na Allaah Ni Mwenye wasaa, Mjuzi wa yote.

 

 

يَخْتَصُّ بِرَحْمَتِهِ مَن يَشَاءُ ۗ وَاللَّـهُ ذُو الْفَضْلِ الْعَظِيمِ ﴿٧٤﴾

74. Humchagua kwa Rehma Yake Amtakaye, na Allaah Ni Mwenye Fadhila kuu kabisa.

 

 

وَمِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ مَنْ إِن تَأْمَنْهُ بِقِنطَارٍ يُؤَدِّهِ إِلَيْكَ وَمِنْهُم مَّنْ إِن تَأْمَنْهُ بِدِينَارٍ لَّا يُؤَدِّهِ إِلَيْكَ إِلَّا مَا دُمْتَ عَلَيْهِ قَائِمًا ۗ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ قَالُوا لَيْسَ عَلَيْنَا فِي الْأُمِّيِّينَ سَبِيلٌ وَيَقُولُونَ عَلَى اللَّـهِ الْكَذِبَ وَهُمْ يَعْلَمُونَ ﴿٧٥﴾

75. Na katika Watu wa Kitabu yuko ambaye ukimpa amana ya mrundi wa mali atakurejeshea, na katika wao yuko ambaye ukimpa amana ya dinari moja tu hatoirudisha kwako isipokuwa utakapodumisha kumsimamia (kumdai). Hilo ni kwa sababu wao wamesema: Hakuna juu yetu lawama kwa wasiojua kusoma na kuandika na wanamsingizia uongo Allaah, na hali wao wanajua.

 

 

بَلَىٰ مَنْ أَوْفَىٰ بِعَهْدِهِ وَاتَّقَىٰ فَإِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُتَّقِينَ ﴿٧٦﴾

76. Sivyo hivyo! Bali atakayetimiza ahadi yake akawa na taqwa, basi hakika Allaah Anapenda wenye taqwa.

 

 

إِنَّ الَّذِينَ يَشْتَرُونَ بِعَهْدِ اللَّـهِ وَأَيْمَانِهِمْ ثَمَنًا قَلِيلًا أُولَـٰئِكَ لَا خَلَاقَ لَهُمْ فِي الْآخِرَةِ وَلَا يُكَلِّمُهُمُ اللَّـهُ وَلَا يَنظُرُ إِلَيْهِمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَلَا يُزَكِّيهِمْ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿٧٧﴾

77. Hakika wale wanaobadilisha Ahadi ya Allaah na viapo vyao kwa thamani ndogo, hao hawana sehemu yoyote katika Aakhirah na wala Allaah Hatowasemesha na wala Hatowatazama Siku Ya Qiyaamah na wala Hatowatakasa na watapata adhabu iumizayo.

 

 

 وَإِنَّ مِنْهُمْ لَفَرِيقًا يَلْوُونَ أَلْسِنَتَهُم بِالْكِتَابِ لِتَحْسَبُوهُ مِنَ الْكِتَابِ وَمَا هُوَ مِنَ الْكِتَابِ وَيَقُولُونَ هُوَ مِنْ عِندِ اللَّـهِ وَمَا هُوَ مِنْ عِندِ اللَّـهِ وَيَقُولُونَ عَلَى اللَّـهِ الْكَذِبَ وَهُمْ يَعْلَمُونَ ﴿٧٨﴾

78. Na hakika miongoni mwao kuna kundi wanaopotosha Kitabu kwa ndimi zao (wanaposoma) ili mdhanie kuwa hayo yanayotoka katika Kitabu, na hali hayo si yenye kutoka katika Kitabu, na wanasema: Hayo ni kutoka kwa Allaah, ilhali hayo si kutoka kwa Allaah, na wanamsingizia uongo Allaah na wao wanajua.

 

 

مَا كَانَ لِبَشَرٍ أَن يُؤْتِيَهُ اللَّـهُ الْكِتَابَ وَالْحُكْمَ وَالنُّبُوَّةَ ثُمَّ يَقُولَ لِلنَّاسِ كُونُوا عِبَادًا لِّي مِن دُونِ اللَّـهِ وَلَـٰكِن كُونُوا رَبَّانِيِّينَ بِمَا كُنتُمْ تُعَلِّمُونَ الْكِتَابَ وَبِمَا كُنتُمْ تَدْرُسُونَ ﴿٧٩﴾

79. Ni mustahili kwa mtu kwamba Allaah Amempa Kitabu na Al-Hukma[25] na Unabii kisha aje awaambie watu: Kuweni wenye kuniabudu mimi badala ya Allaah, bali (atawaambia): Kuweni Rabbaaniyyuwn[26] (Marabi) kwa yale mliyokuwa mkiyafundisha ya Kitabu na kwa yale mliyokuwa mkiyadurusu.

 

 

وَلَا يَأْمُرَكُمْ أَن تَتَّخِذُوا الْمَلَائِكَةَ وَالنَّبِيِّينَ أَرْبَابًا ۗ أَيَأْمُرُكُم بِالْكُفْرِ بَعْدَ إِذْ أَنتُم مُّسْلِمُونَ ﴿٨٠﴾ 

80. Na wala hakuamuruni kuwachukua Malaika na Manabii kuwafanya miola. Je, anakuamrisheni ukafiri baada ya nyinyi kuwa mmejisalimisha kwa Allaah?

 

 

وَإِذْ أَخَذَ اللَّـهُ مِيثَاقَ النَّبِيِّينَ لَمَا آتَيْتُكُم مِّن كِتَابٍ وَحِكْمَةٍ ثُمَّ جَاءَكُمْ رَسُولٌ مُّصَدِّقٌ لِّمَا مَعَكُمْ لَتُؤْمِنُنَّ بِهِ وَلَتَنصُرُنَّهُ ۚ قَالَ أَأَقْرَرْتُمْ وَأَخَذْتُمْ عَلَىٰ ذَٰلِكُمْ إِصْرِي ۖ قَالُوا أَقْرَرْنَا ۚ قَالَ فَاشْهَدُوا وَأَنَا مَعَكُم مِّنَ الشَّاهِدِينَ ﴿٨١﴾

81. Na pale Allaah Alipochukua fungamano kwa Manabii (akawaambia): Ninayokupeni katika Kitabu na Hikmah, kisha akakujieni Rasuli (Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) mwenye kusadikisha yaliyo pamoja nanyi, basi ni lazima kumwamini na kumnusuru. (Kisha Allaah) Akasema: Je, mmekubali na mtashika fungamano Langu juu ya hayo? Wakasema: Tumekubali. (Allaah) Akasema: Basi shuhudieni na Mimi Niko pamoja nanyi katika wenye kushuhudia.[27]

 

 

فَمَن تَوَلَّىٰ بَعْدَ ذَٰلِكَ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْفَاسِقُونَ ﴿٨٢﴾

82. Atakayekengeuka baada ya hayo, basi hao ni mafasiki.

 

 

أَفَغَيْرَ دِينِ اللَّـهِ يَبْغُونَ وَلَهُ أَسْلَمَ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ طَوْعًا وَكَرْهًا وَإِلَيْهِ يُرْجَعُونَ ﴿٨٣﴾

83. Je, wanataka dini isiyokuwa ya Allaah, na hali amejisalimisha Kwake kila aliye katika mbingu na katika ardhi akipenda asipende na Kwake watarejeshwa?  

 

 

قُلْ آمَنَّا بِاللَّـهِ وَمَا أُنزِلَ عَلَيْنَا وَمَا أُنزِلَ عَلَىٰ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْمَاعِيلَ وَإِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ وَالْأَسْبَاطِ وَمَا أُوتِيَ مُوسَىٰ وَعِيسَىٰ وَالنَّبِيُّونَ مِن رَّبِّهِمْ لَا نُفَرِّقُ بَيْنَ أَحَدٍ مِّنْهُمْ وَنَحْنُ لَهُ مُسْلِمُونَ ﴿٨٤﴾

84. Sema: Tumemwamini Allaah, na yaliyoteremshwa kwetu na yaliyoteremshwa kwa Ibraahiym, na Ismaa’iyl na Is-haaq, na Ya’quwb na Al-Asbaatw[28] (kizazi chake), na yale aliyopewa Muwsaa na ‘Iysaa na Manabii kutoka kwa Rabb wao, hatutofautishi baina ya yeyote miongoni mwao, nasi ni Waislamu Wenye kujisalimisha) Kwake.

 

 

 وَمَن يَبْتَغِ غَيْرَ الْإِسْلَامِ دِينًا فَلَن يُقْبَلَ مِنْهُ وَهُوَ فِي الْآخِرَةِ مِنَ الْخَاسِرِينَ ﴿٨٥﴾

85. Na yeyote anayetaka dini isiyokuwa ya Kiislamu basi haitokubaliwa kwake, naye katika Aakhirah atakuwa miongoni mwa waliokhasirika.[29]

 

 

كَيْفَ يَهْدِي اللَّـهُ قَوْمًا كَفَرُوا بَعْدَ إِيمَانِهِمْ وَشَهِدُوا أَنَّ الرَّسُولَ حَقٌّ وَجَاءَهُمُ الْبَيِّنَاتُ ۚ وَاللَّـهُ لَا يَهْدِي الْقَوْمَ الظَّالِمِينَ ﴿٨٦﴾ 

86. Vipi Allaah Atawaongoza watu waliokufuru baada ya kuamini kwao na wakashuhudia kwamba Rasuli ni haki na zikawajia hoja bayana? Na Allaah Hawahidi watu madhalimu.

 

 

 أُولَـٰئِكَ جَزَاؤُهُمْ أَنَّ عَلَيْهِمْ لَعْنَةَ اللَّـهِ وَالْمَلَائِكَةِ وَالنَّاسِ أَجْمَعِينَ ﴿٨٧﴾

87. Hao jazaa yao ni kwamba juu yao ipo Laana ya Allaah na ya Malaika na ya watu wote.

 

 

خَالِدِينَ فِيهَا لَا يُخَفَّفُ عَنْهُمُ الْعَذَابُ وَلَا هُمْ يُنظَرُونَ ﴿٨٨﴾

88. Wadumu humo, hawatopunguziwa adhabu wala hawatopewa muda wa kuakhirishwa adhabu.

 

 

إِلَّا الَّذِينَ تَابُوا مِن بَعْدِ ذَٰلِكَ وَأَصْلَحُوا فَإِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٨٩﴾

89. Isipokuwa wale waliotubu baada ya hayo na wakatengeneza, kwani hakika Allaah Ni Mwingi wa Kughufiria, Mwenye Kurehemu.

 

 

إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا بَعْدَ إِيمَانِهِمْ ثُمَّ ازْدَادُوا كُفْرًا لَّن تُقْبَلَ تَوْبَتُهُمْ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الضَّالُّونَ ﴿٩٠﴾ 

90. Hakika wale waliokufuru baada ya kuamini kwao kisha wakazidi kukufuru, haitokubaliwa tawbah yao, na hao ndio waliopotoka.

 

 

 إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا وَمَاتُوا وَهُمْ كُفَّارٌ فَلَن يُقْبَلَ مِنْ أَحَدِهِم مِّلْءُ الْأَرْضِ ذَهَبًا وَلَوِ افْتَدَىٰ بِهِ ۗ أُولَـٰئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ وَمَا لَهُم مِّن نَّاصِرِينَ ﴿٩١﴾

91. Hakika wale waliokufuru na wakafa nao wakiwa makafiri, basi kamwe haitakubaliwa kutoka kwa mmoja wao, dhahabu ya ujazo wa dunia nzima lau wakitaka kujifidia nayo. Hao watapata adhabu iumizayo na hawatopata watu wa kuwasaidia.

 

 

 لَن تَنَالُوا الْبِرَّ حَتَّىٰ تُنفِقُوا مِمَّا تُحِبُّونَ ۚ وَمَا تُنفِقُوا مِن شَيْءٍ فَإِنَّ اللَّـهَ بِهِ عَلِيمٌ ﴿٩٢﴾

92. Hamtoweza kuufikia wema kamili mpaka mtoe katika vile mnavyovipenda. Na kitu chochote mnachotoa basi hakika Allaah kwacho Ni Mjuzi.

 

 

 كُلُّ الطَّعَامِ كَانَ حِلًّا لِّبَنِي إِسْرَائِيلَ إِلَّا مَا حَرَّمَ إِسْرَائِيلُ عَلَىٰ نَفْسِهِ مِن قَبْلِ أَن تُنَزَّلَ التَّوْرَاةُ ۗ قُلْ فَأْتُوا بِالتَّوْرَاةِ فَاتْلُوهَا إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿٩٣﴾

93. Kila chakula kilikuwa halali kwa wana wa Israaiyl, isipokuwa kile alichojiharamishia Israaiyl[30] (Ya’quwb (عليه السّلام mwenyewe kabla ya kuteremshwa Tawraat. Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Basi leteni Tawraat kisha muisome mkiwa wakweli.

 

 

 

فَمَنِ افْتَرَىٰ عَلَى اللَّـهِ الْكَذِبَ مِن بَعْدِ ذَٰلِكَ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الظَّالِمُونَ ﴿٩٤﴾

94. Na yeyote atakayemtungia Allaah uongo baada ya hayo, basi hao ndio madhalimu.

 

 

قُلْ صَدَقَ اللَّـهُ ۗ فَاتَّبِعُوا مِلَّةَ إِبْرَاهِيمَ حَنِيفًا وَمَا كَانَ مِنَ الْمُشْرِكِينَ ﴿٩٥﴾

95. Sema: Allaah Amesema kweli. Basi fuateni mila ya Ibraahiym aliyejiengua na upotofu akaelemea Dini ya haki na hakuwa miongoni mwa washirikina.[31]

 

 

إِنَّ أَوَّلَ بَيْتٍ وُضِعَ لِلنَّاسِ لَلَّذِي بِبَكَّةَ مُبَارَكًا وَهُدًى لِّلْعَالَمِينَ ﴿٩٦﴾ 

96. Hakika nyumba (Al-Ka’bah) ya awali iliyowekwa kwa ajili ya watu (kufanya ibaada) ni ile ambayo iko Bakkah (Makkah),[32] yenye barakah na mwongozo kwa walimwengu.

 

 

فِيهِ آيَاتٌ بَيِّنَاتٌ مَّقَامُ إِبْرَاهِيمَ ۖ وَمَن دَخَلَهُ كَانَ آمِنًا ۗ وَلِلَّـهِ عَلَى النَّاسِ حِجُّ الْبَيْتِ مَنِ اسْتَطَاعَ إِلَيْهِ سَبِيلًا ۚ وَمَن كَفَرَ فَإِنَّ اللَّـهَ غَنِيٌّ عَنِ الْعَالَمِينَ ﴿٩٧﴾ 

97. Ndani yake kuna Aayaat (Ishara na Dalili) zilizo wazi mahali aliposimama Ibraahiym (kujenga). Na mwenye kuingia humo anakuwa katika amani. Na kwa ajili ya Allaah imewajibika watu watekeleze Hajj katika nyumba (Al-Ka’bah) hiyo kwa mwenye uwezo. Na atakayekufuru, basi hakika Allaah Ni Mkwasi kwa walimwengu.

 

 

قُلْ يَا أَهْلَ الْكِتَابِ لِمَ تَكْفُرُونَ بِآيَاتِ اللَّـهِ وَاللَّـهُ شَهِيدٌ عَلَىٰ مَا تَعْمَلُونَ ﴿٩٨﴾ 

98. Sema: Enyi Watu wa Kitabu! Kwa nini mnakanusha Aayaat (na Ishara, Miujiza, Dalili) za Allaah ilhali Allaah Ni Shahidi juu ya myatendayo?

 

 

قُلْ يَا أَهْلَ الْكِتَابِ لِمَ تَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ اللَّـهِ مَنْ آمَنَ تَبْغُونَهَا عِوَجًا وَأَنتُمْ شُهَدَاءُ ۗ وَمَا اللَّـهُ بِغَافِلٍ عَمَّا تَعْمَلُونَ ﴿٩٩﴾ 

99. Sema: Enyi Watu wa Kitabu! Kwa nini mnamzuilia aliyeamini Njia ya Allaah, mnaitafutia ionekane kombo na hali nyinyi ni mashahidi (juu ya haki)? Na Allaah Si Mwenye Kughafilika na hayo myatendayo.

 

 

 يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِن تُطِيعُوا فَرِيقًا مِّنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ يَرُدُّوكُم بَعْدَ إِيمَانِكُمْ كَافِرِينَ ﴿١٠٠﴾

100. Enyi walioamini! Mkilitii kundi la waliopewa Kitabu watakurudisheni baada ya nyinyi kuamini muwe makafiri.

 

 

وَكَيْفَ تَكْفُرُونَ وَأَنتُمْ تُتْلَىٰ عَلَيْكُمْ آيَاتُ اللَّـهِ وَفِيكُمْ رَسُولُهُ ۗ وَمَن يَعْتَصِم بِاللَّـهِ فَقَدْ هُدِيَ إِلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ ﴿١٠١﴾

101. Na vipi mkufuru na hali mnasomewa Aayaat za Allaah na Rasuli Wake yuko kati yenu? Na atakayeshikamana na Allaah basi kwa yakini ameongozwa kuelekea njia iliyonyooka.

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّـهَ حَقَّ تُقَاتِهِ وَلَا تَمُوتُنَّ إِلَّا وَأَنتُم مُّسْلِمُونَ ﴿١٠٢﴾

102. Enyi walioamini! Mcheni Allaah kama ipasavyo kumcha na chungeni sana, angalieni msife isipokuwa nyinyi ni Waislamu.

 

 

وَاعْتَصِمُوا بِحَبْلِ اللَّـهِ جَمِيعًا وَلَا تَفَرَّقُوا ۚ وَاذْكُرُوا نِعْمَتَ اللَّـهِ عَلَيْكُمْ إِذْ كُنتُمْ أَعْدَاءً فَأَلَّفَ بَيْنَ قُلُوبِكُمْ فَأَصْبَحْتُم بِنِعْمَتِهِ إِخْوَانًا وَكُنتُمْ عَلَىٰ شَفَا حُفْرَةٍ مِّنَ النَّارِ فَأَنقَذَكُم مِّنْهَا ۗ كَذَٰلِكَ يُبَيِّنُ اللَّـهُ لَكُمْ آيَاتِهِ لَعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ ﴿١٠٣﴾ 

103. Na shikamaneni kwa Kamba ya Allaah nyote pamoja, wala msifarikiane.[33] Na kumbukeni Neema ya Allaah juu yenu, pale mlipokuwa maadui (kati yenu), kisha Akaunganisha nyoyo zenu, mkawa ndugu kwa Neema Yake, na mlikuwa ukingoni mwa shimo la moto Akakuokoeni humo. Hivyo ndivyo Allaah Anavyokubainishieni Aayaat (na Ishara) Zake mpate kuhidika.   

 

 

 

وَلْتَكُن مِّنكُمْ أُمَّةٌ يَدْعُونَ إِلَى الْخَيْرِ وَيَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ ۚ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفلِحُونَ ﴿١٠٤﴾

104. Na watokeze kutoka kwenu ummah wa watu unaolingania kheri, na unaoamrisha mema na unaokataza munkari. Na hao ndio waliofaulu.

 

 

وَلَا تَكُونُوا كَالَّذِينَ تَفَرَّقُوا وَاخْتَلَفُوا مِن بَعْدِ مَا جَاءَهُمُ الْبَيِّنَاتُ ۚ وَأُولَـٰئِكَ لَهُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ ﴿١٠٥﴾

105. Na wala msiwe kama wale waliofarikiana na wakakhitilafiana[34]  baada ya kuwajia hoja bayana. Na hao watapata adhabu kuu kabisa.

 

 

 

يَوْمَ تَبْيَضُّ وُجُوهٌ وَتَسْوَدُّ وُجُوهٌ ۚ فَأَمَّا الَّذِينَ اسْوَدَّتْ وُجُوهُهُمْ أَكَفَرْتُم بَعْدَ إِيمَانِكُمْ فَذُوقُوا الْعَذَابَ بِمَا كُنتُمْ تَكْفُرُونَ ﴿١٠٦﴾ 

106. Siku nyuso zitakuwa nyeupe na nyuso (nyingine) zitakuwa nyeusi. Basi wale ambao nyuso zao zitakuwa nyeusi (wataambiwa): Je, mlikufuru baada ya kuamini kwenu?!  Basi onjeni adhabu kwa sababu ya yale mliyokuwa mkiyakanusha.

 

 

 وَأَمَّا الَّذِينَ ابْيَضَّتْ وُجُوهُهُمْ فَفِي رَحْمَةِ اللَّـهِ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿١٠٧﴾

107. Na wale ambao nyuso zao zitakuwa nyeupe, basi watakuwa katika Rehma ya Allaah. Wao humo watadumu.

 

 

تِلْكَ آيَاتُ اللَّـهِ نَتْلُوهَا عَلَيْكَ بِالْحَقِّ ۗ وَمَا اللَّـهُ يُرِيدُ ظُلْمًا لِّلْعَالَمِينَ ﴿١٠٨﴾

108. Hizi ni Aayaat za Allaah Tunakusomea kwa haki (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم). Na Allaah Hataki dhulma kwa walimwengu.

 

 

 

وَلِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۚ وَإِلَى اللَّـهِ تُرْجَعُ الْأُمُورُ ﴿١٠٩﴾

109. Na ni vya Allaah vilivyomo katika mbingu na katika ardhi. Na kwa Allaah Pekee mambo (yote) yatarejeshwa.

 

 

 كُنتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ ۗ وَلَوْ آمَنَ أَهْلُ الْكِتَابِ لَكَانَ خَيْرًا لَّهُم ۚ مِّنْهُمُ الْمُؤْمِنُونَ وَأَكْثَرُهُمُ الْفَاسِقُونَ ﴿١١٠﴾

110. Mmekuwa ummah bora[35] kabisa uliotolewa (mfano) kwa watu, mnaamrisha mema na mnakataza munkari na mnamwamini Allaah. Na lau wangeliamini Watu wa Kitabu, basi ingelikuwa ni bora kwao. Wako miongoni mwao wanaoamini lakini wengi wao ni mafasiki.

 

 

لَن يَضُرُّوكُمْ إِلَّا أَذًى ۖ وَإِن يُقَاتِلُوكُمْ يُوَلُّوكُمُ الْأَدْبَارَ ثُمَّ لَا يُنصَرُونَ ﴿١١١﴾

111. Hawatokudhuruni isipokuwa udhia tu, na wakikupigeni vita watakupeni migongo (wakimbie), kisha hawatonusuriwa.

 

 

ضُرِبَتْ عَلَيْهِمُ الذِّلَّةُ أَيْنَ مَا ثُقِفُوا إِلَّا بِحَبْلٍ مِّنَ اللَّـهِ وَحَبْلٍ مِّنَ النَّاسِ وَبَاءُوا بِغَضَبٍ مِّنَ اللَّـهِ وَضُرِبَتْ عَلَيْهِمُ الْمَسْكَنَةُ ۚ ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ كَانُوا يَكْفُرُونَ بِآيَاتِ اللَّـهِ وَيَقْتُلُونَ الْأَنبِيَاءَ بِغَيْرِ حَقٍّ ۚ ذَٰلِكَ بِمَا عَصَوا وَّكَانُوا يَعْتَدُونَ ﴿١١٢﴾ 

112. Wamepigwa na udhalili popote wanapopatikana ila tu pale wanapolindwa na Ahadi ya Allaah na ahadi ya watu, na (pamoja na hayo) wamestahiki ghadhabu kutoka kwa Allaah, na wakapigwa na umasikini. Sababu ya hayo ni kuwa wao walikuwa wakikanusha Aayaat (na Ishara, Dalili) za Allaah na wakiua Manabii pasi na haki. Hayo (pia) ni kwa sababu ya kuasi kwao, na walikuwa wanataadi (kuvuka mipaka).

 

 

لَيْسُوا سَوَاءً ۗ مِّنْ أَهْلِ الْكِتَابِ أُمَّةٌ قَائِمَةٌ يَتْلُونَ آيَاتِ اللَّـهِ آنَاءَ اللَّيْلِ وَهُمْ يَسْجُدُونَ ﴿١١٣﴾

113. Hawako sawa sawa. Miongoni mwa Watu wa Kitabu wako watu wenye kusimama (kwa utiifu), wanasoma Aayaat za Allaah nyakati za usiku na wao wanasujudu (katika Swalaah).

 

 

يُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَيَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَيَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَيُسَارِعُونَ فِي الْخَيْرَاتِ وَأُولَـٰئِكَ مِنَ الصَّالِحِينَ ﴿١١٤﴾

114. Wanamwamini Allaah na Siku ya Mwisho, na wanaamrisha mema na wanakataza munkari[36]  na wanakimbilia katika mambo ya kheri, na hao ni miongoni mwa Swalihina.

 

 

وَمَا يَفْعَلُوا مِنْ خَيْرٍ فَلَن يُكْفَرُوهُ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ بِالْمُتَّقِينَ ﴿١١٥﴾

115. Na kheri yoyote waifanyayo basi hawatokanushiwa (thawabu zake).  Na Allaah Anawajua vyema wenye taqwa.

 

 

 

إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا لَن تُغْنِيَ عَنْهُمْ أَمْوَالُهُمْ وَلَا أَوْلَادُهُم مِّنَ اللَّـهِ شَيْئًا ۖ وَأُولَـٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ ۚ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ ﴿١١٦﴾

116.  Hakika wale waliokufuru hazitowafaa kitu mali zao wala watoto wao mbele ya Allaah. Hao ni watu wa motoni. Wao humo watadumu.

 

 

 

مَثَلُ مَا يُنفِقُونَ فِي هَـٰذِهِ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا كَمَثَلِ رِيحٍ فِيهَا صِرٌّ أَصَابَتْ حَرْثَ قَوْمٍ ظَلَمُوا أَنفُسَهُمْ فَأَهْلَكَتْهُ ۚ وَمَا ظَلَمَهُمُ اللَّـهُ وَلَـٰكِنْ أَنفُسَهُمْ يَظْلِمُونَ ﴿١١٧﴾ 

117. Mfano wa vile wanavyovitoa katika uhai (wao) huu wa duniani ni kama mfano wa upepo ndani yake mna baridi ya barafu, ukasibu shamba lilolimwa la watu waliojidhulumu nafsi zao ukaliangamiza. Na Allaah Hakuwadhulumu lakini wamejidhulumu nafsi zao.

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا بِطَانَةً مِّن دُونِكُمْ لَا يَأْلُونَكُمْ خَبَالًا وَدُّوا مَا عَنِتُّمْ قَدْ بَدَتِ الْبَغْضَاءُ مِنْ أَفْوَاهِهِمْ وَمَا تُخْفِي صُدُورُهُمْ أَكْبَرُ ۚ قَدْ بَيَّنَّا لَكُمُ الْآيَاتِ ۖ إِن كُنتُمْ تَعْقِلُونَ ﴿١١٨﴾

118. Enyi walioamini! Msifanye rafiki mwandani na msiri (wenu) wasiokuwa nyinyi. Hawatoacha kukuharibieni. Wanatamani kama mngetaabika. Imekwishajitokeza bughudha kutoka midomoni mwao. Na yale yanayoficha vifua vyao ni makubwa zaidi. Tumekwisha kubainishieni Aayaat (Ishara, Dalili, Alama) [zao] mkiwa mtatia akilini.

 

 

هَا أَنتُمْ أُولَاءِ تُحِبُّونَهُمْ وَلَا يُحِبُّونَكُمْ وَتُؤْمِنُونَ بِالْكِتَابِ كُلِّهِ وَإِذَا لَقُوكُمْ قَالُوا آمَنَّا وَإِذَا خَلَوْا عَضُّوا عَلَيْكُمُ الْأَنَامِلَ مِنَ الْغَيْظِ ۚ قُلْ مُوتُوا بِغَيْظِكُمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُورِ ﴿١١٩﴾ 

119. Ha! Nyinyi ndio wale mnaowapenda na wala wao hawakupendeni, na mnaamini Kitabu chote, na wanapokukuteni husema: Tumeamini, na wanapokuwa peke yao wanakutafunieni ncha za vidole kutokana na chuki. Sema: Kufeni kwa chuki zenu! Hakika Allaah Anayajua vyema yaliyomo vifuani.

 

 

إِن تَمْسَسْكُمْ حَسَنَةٌ تَسُؤْهُمْ وَإِن تُصِبْكُمْ سَيِّئَةٌ يَفْرَحُوا بِهَا ۖ وَإِن تَصْبِرُوا وَتَتَّقُوا لَا يَضُرُّكُمْ كَيْدُهُمْ شَيْئًا ۗ إِنَّ اللَّـهَ بِمَا يَعْمَلُونَ مُحِيطٌ ﴿١٢٠﴾

120. Ikikupateni kheri (nusura, ushindi) inawachukiza, na likikusibuni baya hulifurahia. Na kama mtasubiri na mkashikamana na taqwa, basi hila zao hazitakudhuruni kitu. Hakika Allaah Ni Mwenye Kuyazunguka wayatendayo. 

 

 

وَإِذْ غَدَوْتَ مِنْ أَهْلِكَ تُبَوِّئُ الْمُؤْمِنِينَ مَقَاعِدَ لِلْقِتَالِ ۗ وَاللَّـهُ سَمِيعٌ عَلِيمٌ ﴿١٢١﴾ 

121. Na pale ulipotoka asubuhi mapema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) ukaacha ahli zako ili uwapangie Waumini vituo vya kupigana (Vita vya Uhud).[37] Na Allaah Ni Mwenye Kusikia yote, Mjuzi wa yote.

 

 

 

إِذْ هَمَّت طَّائِفَتَانِ مِنكُمْ أَن تَفْشَلَا وَاللَّـهُ وَلِيُّهُمَا ۗ وَعَلَى اللَّـهِ فَلْيَتَوَكَّلِ الْمُؤْمِنُونَ ﴿١٢٢﴾

122. Pale makundi mawili miongoni mwenu walipofanya wasiwasi kwamba watashindwa nailhali Allaah Ndiye Rafiki Mlinzi wao.  Basi kwa Allaah Pekee Waumini watawakali.

 

 

وَلَقَدْ نَصَرَكُمُ اللَّـهُ بِبَدْرٍ وَأَنتُمْ أَذِلَّةٌ ۖ فَاتَّقُوا اللَّـهَ لَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ ﴿١٢٣﴾

123. Kwa yakini Allaah Alikunusuruni katika Badr[38] na hali nyinyi ni wanyonge. Basi mcheni Allaah mpate kushukuru.

 

 

إِذْ تَقُولُ لِلْمُؤْمِنِينَ أَلَن يَكْفِيَكُمْ أَن يُمِدَّكُمْ رَبُّكُم بِثَلَاثَةِ آلَافٍ مِّنَ الْمَلَائِكَةِ مُنزَلِينَ ﴿١٢٤﴾

124. Pindi ulipowaambia Waumini: Je, haikutosheni ikiwa Rabb wenu Atakuongezeeni nguvu kwa Malaika elfu tatu walioteremshwa?

 

 

بَلَىٰ ۚ إِن تَصْبِرُوا وَتَتَّقُوا وَيَأْتُوكُم مِّن فَوْرِهِمْ هَـٰذَا يُمْدِدْكُمْ رَبُّكُم بِخَمْسَةِ آلَافٍ مِّنَ الْمَلَائِكَةِ مُسَوِّمِينَ ﴿١٢٥﴾ 

125. Bali, naam! Mkisubiri na mkashikamana na taqwa na hata wakikujieni kwa ghafla hivi (kukumalizeni), basi (mkitekeleza mawili hayo), Rabb wenu Atakuongezeeni nguvu kwa Malaika elfu tano waliojitia wenyewe na farasi wao alama maalum.

 

 

 وَمَا جَعَلَهُ اللَّـهُ إِلَّا بُشْرَىٰ لَكُمْ وَلِتَطْمَئِنَّ قُلُوبُكُم بِهِ ۗ وَمَا النَّصْرُ إِلَّا مِنْ عِندِ اللَّـهِ الْعَزِيزِ الْحَكِيمِ ﴿١٢٦﴾

126. Na Allaah Hakujaalia hayo isipokuwa ni bishara kwenu, na ili zitue nyoyo zenu kwayo. Na hakuna ushindi isipokuwa kutoka kwa Allaah Mwenye Enzi ya Nguvu Asiyeshindika, Mwenye Hikmah wa yote.

 

 

لِيَقْطَعَ طَرَفًا مِّنَ الَّذِينَ كَفَرُوا أَوْ يَكْبِتَهُمْ فَيَنقَلِبُوا خَائِبِينَ ﴿١٢٧﴾ 

127. Ili Akate sehemu ya waliokufuru au Awafedheheshe, warudi nyuma wakiwa wamekata tamaa.

 

 

 لَيْسَ لَكَ مِنَ الْأَمْرِ شَيْءٌ أَوْ يَتُوبَ عَلَيْهِمْ أَوْ يُعَذِّبَهُمْ فَإِنَّهُمْ ظَالِمُونَ ﴿١٢٨﴾

128. Jambo hili halikuhusu wewe, ima Apokee tawbah yao au Awaadhibu, kwani wao ni madhalimu.

 

 

وَلِلَّـهِ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۚ يَغْفِرُ لِمَن يَشَاءُ وَيُعَذِّبُ مَن يَشَاءُ ۚ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿١٢٩﴾

129. Ni vya Allaah Pekee vilivyomo katika mbingu na katika ardhi. Anamghufuria Amtakaye na Anamuadhibu Amtakaye. Na Allaah Ni Mwingi wa Kughufuria, Mwenye Kurehemu.

 

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَأْكُلُوا الرِّبَا أَضْعَافًا مُّضَاعَفَةً ۖ وَاتَّقُوا اللَّـهَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ ﴿١٣٠﴾

130. Enyi walioamini! Msile riba mkizidisha maradufu juu ya maradufu. Na mcheni Allaah mpate kufaulu.[39]

 

 

وَاتَّقُوا النَّارَ الَّتِي أُعِدَّتْ لِلْكَافِرِينَ ﴿١٣١﴾ 

131. Na uogopeni moto ambao umeandaliwa kwa makafiri.

 

 

وَأَطِيعُوا اللَّـهَ وَالرَّسُولَ لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ ﴿١٣٢﴾

132. Na mtiini Allaah na Rasuli mpate kurehemewa.

 

 

 

وَسَارِعُوا إِلَىٰ مَغْفِرَةٍ مِّن رَّبِّكُمْ وَجَنَّةٍ عَرْضُهَا السَّمَاوَاتُ وَالْأَرْضُ أُعِدَّتْ لِلْمُتَّقِينَ﴿١٣٣﴾ 

133. Na kimbilieni maghfirah kutoka kwa Rabb wenu, na Jannah upana wake ni wa mbingu na ardhi imeandaliwa kwa wenye taqwa.

 

 

الَّذِينَ يُنفِقُونَ فِي السَّرَّاءِ وَالضَّرَّاءِ وَالْكَاظِمِينَ الْغَيْظَ وَالْعَافِينَ عَنِ النَّاسِ ۗ وَاللَّـهُ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ ﴿١٣٤﴾ 

134. Ambao wanatoa (kwa ajili ya Allaah) katika hali ya wasaa na katika hali ya shida, na wanazuia ghadhabu, na wenye kusamehe watu. Na Allaah Anapenda wafanyao ihsaan.

 

 

وَالَّذِينَ إِذَا فَعَلُوا فَاحِشَةً أَوْ ظَلَمُوا أَنفُسَهُمْ ذَكَرُوا اللَّـهَ فَاسْتَغْفَرُوا لِذُنُوبِهِمْ وَمَن يَغْفِرُ الذُّنُوبَ إِلَّا اللَّـهُ وَلَمْ يُصِرُّوا عَلَىٰ مَا فَعَلُوا وَهُمْ يَعْلَمُونَ ﴿١٣٥﴾

135. Na ambao wanapofanya machafu au wakajidhulumu nafsi zao (kwa maasi), humdhukuru Allaah wakaomba maghfirah kwa madhambi yao. Na nani anayeghufuria madhambi isipokuwa Allaah. Na hawaendelei katika waliyoyafanya na hali wanajua.[40]

 

 

أُولَـٰئِكَ جَزَاؤُهُم مَّغْفِرَةٌ مِّن رَّبِّهِمْ وَجَنَّاتٌ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا ۚ وَنِعْمَ أَجْرُ الْعَامِلِينَ ﴿١٣٦﴾

136. Hao jazaa yao ni maghfirah kutoka kwa Rabb wao na Jannaat zipitazo chini yake mito, wadumu humo. Ni uzuri ulioje ujira wa watendaji (wema).

 

 

قَدْ خَلَتْ مِن قَبْلِكُمْ سُنَنٌ فَسِيرُوا فِي الْأَرْضِ فَانظُرُوا كَيْفَ كَانَ عَاقِبَةُ الْمُكذِّبِينَ ﴿١٣٧﴾

137. Kwa hakika zimekwishapita kabla yenu nyendo nyingi (kama hali  yenu), basi tembeeni katika ardhi kisha mtazame vipi ilikuwa hatima ya wenye kukadhibisha.[41]

 

 

 

هَـٰذَا بَيَانٌ لِّلنَّاسِ وَهُدًى وَمَوْعِظَةٌ لِّلْمُتَّقِينَ ﴿١٣٨﴾

138. Hii (Qur-aan) ni ubainisho kwa watu na mwongozo na mawaidha kwa wenye taqwa.

 

 

وَلَا تَهِنُوا وَلَا تَحْزَنُوا وَأَنتُمُ الْأَعْلَوْنَ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ﴿١٣٩﴾ 

139. Na wala msilegee na wala msihuzunike ilhali nyinyi mko juu mkiwa ni Waumini.

 

 

 إِن يَمْسَسْكُمْ قَرْحٌ فَقَدْ مَسَّ الْقَوْمَ قَرْحٌ مِّثْلُهُ ۚ وَتِلْكَ الْأَيَّامُ نُدَاوِلُهَا بَيْنَ النَّاسِ وَلِيَعْلَمَ اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا وَيَتَّخِذَ مِنكُمْ شُهَدَاءَ ۗ وَاللَّـهُ لَا يُحِبُّ الظَّالِمِينَ ﴿١٤٠﴾

140. Yakikupateni majeraha basi yamekwishawapata watu majeraha kama hayo. Na hizo ni siku Tunazizungusha zamu (za mabadiliko ya hali) baina ya watu, na ili Allaah Adhihirishe walioamini na Afanye miongoni mwenu Shuhadaa[42] (waliofariki katika vita vya Jihaad).  Na Allaah Hapendi madhalimu.

 

 

وَلِيُمَحِّصَ اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا وَيَمْحَقَ الْكَافِرِينَ ﴿١٤١﴾ 

141. Na ili Allaah Awajaribu (au Awatakase) walioamini  na Awafutilie mbali makafiri.

 

 

 أَمْ حَسِبْتُمْ أَن تَدْخُلُوا الْجَنَّةَ وَلَمَّا يَعْلَمِ اللَّـهُ الَّذِينَ جَاهَدُوا مِنكُمْ وَيَعْلَمَ الصَّابِرِينَ ﴿١٤٢﴾

142. Je, Mnadhani kwamba mtaingia Jannah na hali Allaah bado Hajawadhihirisha wale waliofanya Jihaad miongoni mwenu na Akadhihirisha wenye subira?

 

 

وَلَقَدْ كُنتُمْ تَمَنَّوْنَ الْمَوْتَ مِن قَبْلِ أَن تَلْقَوْهُ فَقَدْ رَأَيْتُمُوهُ وَأَنتُمْ تَنظُرُونَ ﴿١٤٣﴾

143. Na kwa yakini mlikuwa mnatamani mauti kabla hamjakutana nayo, basi mmekwishayaona na huku mnayatazama. 

 

 

وَمَا مُحَمَّدٌ إِلَّا رَسُولٌ قَدْ خَلَتْ مِن قَبْلِهِ الرُّسُلُ ۚ أَفَإِن مَّاتَ أَوْ قُتِلَ انقَلَبْتُمْ عَلَىٰ أَعْقَابِكُمْ ۚ وَمَن يَنقَلِبْ عَلَىٰ عَقِبَيْهِ فَلَن يَضُرَّ اللَّـهَ شَيْئًا ۗ وَسَيَجْزِي اللَّـهُ الشَّاكِرِينَ ﴿١٤٤﴾

144. Na Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) hakuwa isipokuwa ni Rasuli tu. Wamekwishapita kabla yake Rusuli. Je, akifa au akiuawa ndio mtageuka nyuma mrudi mlikotoka (ukafirini)? Na atakayegeuka nyuma akarudi alikotoka basi hatomdhuru Allaah kwa chochote. Na Allaah Atawalipa wenye kushukuru.

 

 

 

وَمَا كَانَ لِنَفْسٍ أَن تَمُوتَ إِلَّا بِإِذْنِ اللَّـهِ كِتَابًا مُّؤَجَّلًا ۗ وَمَن يُرِدْ ثَوَابَ الدُّنْيَا نُؤْتِهِ مِنْهَا وَمَن يُرِدْ ثَوَابَ الْآخِرَةِ نُؤْتِهِ مِنْهَا ۚ وَسَنَجْزِي الشَّاكِرِينَ ﴿١٤٥﴾ 

145. Na haiwezekani nafsi yeyote kufa isipokuwa kwa Idhini ya Allaah, kwani imeandikiwa muda wake maalumu. Na yeyote anayetaka malipo ya dunia basi Tutampa sehemu tu ya hayo (Tuliyomkadiria). Na yeyote anayetaka thawabu za Aakhirah basi Tutampa sehemu ya hayo (bila mipaka) na Tutawalipa wenye kushukuru. 

 

 

وَكَأَيِّن مِّن نَّبِيٍّ قَاتَلَ مَعَهُ رِبِّيُّونَ كَثِيرٌ فَمَا وَهَنُوا لِمَا أَصَابَهُمْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَمَا ضَعُفُوا وَمَا اسْتَكَانُوا ۗ وَاللَّـهُ يُحِبُّ الصَّابِرِينَ ﴿١٤٦﴾

146. Na Manabii wangapi walipigana vita wakiwa pamoja nao Waumini wengi waliojaa imaan ya kikweli, basi hawakulegea kwa yaliyowasibu katika Njia ya Allaah, wala hawakudhoofika na wala hawakunyong’onyea. Na Allaah Anapenda wenye subira.

 

 

وَمَا كَانَ قَوْلَهُمْ إِلَّا أَن قَالُوا رَبَّنَا اغْفِرْ لَنَا ذُنُوبَنَا وَإِسْرَافَنَا فِي أَمْرِنَا وَثَبِّتْ أَقْدَامَنَا وَانصُرْنَا عَلَى الْقَوْمِ الْكَافِرِينَ ﴿١٤٧﴾

147. Na haikuwa kauli yao isipokuwa walisema: Rabb wetu! Tughufurie madhambi yetu na upindukaji wetu mipaka katika mambo yetu, na Ithibitishe miguu yetu na Tunusuru dhidi ya watu makafiri.

 

 

فَآتَاهُمُ اللَّـهُ ثَوَابَ الدُّنْيَا وَحُسْنَ ثَوَابِ الْآخِرَةِ ۗ وَاللَّـهُ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ ﴿١٤٨﴾ 

148. Basi Allaah Akawalipa malipo ya dunia na thawabu nzuri za Aakhirah. Na Allaah Anapenda wafanyao ihsaan. 

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِن تُطِيعُوا الَّذِينَ كَفَرُوا يَرُدُّوكُمْ عَلَىٰ أَعْقَابِكُمْ فَتَنقَلِبُوا خَاسِرِينَ ﴿١٤٩﴾

149. Enyi walioamini! Mkiwatii wale waliokufuru watakurudisheni nyuma mlikotoka kisha mtageuka mkiwa wenye kukhasirika.

 

 

بَلِ اللَّـهُ مَوْلَاكُمْ ۖ وَهُوَ خَيْرُ النَّاصِرِينَ ﴿١٥٠﴾

150. Bali Allaah Ndio Rafiki Mlinzi wenu. Naye Ndiye Mbora kabisa kuliko wote wenye kusaidia.

 

 

سَنُلْقِي فِي قُلُوبِ الَّذِينَ كَفَرُوا الرُّعْبَ بِمَا أَشْرَكُوا بِاللَّـهِ مَا لَمْ يُنَزِّلْ بِهِ سُلْطَانًا ۖ وَمَأْوَاهُمُ النَّارُ ۚ وَبِئْسَ مَثْوَى الظَّالِمِينَ ﴿١٥١﴾

151. Tutatia hofu na woga katika nyoyo za waliokufuru kwa sababu ya kumshirikisha Allaah na (masanamu) ambayo Hakuyateremshia hoja wala dalili (kwamba yanastahiki kuabudiwa). Na makazi yao ni moto, na ubaya ulioje maskani ya madhalimu.

 

 

وَلَقَدْ صَدَقَكُمُ اللَّـهُ وَعْدَهُ إِذْ تَحُسُّونَهُم بِإِذْنِهِ ۖ حَتَّىٰ إِذَا فَشِلْتُمْ وَتَنَازَعْتُمْ فِي الْأَمْرِ وَعَصَيْتُم مِّن بَعْدِ مَا أَرَاكُم مَّا تُحِبُّونَ ۚ مِنكُم مَّن يُرِيدُ الدُّنْيَا وَمِنكُم مَّن يُرِيدُ الْآخِرَةَ ۚ ثُمَّ صَرَفَكُمْ عَنْهُمْ لِيَبْتَلِيَكُمْ ۖ وَلَقَدْ عَفَا عَنكُمْ ۗ وَاللَّـهُ ذُو فَضْلٍ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ ﴿١٥٢﴾

152. Na kwa yakini Allaah Amekwisha kusadikishieni Ahadi Yake mlipowaua vikali kwa Idhini Yake, mpaka mliposhindwa na mkazozana katika amri (aliyokupeni Rasuli) na mkaasi baada ya Yeye kukuonyesheni yale mnayoyapenda. Miongoni mwenu wako wenye kutaka dunia, na miongoni mwenu wako wenye kutaka Aakhirah. Kisha Akakugeuzeni nyuma mbali nao (hao maadui) ili Akujaribuni. Na kwa yakini Amekwisha kusameheni. Na Allaah Ni Mwenye Fadhila kwa Waumini.

 

 

إِذْ تُصْعِدُونَ وَلَا تَلْوُونَ عَلَىٰ أَحَدٍ وَالرَّسُولُ يَدْعُوكُمْ فِي أُخْرَاكُمْ فَأَثَابَكُمْ غَمًّا بِغَمٍّ لِّكَيْلَا تَحْزَنُوا عَلَىٰ مَا فَاتَكُمْ وَلَا مَا أَصَابَكُمْ ۗ وَاللَّـهُ خَبِيرٌ بِمَا تَعْمَلُونَ ﴿١٥٣﴾

153. Pale mlipotimka kukimbia mbali wala hamgeuki nyuma kumtazama yeyote, na Rasuli anakuiteni nyuma yenu, kisha Allaah Akakulipizeni dhiki juu ya dhiki ili (kukufundisheni) msihuzunike kwa yaliyokupiteni na wala kwa yaliyokusibuni. Na Allaah Ni Mjuzi wa Khabari za dhahiri na siri kwa yale myatendayo.

 

 

ثُمَّ أَنزَلَ عَلَيْكُم مِّن بَعْدِ الْغَمِّ أَمَنَةً نُّعَاسًا يَغْشَىٰ طَائِفَةً مِّنكُمْ ۖ وَطَائِفَةٌ قَدْ أَهَمَّتْهُمْ أَنفُسُهُمْ يَظُنُّونَ بِاللَّـهِ غَيْرَ الْحَقِّ ظَنَّ الْجَاهِلِيَّةِ ۖ يَقُولُونَ هَل لَّنَا مِنَ الْأَمْرِ مِن شَيْءٍ ۗ قُلْ إِنَّ الْأَمْرَ كُلَّهُ لِلَّـهِ ۗ يُخْفُونَ فِي أَنفُسِهِم مَّا لَا يُبْدُونَ لَكَ ۖ يَقُولُونَ لَوْ كَانَ لَنَا مِنَ الْأَمْرِ شَيْءٌ مَّا قُتِلْنَا هَاهُنَا ۗ قُل لَّوْ كُنتُمْ فِي بُيُوتِكُمْ لَبَرَزَ الَّذِينَ كُتِبَ عَلَيْهِمُ الْقَتْلُ إِلَىٰ مَضَاجِعِهِمْ ۖ وَلِيَبْتَلِيَ اللَّـهُ مَا فِي صُدُورِكُمْ وَلِيُمَحِّصَ مَا فِي قُلُوبِكُمْ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُورِ ﴿١٥٤﴾

154. Kisha Akakuteremshieni amani baada ya dhiki; usingizi unaofunika kundi miongoni mwenu na kundi likawashughulisha nafsi zao wakamdhania Allaah pasi na haki dhana ya kijahili, wanasema: Je, tuna amri yoyote sisi katika jambo hili? Sema: Hakika amri yote ni ya Allaah. Wanaficha katika nafsi zao yale wasiyokubainishia. Wanasema: Lau tungelikuwa tuna amri yoyote katika jambo basi tusingeliuliwa hapa. Sema: Lau mngelikuwa majumbani mwenu, bila shaka wangejitokeza wale walioandikiwa kuuawa kwenye mahali pa kuangukia wafe. Ili Allaah Ayajaribu yale yaliyomo katika vifua vyenu na Atakase yale yaliyomo katika nyoyo zenu. Na Allaah Anayajua vyema yaliyomo vifuani.

 

 

إِنَّ الَّذِينَ تَوَلَّوْا مِنكُمْ يَوْمَ الْتَقَى الْجَمْعَانِ إِنَّمَا اسْتَزَلَّهُمُ الشَّيْطَانُ بِبَعْضِ مَا كَسَبُوا ۖ وَلَقَدْ عَفَا اللَّـهُ عَنْهُمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ حَلِيمٌ ﴿١٥٥﴾ 

155. Hakika wale waliokengeuka miongoni mwenu siku yalipokutana makundi mawili (kwa mapambano), hakika hapana ila shaytwaan aliwatelezesha kutokana na baadhi ya waliyoyachuma. Na kwa yakini Allaah Aliwasamehe. Hakika Allaah Ni Mwingi wa Kughufuria, Mvumilivu.   

 

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَكُونُوا كَالَّذِينَ كَفَرُوا وَقَالُوا لِإِخْوَانِهِمْ إِذَا ضَرَبُوا فِي الْأَرْضِ أَوْ كَانُوا غُزًّى لَّوْ كَانُوا عِندَنَا مَا مَاتُوا وَمَا قُتِلُوا لِيَجْعَلَ اللَّـهُ ذَٰلِكَ حَسْرَةً فِي قُلُوبِهِمْ ۗ وَاللَّـهُ يُحْيِي وَيُمِيتُ ۗ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ ﴿١٥٦﴾ 

156. Enyi walioamini! Msiwe kama wale waliokufuru na wakasema kuhusu ndugu zao waliposafiri katika ardhi au walipokuwa vitani: Lau wangelikuwa kwetu wasingelikufa na wala wasingeliuawa, ili Allaah Afanye hayo (yaliyoeleweka vibaya) kuwa majuto katika nyoyo zao. Na Allaah Anahuisha na Anafisha. Na Allaah Anayaona vyema myatendayo.

 

 

وَلَئِن قُتِلْتُمْ فِي سَبِيلِ اللَّـهِ أَوْ مُتُّمْ لَمَغْفِرَةٌ مِّنَ اللَّـهِ وَرَحْمَةٌ خَيْرٌ مِّمَّا يَجْمَعُونَ ﴿١٥٧﴾

157. Na kama mtauliwa katika Njia ya Allaah au mtakufa, basi bila shaka Maghfirah kutoka kwa Allaah na Rehma ni bora kuliko yale wanayoyakusanya.

 

 

وَلَئِن مُّتُّمْ أَوْ قُتِلْتُمْ لَإِلَى اللَّـهِ تُحْشَرُونَ ﴿١٥٨﴾

158. Na kama mtakufa au mtauliwa, bila shaka kwa Allaah mtakusanywa.

 

 

فَبِمَا رَحْمَةٍ مِّنَ اللَّـهِ لِنتَ لَهُمْ ۖ وَلَوْ كُنتَ فَظًّا غَلِيظَ الْقَلْبِ لَانفَضُّوا مِنْ حَوْلِكَ ۖ فَاعْفُ عَنْهُمْ وَاسْتَغْفِرْ لَهُمْ وَشَاوِرْهُمْ فِي الْأَمْرِ ۖ فَإِذَا عَزَمْتَ فَتَوَكَّلْ عَلَى اللَّـهِ ۚإِنَّ اللَّـهَ يُحِبُّ الْمُتَوكِّلِينَ ﴿١٥٩﴾

159. Basi ni kwa sababu ya Rehma kutoka kwa Allaah ndio umekuwa mpole kwao (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم).[43] Na lau ungelikuwa mjeuri mwenye moyo mgumu, wangelitawanyika mbali nawe. Basi wasamehe na waombee maghfirah na washauri katika mambo. Na unapoazimia, basi tawakali kwa Allaah. Hakika Allaah Anapenda wanaotawakali.

 

 

 

إِن يَنصُرْكُمُ اللَّـهُ فَلَا غَالِبَ لَكُمْ ۖ وَإِن يَخْذُلْكُمْ فَمَن ذَا الَّذِي يَنصُرُكُم مِّن بَعْدِهِ ۗ وَعَلَى اللَّـهِ فَلْيَتَوَكَّلِ الْمُؤْمِنُونَ ﴿١٦٠﴾ 

160. Akikunusuruni Allaah, basi hakuna wa kukushindeni. Na Akikutelekezeni, basi nani atakunusuruni baada Yake? Na kwa Allaah Pekee watawakali Waumini.

 

 

 وَمَا كَانَ لِنَبِيٍّ أَن يَغُلَّ ۚ وَمَن يَغْلُلْ يَأْتِ بِمَا غَلَّ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۚ ثُمَّ تُوَفَّىٰ كُلُّ نَفْسٍ مَّا كَسَبَتْ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ ﴿١٦١﴾

161. Na haikuwa (ni tabia) kwa Nabiy yeyote kukhini (ngawira). Na yeyote atakayekhini atakuja na kile alichokikhini Siku ya Qiyaamah. Kisha kila nafsi italipwa kamilifu yale iliyoyachuma, nao hawatodhulumiwa.

 

 

أَفَمَنِ اتَّبَعَ رِضْوَانَ اللَّـهِ كَمَن بَاءَ بِسَخَطٍ مِّنَ اللَّـهِ وَمَأْوَاهُ جَهَنَّمُ ۚ وَبِئْسَ الْمَصِيرُ ﴿١٦٢﴾ 

162. Je, aliyefuata Radhi za Allaah ni kama aliyestahiki ghadhabu kutoka kwa Allaah?!  Na makazi yake ni Jahannam, na ubaya ulioje mahali pa kuishia!  

 

 

هُمْ دَرَجَاتٌ عِندَ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ بَصِيرٌ بِمَا يَعْمَلُونَ ﴿١٦٣﴾

163. Wao wana vyeo mbali mbali mbele ya Allaah. Na Allaah Anayaona vyema yale wayatendayo.

 

 

لَقَدْ مَنَّ اللَّـهُ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ إِذْ بَعَثَ فِيهِمْ رَسُولًا مِّنْ أَنفُسِهِمْ يَتْلُو عَلَيْهِمْ آيَاتِهِ وَيُزَكِّيهِمْ وَيُعَلِّمُهُمُ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَإِن كَانُوا مِن قَبْلُ لَفِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ ﴿١٦٤﴾

164. Kwa yakini Allaah Amewafanyia fadhila Waumini pale Alipomtuma kwao Rasuli miongoni mwao wenyewe, anawasomea Aayaat Zake na anawatakasa na anawafunza Kitabu na Hikmah (Sunnah), japokuwa walikuwa kabla katika upotofu bayana.

 

 

أَوَلَمَّا أَصَابَتْكُم مُّصِيبَةٌ قَدْ أَصَبْتُم مِّثْلَيْهَا قُلْتُمْ أَنَّىٰ هَـٰذَا ۖ قُلْ هُوَ مِنْ عِندِ أَنفُسِكُمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿١٦٥﴾

165. Ulipokusibuni msiba ingawa nyinyi mliwasibu (maadui) mara mbili yake mlisema: Umetoka wapi huu? Sema: Huo ni kutoka kwenu wenyewe. Hakika Allaah Ni Muweza juu ya kila kitu.  

 

 

وَمَا أَصَابَكُمْ يَوْمَ الْتَقَى الْجَمْعَانِ فَبِإِذْنِ اللَّـهِ وَلِيَعْلَمَ الْمُؤْمِنِينَ ﴿١٦٦﴾

166. Na yale yaliyokusibuni siku yalipokutana makundi mawili (katika Uhud), basi ni kwa Idhini ya Allaah na ili Adhihirishe Waumini.

 

 

وَلِيَعْلَمَ الَّذِينَ نَافَقُوا ۚ وَقِيلَ لَهُمْ تَعَالَوْا قَاتِلُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ أَوِ ادْفَعُوا ۖ قَالُوا لَوْ نَعْلَمُ قِتَالًا لَّاتَّبَعْنَاكُمْ ۗ هُمْ لِلْكُفْرِ يَوْمَئِذٍ أَقْرَبُ مِنْهُمْ لِلْإِيمَانِ ۚ يَقُولُونَ بِأَفْوَاهِهِم مَّا لَيْسَ فِي قُلُوبِهِمْ ۗ وَاللَّـهُ أَعْلَمُ بِمَا يَكْتُمُونَ ﴿١٦٧﴾

167. Na ili Adhihirishe wale waliofanya unafiki na wakaambiwa: Njooni mpigane katika Njia ya Allaah au (angalau) lindeni. Wakasema: Lau tungelijua kuwa kuna kupigana bila shaka tungelikufuateni. Wao siku hiyo walikuwa karibu zaidi na ukafiri kuliko imaan. Wanasema kwa midomo yao yasiyokuwemo ndani ya nyoyo zao. Na Allaah Anajua zaidi wanayoyaficha.

 

 

الَّذِينَ قَالُوا لِإِخْوَانِهِمْ وَقَعَدُوا لَوْ أَطَاعُونَا مَا قُتِلُوا ۗ قُلْ فَادْرَءُوا عَنْ أَنفُسِكُمُ الْمَوْتَ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿١٦٨﴾ 

168. Wale waliowaambia ndugu zao nao wakakaa (wasiende vitani): Lau wangelitutii basi wasingeliuawa. Sema: Basi ziondoleeni nafsi zenu mauti mkiwa ni wakweli.

 

 

وَلَا تَحْسَبَنَّ الَّذِينَ قُتِلُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ أَمْوَاتًا ۚ بَلْ أَحْيَاءٌ عِندَ رَبِّهِمْ يُرْزَقُونَ ﴿١٦٩﴾ 

169. Na wala usiwadhanie kabisa wale waliouawa katika Njia ya Allaah[44] kuwa ni wafu, bali wahai, wako kwa Rabb wao wanaruzukiwa.

 

 

فَرِحِينَ بِمَا آتَاهُمُ اللَّـهُ مِن فَضْلِهِ وَيَسْتَبْشِرُونَ بِالَّذِينَ لَمْ يَلْحَقُوا بِهِم مِّنْ خَلْفِهِمْ أَلَّا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ ﴿١٧٠﴾ 

170. Wanafurahia kwa Aliyowapa Allaah kwa Fadhila Zake na wanawashangilia ambao bado hawajaungana nao, walio nyuma yao, kwamba: Hakuna khofu juu yao na wala hawatohuzunika.

 

 

يَسْتَبْشِرُونَ بِنِعْمَةٍ مِّنَ اللَّـهِ وَفَضْلٍ وَأَنَّ اللَّـهَ لَا يُضِيعُ أَجْرَ الْمُؤْمِنِينَ ﴿١٧١﴾

171. Wanashangilia Neema kutoka kwa Allaah na Fadhila na kwamba Allaah Hapotezi ujira wa Waumini.

 

 

الَّذِينَ اسْتَجَابُوا لِلَّـهِ وَالرَّسُولِ مِن بَعْدِ مَا أَصَابَهُمُ الْقَرْحُ ۚ لِلَّذِينَ أَحْسَنُوا مِنْهُمْ وَاتَّقَوْا أَجْرٌ عَظِيمٌ ﴿١٧٢﴾

172. Wale waliomwitikia Allaah na Rasuli baada ya kuwasibu majeraha. Kwa wale waliofanya ihsaan miongoni mwao na wakawa na taqwa watapa ujira mkuu kabisa.

 

 

الَّذِينَ قَالَ لَهُمُ النَّاسُ إِنَّ النَّاسَ قَدْ جَمَعُوا لَكُمْ فَاخْشَوْهُمْ فَزَادَهُمْ إِيمَانًا وَقَالُوا حَسْبُنَا اللَّـهُ وَنِعْمَ الْوَكِيلُ ﴿١٧٣﴾

173. Wale walioambiwa na watu: Hakika watu wamejumuika dhidi yenu, basi waogopeni. Lakini hilo liliwazidishia imaan wakasema: Hasbuna-Allaah! (Allaah Anatutosheleza) Mzuri Alioje Mtegemewa.[45]  

 

 

فَانقَلَبُوا بِنِعْمَةٍ مِّنَ اللَّـهِ وَفَضْلٍ لَّمْ يَمْسَسْهُمْ سُوءٌ وَاتَّبَعُوا رِضْوَانَ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ ذُو فَضْلٍ عَظِيمٍ ﴿١٧٤﴾

174. Basi wakarudi na Neema kutoka kwa Allaah na Fadhila, halijawagusa ovu lolote na wakafuatilia Radhi za Allaah.  Na Allaah Ni Mwenye Fadhila kuu kabisa.

 

 

 إِنَّمَا ذَٰلِكُمُ الشَّيْطَانُ يُخَوِّفُ أَوْلِيَاءَهُ فَلَا تَخَافُوهُمْ وَخَافُونِ إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ ﴿١٧٥﴾

175. Hakika huyo ni shaytwaan anawakhofisha marafiki wake wandani. Basi msiwakhofu, na nikhofuni Mimi mkiwa ni Waumini.

 

 

وَلَا يَحْزُنكَ الَّذِينَ يُسَارِعُونَ فِي الْكُفْرِ ۚ إِنَّهُمْ لَن يَضُرُّوا اللَّـهَ شَيْئًا ۗ يُرِيدُ اللَّـهُ أَلَّا يَجْعَلَ لَهُمْ حَظًّا فِي الْآخِرَةِ ۖ وَلَهُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ ﴿١٧٦﴾ 

176. Wala wasikuhuzunishe kabisa (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم) wale wanaokimbilia katika ukafiri. Hakika wao hawamdhuru Allaah kitu chochote. Allaah Anakusudia Asiwawekee fungu lolote Aakhirah, na watapata adhabu kuu kabisa.

 

 

إِنَّ الَّذِينَ اشْتَرَوُا الْكُفْرَ بِالْإِيمَانِ لَن يَضُرُّوا اللَّـهَ شَيْئًا وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿١٧٧﴾ 

177. Hakika wale waliobadilisha ukafiri badala ya imaan, hawatomdhuru Allaah kitu chochote, nao watapata adhabu iumizayo.

 

 

وَلَا يَحْسَبَنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا أَنَّمَا نُمْلِي لَهُمْ خَيْرٌ لِّأَنفُسِهِمْ ۚ إِنَّمَا نُمْلِي لَهُمْ لِيَزْدَادُوا إِثْمًا ۚ وَلَهُمْ عَذَابٌ مُّهِينٌ ﴿١٧٨﴾

178. Na wala wasidhanie kabisa wale waliokufuru kwamba muhula Tunaowapa (wa kustarehe) ni kheri kwao. Hakika Tunawapa muhula ili wazidi (kuchuma) dhambi. Nao watapata adhabu ya kudhalilisha.

 

 

 

مَّا كَانَ اللَّـهُ لِيَذَرَ الْمُؤْمِنِينَ عَلَىٰ مَا أَنتُمْ عَلَيْهِ حَتَّىٰ يَمِيزَ الْخَبِيثَ مِنَ الطَّيِّبِ ۗ وَمَا كَانَ اللَّـهُ لِيُطْلِعَكُمْ عَلَى الْغَيْبِ وَلَـٰكِنَّ اللَّـهَ يَجْتَبِي مِن رُّسُلِهِ مَن يَشَاءُ ۖ فَآمِنُوا بِاللَّـهِ وَرُسُلِهِ ۚ وَإِن تُؤْمِنُوا وَتَتَّقُوا فَلَكُمْ أَجْرٌ عَظِيمٌ ﴿١٧٩﴾

179. Haiwi kwa Allaah kuwaacha Waumini katika hali mliyo nayo mpaka Apambanue mbaya na mwema. Na haiwi kwa Allaah Akujulisheni ya ghaibu, lakini Allaah Humteua katika Rusuli Wake Amtakaye. Basi mwaminini Allaah na Rusuli Wake. Na mkiamini (imaan ya kweli) na mkawa na taqwa basi mtapata ujira mkuu kabisa.

 

 

 وَلَا يَحْسَبَنَّ الَّذِينَ يَبْخَلُونَ بِمَا آتَاهُمُ اللَّـهُ مِن فَضْلِهِ هُوَ خَيْرًا لَّهُم ۖ بَلْ هُوَ شَرٌّ لَّهُمْ ۖ سَيُطَوَّقُونَ مَا بَخِلُوا بِهِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۗ وَلِلَّـهِ مِيرَاثُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۗ وَاللَّـهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ ﴿١٨٠﴾

180. Wala wasidhani kabisa wale wanaofanya ubakhili kwa yale Aliyowapa Allaah katika Fadhila Zake kwamba hayo ni kheri kwao, bali ni shari kwao. Watafungwa kongwa yale waliyoyafanyia ubakhili Siku ya Qiyaamah. [46] Na Ni Wake Allaah Pekee urithi wa mbingu na ardhi. Na Allaah kwa yale myatendayo Ni Mjuzi wa Khabari za dhahiri na siri.

 

 

لَّقَدْ سَمِعَ اللَّـهُ قَوْلَ الَّذِينَ قَالُوا إِنَّ اللَّـهَ فَقِيرٌ وَنَحْنُ أَغْنِيَاءُ ۘ سَنَكْتُبُ مَا قَالُوا وَقَتْلَهُمُ الْأَنبِيَاءَ بِغَيْرِ حَقٍّ وَنَقُولُ ذُوقُوا عَذَابَ الْحَرِيقِ ﴿١٨١﴾

181. Kwa yakini Allaah Ameisikia kauli ya wale (Mayahudi) waliosema: Hakika Allaah ni fakiri na sisi ni matajiri.[47] Tutayaandika waliyoyasema na kuua kwao Manabii pasi na haki na Tutasema: Onjeni adhabu ya kuunguza!

 

 

ذَٰلِكَ بِمَا قَدَّمَتْ أَيْدِيكُمْ وَأَنَّ اللَّـهَ لَيْسَ بِظَلَّامٍ لِّلْعَبِيدِ ﴿١٨٢﴾

182. Hivyo ni kwa sababu ya yale iliyotanguliza mikono yenu na kwamba Allaah Si dhalimu kabisa kwa waja.

 

 

الَّذِينَ قَالُوا إِنَّ اللَّـهَ عَهِدَ إِلَيْنَا أَلَّا نُؤْمِنَ لِرَسُولٍ حَتَّىٰ يَأْتِيَنَا بِقُرْبَانٍ تَأْكُلُهُ النَّارُ ۗ قُلْ قَدْ جَاءَكُمْ رُسُلٌ مِّن قَبْلِي بِالْبَيِّنَاتِ وَبِالَّذِي قُلْتُمْ فَلِمَ قَتَلْتُمُوهُمْ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ ﴿١٨٣﴾

183. (Hao ndio) Wale waliosema: Hakika Allaah Ametuahidi kwamba tusimwamini Rasuli yeyote mpaka atuletee dhabihu itakayoangamizwa na moto.  Sema: Kwa yakini walikujieni Rusuli kabla yangu kwa hoja bayana, na hata kwa haya ambayo mmesema, basi kwa nini mliwaua mkiwa ni wakweli?

 

 

فَإِن كَذَّبُوكَ فَقَدْ كُذِّبَ رُسُلٌ مِّن قَبْلِكَ جَاءُوا بِالْبَيِّنَاتِ وَالزُّبُرِ وَالْكِتَابِ الْمُنِيرِ ﴿١٨٤﴾

184. Basi wakikukadhibisha (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم), kwa yakini wamekadhibishwa Rusuli kabla yako. Walikuja na hoja bayana na Vitabu vya Hukumu, na Kitabu chenye Nuru.

 

 

 

كُلُّ نَفْسٍ ذَائِقَةُ الْمَوْتِ ۗ وَإِنَّمَا تُوَفَّوْنَ أُجُورَكُمْ يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۖ فَمَن زُحْزِحَ عَنِ النَّارِ وَأُدْخِلَ الْجَنَّةَ فَقَدْ فَازَ ۗ وَمَا الْحَيَاةُ الدُّنْيَا إِلَّا مَتَاعُ الْغُرُورِ ﴿١٨٥﴾

185. Kila nafsi itaonja mauti. Na hakika mtalipwa kikamilifu ujira wenu Siku ya Qiyaamah. Basi atakayewekwa mbali na moto na akaingizwa Jannah, huyo kwa yakini amefuzu. Na uhai wa dunia si lolote ila ni starehe ya udanganyifu.

 

 

لَتُبْلَوُنَّ فِي أَمْوَالِكُمْ وَأَنفُسِكُمْ وَلَتَسْمَعُنَّ مِنَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ مِن قَبْلِكُمْ وَمِنَ الَّذِينَ أَشْرَكُوا أَذًى كَثِيرًا ۚ وَإِن تَصْبِرُوا وَتَتَّقُوا فَإِنَّ ذَٰلِكَ مِنْ عَزْمِ الْأُمُورِ ﴿١٨٦﴾

186. Bila shaka mtajaribiwa katika mali zenu na nafsi zenu, na bila shaka mtasikia kutoka kwa wale waliopewa Kitabu kabla yenu na kutoka kwa wale walioshirikisha udhia mwingi. Lakini mkisubiri na mkawa na taqwa basi hakika hayo ni katika mambo ya kuazimiwa.

 

 

 وَإِذْ أَخَذَ اللَّـهُ مِيثَاقَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ لَتُبَيِّنُنَّهُ لِلنَّاسِ وَلَا تَكْتُمُونَهُ فَنَبَذُوهُ وَرَاءَ ظُهُورِهِمْ وَاشْتَرَوْا بِهِ ثَمَنًا قَلِيلًا ۖ فَبِئْسَ مَا يَشْتَرُونَ ﴿١٨٧﴾

187. Na pale Alipochukua Allaah fungamano la wale waliopewa Kitabu (Allaah Akawaambia): Bila shaka mtakibainisha kwa watu na wala hamtokificha. Lakini walikitupa nyuma ya migongo yao na wakakibadilisha kwa thamani ndogo. Basi ubaya ulioje kwa yale wanayoyanunua!  

 

 

 

لَا تَحْسَبَنَّ الَّذِينَ يَفْرَحُونَ بِمَا أَتَوا وَّيُحِبُّونَ أَن يُحْمَدُوا بِمَا لَمْ يَفْعَلُوا فَلَا تَحْسَبَنَّهُم بِمَفَازَةٍ مِّنَ الْعَذَابِ ۖ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿١٨٨﴾ 

188. Usiwadhanie kabisa wale wanaofurahia (mabaya) waliyoyafanya na wanapenda wasifiwe kwa (mazuri) wasiyoyatenda. Usiwadhanie kabisa kuwa watasalimika na adhabu. Nao watapata adhabu iumizayo.

 

 

وَلِلَّـهِ مُلْكُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۗ وَاللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ ﴿١٨٩﴾

189. Ni Wake Allaah ufalme wa mbingu na ardhi. Na Allaah juu ya kila kitu Ni Muweza.

 

 

إِنَّ فِي خَلْقِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَاخْتِلَافِ اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ لَآيَاتٍ لِّأُولِي الْأَلْبَابِ ﴿١٩٠﴾ 

190. Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi, na mabadiliko ya mfuatano wa usiku na mchana, bila shaka ni Aayaat (Ishara, Dalili, Mazingatio) kwa wenye akili.[48]

 

 

الَّذِينَ يَذْكُرُونَ اللَّـهَ قِيَامًا وَقُعُودًا وَعَلَىٰ جُنُوبِهِمْ وَيَتَفَكَّرُونَ فِي خَلْقِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ رَبَّنَا مَا خَلَقْتَ هَـٰذَا بَاطِلًا سُبْحَانَكَ فَقِنَا عَذَابَ النَّارِ ﴿١٩١﴾ 

191. Ambao wanamdhukuru Allaah wakiwa wima, au wamekaa au wamejinyoosha, na wanatafakari katika kuumbwa mbingu na ardhi (wakisema): Rabb wetu, Hukuumba haya bure, Utakasifu Ni Wako! Basi Tukinge na adhabu ya moto.

 

 

رَبَّنَا إِنَّكَ مَن تُدْخِلِ النَّارَ فَقَدْ أَخْزَيْتَهُ ۖ وَمَا لِلظَّالِمِينَ مِنْ أَنصَارٍ ﴿١٩٢﴾

192. Rabb wetu! Hakika Umuingizaye motoni, kwa yakini Umemhizi. Na madhalimu hawana wasaidizi wa kuwanusuru.

 

 

رَّبَّنَا إِنَّنَا سَمِعْنَا مُنَادِيًا يُنَادِي لِلْإِيمَانِ أَنْ آمِنُوا بِرَبِّكُمْ فَآمَنَّا ۚ رَبَّنَا فَاغْفِرْ لَنَا ذُنُوبَنَا وَكَفِّرْ عَنَّا سَيِّئَاتِنَا وَتَوَفَّنَا مَعَ الْأَبْرَارِ ﴿١٩٣﴾

193. Rabb wetu! Hakika sisi tumemsikia mwitaji anaita kwenye imaan kwamba: Mwaminini Rabb wenu. Basi tukaamini.  Rabb wetu!  Tghufurie madhambi yetu na Tufutie mabaya yetu na Tufishe pamoja na Waumini wema.

 

 

 رَبَّنَا وَآتِنَا مَا وَعَدتَّنَا عَلَىٰ رُسُلِكَ وَلَا تُخْزِنَا يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۗ إِنَّكَ لَا تُخْلِفُ الْمِيعَادَ ﴿١٩٤﴾

194. Rabb wetu! Tupe pia Uliyotuahidi kupitia Rusuli Wako, wala Usituhizi Siku ya Qiyaamah. Hakika Wewe Huendi kinyume na ahadi.

 

 

 

فَاسْتَجَابَ لَهُمْ رَبُّهُمْ أَنِّي لَا أُضِيعُ عَمَلَ عَامِلٍ مِّنكُم مِّن ذَكَرٍ أَوْ أُنثَىٰ ۖ بَعْضُكُم مِّن بَعْضٍ ۖ فَالَّذِينَ هَاجَرُوا وَأُخْرِجُوا مِن دِيَارِهِمْ وَأُوذُوا فِي سَبِيلِي وَقَاتَلُوا وَقُتِلُوا لَأُكَفِّرَنَّ عَنْهُمْ سَيِّئَاتِهِمْ وَلَأُدْخِلَنَّهُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ ثَوَابًا مِّنْ عِندِ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ عِندَهُ حُسْنُ الثَّوَابِ ﴿١٩٥﴾

195. Rabb wao Akiwajibu:  Hakika Mimi Sipotezi amali za mtendaji yeyote yule miongoni mwenu akiwa mwanamume au mwanamke, nyinyi kwa nyinyi. Basi wale waliohajiri na wakatolewa majumbani mwao na wakaudhiwa katika Njia Yangu, wakapigana na wakauliwa, bila shaka Nitawafutia makosa yao, na kwa yakini Nitawaingiza Jannaat zipitazo chini yake mito.  Hayo ni malipo kutoka kwa Allaah.  Na kwa Allaah kuna thawabu nzuri kabisa.

 

 

 لَا يَغُرَّنَّكَ تَقَلُّبُ الَّذِينَ كَفَرُوا فِي الْبِلَادِ ﴿١٩٦﴾

196. Kusikubabaishe kabisa kuzunguka makafiri kwa vishindo huku na kule katika ardhi.

 

 

مَتَاعٌ قَلِيلٌ ثُمَّ مَأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ ۚ وَبِئْسَ الْمِهَادُ ﴿١٩٧﴾ 

197. Ni starehe ndogo, kisha makazi yao ni Jahannam. Na ni mahala pabaya mno pa kupumzikia.

 

 

 لَـٰكِنِ الَّذِينَ اتَّقَوْا رَبَّهُمْ لَهُمْ جَنَّاتٌ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الْأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا نُزُلًا مِّنْ عِندِ اللَّـهِ ۗ وَمَا عِندَ اللَّـهِ خَيْرٌ لِّلْأَبْرَارِ ﴿١٩٨﴾

198. Lakini wale waliomcha Rabb wao watapata Jannaat zipitazo chini yake mito, wadumu humo. Ni mapokezi kutoka kwa Allaah. Na vilioko kwa Allaah ni bora zaidi kwa ajili ya wema watiifu.

 

 

وَإِنَّ مِنْ أَهْلِ الْكِتَابِ لَمَن يُؤْمِنُ بِاللَّـهِ وَمَا أُنزِلَ إِلَيْكُمْ وَمَا أُنزِلَ إِلَيْهِمْ خَاشِعِينَ لِلَّـهِ لَا يَشْتَرُونَ بِآيَاتِ اللَّـهِ ثَمَنًا قَلِيلًا ۗ أُولَـٰئِكَ لَهُمْ أَجْرُهُمْ عِندَ رَبِّهِمْ ۗ إِنَّ اللَّـهَ سَرِيعُ الْحِسَابِ ﴿١٩٩﴾

199. Na miongoni mwa Watu wa Kitabu wamo ambao kwa hakika wanamwamini Allaah na yaliyoteremshwa kwenu, na yaliyoteremshwa kwao, wananyenyekea kwa Allaah, na hawabadilishi Aayaat za Allaah kwa thamani ndogo. Hao watapata ujira wao kwa Rabb wao. Hakika Allaah Ni Mwepesi Mno wa Kuhesabu.

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اصْبِرُوا وَصَابِرُوا وَرَابِطُوا وَاتَّقُوا اللَّـهَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ ﴿٢٠٠﴾

200. Enyi walioamini! Subirini na zidini kuvuta subira, na bakieni imara na mcheni Allaah ili mpate kufaulu.[49]

 

 

 

 

[1] الحروف المقطعة  (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah):

 

Hizi ni herufi zinazojulikana kama الحروف المقطعة  (Al-Huruwf Al-Muqatw-twa’ah), ambazo hakuna ajuaye maana zake isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى). Rejea Tanbihi ya Al-Baqarah (2:1).

 

[2] Al-Hayyu Al-Qayyuwm: Jina Tukufu Kabisa La Allaah (سبحانه وتعالى):

 

Rejea Tanbihi Al-Baqarah (2:255).

 

[3] Nyoyo Zenye Upotovu, Shaka, Na Kadhaalika:

 

Rejea Al-Hajj (22:46) kwenye faida na rejea nyenginezo.

 

 

[4] Aayaat Muhkamaat Na Mutashaabihaat:

 

Aayaat Muhkamaat: Ni Aayaat ambazo maana zake zinafahamika kiwepesi, hazina mushkila wala utata, na dalili zake ziko wazi.   Ama Aayaat Mutashaabihaat, hizi ni Aayah ambazo ni ngumu kufahamika, na zinawatatanisha baadhi ya watu wasio na ilimu ya kutosha. Hivyo warudie kwa ‘Ulamaa kuelewa maana zake.

 

Mama wa Waumini ‘Aaishah (رضي الله عنها) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) aliisoma Aayah hii:

هُوَ الَّذِي أَنزَلَ عَلَيْكَ الْكِتَابَ مِنْهُ آيَاتٌ مُّحْكَمَاتٌ هُنَّ أُمُّ الْكِتَابِ وَأُخَرُ مُتَشَابِهَاتٌ

“Yeye Ndiye Aliyekuteremshia Kitabu. Humo mna Aayaat zenye maana wazi, hizo ndio msingi wa Kitabu, na nyinginezo zisizokuwa wazi maana zake…”

mpaka mwisho wa Aayah. Kisha Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akasema: Ee ‘Aaishah! Pindi utakapowaona wale ambao wanafuata zile Aayaat ambazo haziko wazi zaidi, basi fahamu kuwa hao ndio wale ambao Allaah Amewataja katika hii Aayah, basi tahadharini nao.” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

[5] Tofauti Ya Ikabu Na Adhabu: Rejea Al-Hashr (59:4).

 

[6] Kuomba Maghfirah Kabla Ya Alfajiri: Rejea Adh-Dhaariyaat (51:18).

 

[7]  Dini Ya Kiislamu Ni Dini Pekee Anayoiridhia Allaah (سبحانه وتعالى):    

 

Dini ya Kiislamu ni Dini ambayo Allaah (سبحانه وتعالى)     Amewachagulia Waja Wake, na Akawatumiliza kwayo Rusuli Wake, na ambayo Hakubali isipokuwa Dini hii ya Uislamu. Nayo ni kunyenyekea kwa Allaah (عزّ وجلّ) kwa utiifu na kujisalimisha Kwake kwa kumwabudu Yeye Pekee na kuwafuata Rusuli wote katika yale waliyotumiliziwa kwayo katika zama zote, mpaka wakakhitimishiwa kwa Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) ambaye baada ya kutumilizwa kwake, Allaah (عزّ وجلّ) Hakubali dini yoyote ile isipokuwa Uislamu.  Na hata pia kwa Rusuli wote waliomtangulia Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) kabla, wote hao waliulingania Uislamu (Tawhiyd) ingawa sharia tu ndizo zilizotofautiana kati ya Rasuli na Rasuli kwa mujibu wa hali na mazingira, na wote walikuwa ni Waislamu.

 

Khitilafu ya Watu wa Kitabu; Mayahudi na Manaswara iliyowafanya watengane wawe mapote na makundi, haikutokea ila baada ya kuthibiti hoja juu yao kwa kupelekwa Rusuli wao na kuteremshwa Vitabu. Hiyo ilitokana na uadui na uhasidi kwa kutafuta mafao ya dunia. [Tafsiyr Al-Muyassar]

 

Hivyo basi ni kama Anavyosema Allaah (سبحانه وتعالى) pia katika Aayah namba (85):

وَمَن يَبْتَغِ غَيْرَ الْإِسْلَامِ دِينًا فَلَن يُقْبَلَ مِنْهُ وَهُوَ فِي الْآخِرَةِ مِنَ الْخَاسِرِينَ ﴿٨٥﴾

“Na yeyote anayetaka dini isiyokuwa ya Kiislamu haitokubaliwa kwake, naye katika Aakhirah atakuwa miongoni mwa waliokhasirika.”  

 

[8] Maana Ya Baghi Katika Qur-aan:

 

Rejea Ash-Shuwraa (42:14) kupata maana zake mbalimbali

[9]  Onyo Kwa Mayahudi Na Manaswaara Kwa Kutokumuamini Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم):

 

Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  amesema: “Naapa kwa Ambaye nafsi yangu imo Mikononi Mwake, hatosikia yeyote yule kuhusu mimi katika ummah huu; Yahudi wala Naswara, kisha akafariki bila ya kuamini yale ambayo nimetumwa nayo, isipokuwa atakuwa miongoni mwa watu wa motoni.” [Al-Bukhaariy]

 

Na pia amesimulia Jaabir bin ‘Abdillaah (رضي الله عنهما): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)  amesema: “Na alikuwa (kila) Nabiy akitumwa kwa watu wake pekee, lakini mimi nimetumwa kwa watu wote.” [Al-Bukhaariy]

 

[10] Allaah (سبحانه وتعالى) Anatoa Kilicho Hai Kutokana Na Kilicho Mfu, Na Anatoa Kilicho Mfu Kutokana Na Kilicho Hai:

 

Rejea Al-An’aam (6:95), Ar-Ruwm (30:19).

 

[11] Aqiydah Sahihi Ya Ahlus-Sunnah Wal-Jamaa’ah Ni Kuthibisha Sifa Za Allaah.

 

Aayah tukufu imetaja Nafsi ya Allaah (سبحانه وتعالى). Na ‘Aqiydah sahihi ni kuithibitisha hivyo hivyo bila ya kuipa maana nyenginezo. Rejea Huwd (11:47) kwenye maelezo bayana.

 

[12]  Kumpenda Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) Ni Kufuata Sunnah Zake Na Kujiepusha Na Yasiyo Sunnah:

 

Aayah hii tukufu inathibitisha kuwa mapenzi ya Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) hayawezi kutimia isipokuwa kwa kufuata Sunnah zake. Ni hoja ya wazi pia kwa wanaodai kuwa wanampenda Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) lakini wakawa hawafuati matendo yake (Sunnah zake) na kinyume chake wanafanya bid’ah katika Dini kama kusoma mawlid, khitmah, talqiyn (kumsomea maiti), mikusanyiko ya kuomba duaa, kusheherekea maadhimisho na kumbukumbu za miaka, kusherehekea siku wanazosherehekea wasiokuwa Waislamu, na yote mengineyo yasiyokuwemo katika sharia. Na kufuata Sunnah zake ni kutenda yale ambayo ameyasema, ameyatenda au amayeridhia kutendwa; kuanzia khulqa (tabia) zake na jinsi alivyotaamuli na wake zake na Swahaba zake na watumishi wake. Jinsi alivyolingania (da’awah) watu wake, na hata jinsi alivyotendeana na maadui zake. Vile vile jinsi alivyotekeleza ibaada zake za Swalaah za mchana na za usiku. Alivyokuwa akiomba duaa, na jinsi alivyokuwa akileta Adhkaar zake (za kumdhukuru Allaah). Pia alivyokuwa akifunga (Swawm) Jumatatu, Alkhamiys na Masiku Meupe. Hali kadhaalika aliyokuwa akiyatenda na kuyatamka katika siku moja kuanzia kuamka kwake hadi usiku ikijumuisha aina ya chakula chake na jinsi alivyokuwa akila, na alivyokuwa akiamka usiku, na matendo yote mengineyo katika uhai wake.  Akasisitiza mno kushikamana na Sunnah zake katika Hadiyth zifuatazo:  

 

Amesimulia Abu Najiyh Al-‘Irbaadhw bin Saariyah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  alitupa mawaidha mazito (yenye maana kubwa), nyoyo zikaogopa na macho yakabubujikwa machozi. Tukasema: Ee Rasuli wa Allaah! Yanaonekana kama kwamba mawaidha ya kutuaga, basi tuusie.  Akasema: “Nakuusieni kuwa na taqwa kwa Allaah, na usikivu, na utiifu japokuwa mtaongozwa na mtumwa. Hakika atakayeishi umri mrefu miongoni mwenu ataona ikhtilafu nyingi. Kwa hiyo, shikamaneni na Sunnah zangu na mwenendo wa Makhalifa Waongofu, yashikilieni kwa magego (mambo yao). Na tahadharini na mambo yenye kuzushwa, kwani kila uzushi ni bid’ah, na kila bid-ah ni upotofu, na kila upotofu ni motoni.” [Abuu Daawuwd, At-Tirmidhiy, na amesema Hadiyth Hasan Swahiyh]

 

Na katika kila khutbah alitanguliza kusema: “Ammaa Ba’adu. Hakika maneno bora kabisa ni Kitabu cha Allaah (Qur-aan), na mwongozo bora kabisa ni mwongozo wa Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم), na uovu zaidi wa mambo ni yale yenye kuzushwa (bila dalili ya kisharia), na kila bid'ah ni upotofu. [Muslim]

 

[13] Kuzaliwa Kwa Maryam Mama Wa Nabiy ‘Iysaa, Kutajwa Nabiy Zakariyyaa, Kuzaliwa Yahyaa Na kuzaliwa ‘Iysaa (عليهم السّلام):

 

Kuanzia Aayah (35-45) ni maelezo kuhusu   Bi Hannah ambaye alikuwa ni mke wa ‘Imraan na kuzaliwa kwa Maryam. Imeanzia hapa Bi Hannah alipoweka nadhiri ya mimba aliyoibeba baada ya kufariki mumewe ‘Imraan.  Akamzaa mtoto na kumpa jina la Maryam likimaanisha “Mtumishi wa Allaah.” Dada yake Hannah kwa maana ni khaalat (mama mdogo au mkubwa) wa Maryam, alikuwa ni mke wa Nabiy Zakariyyaa (عليه السّلام).  Naye Zakariyyaa (عليه السّلام) ndiye aliyemlea Maryam baada ya kufariki baba yake ‘Imraan.  Kwa hiyo Zakariyyaa (عليه السّلام) ni mume wa khaalat yake Maryam.  Aayah zinaendelea kutaja muujiza wa Maryam vile alivyokuwa  anaruzukiwa vyakula na Allaah (سبحانه وتعالى).  Aayah zinataja pia muujiza wa kuzaliwa Nabiy Yahyaa (عليه السّلام) ilhali baba yake na mama yake walikuwa ni vizee vikongwe. Pia Aayah zimetaja muujiza wa  kuzaliwa kwa Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام).

 

[14] Aina Ya Vyakula Alivyoruzukiwa Maryam:   

 

Zakariyyaa (عليه السّلام)   alimkuta akiwa na matunda ya majira ya joto katika majira ya baridi, na matunda ya majira ya baridi katika majira ya joto. [Tafsiyr Ibn Kathiyr]

 

[15] Neno Kun! (Kuwa!) Rejea Al-Baqarah (2:117).  

 

[16] Malaika Kutajwa Kwa Wingi Ilhali Ni Jibriyl (عليه السّلام):

 

Katika Sarufi ya Lugha ya Kiarabu, wingi unaweza kurejelea umoja. Na katika Aayah hii bila shaka amekusudiwa Jibriyl (عليه السّلام) ambaye daima ndiye mwenye kuteremsha Wahyi wa Allaah (سبحانه وتعالى) kwa Rusuli na Waja Wake, kama vile Jibriyl alivyomjia Maryam kumbashiria mwana katika Suwrah hii ya Aal-‘Imraan (3:45),  na Suwrat Maryam (19:17-21). Mfano pia Allaah (سبحانه وتعالى) Anapotaja kwa wingi “Sisi” ilhali Anakusudia Yeye Pekee Mwenyewe kama katika Kauli Yake Allaah (سبحانه وتعالى):

إِنَّا نَحْنُ نَزَّلْنَا الذِّكْرَ وَإِنَّا لَهُ لَحَافِظُونَ ﴿٩﴾

“Hakika Sisi Tumeteremsha Adh-Dhikra (Qur-aan) na hakika Sisi bila shaka Ndio Wenye Kuihifadhi.” [Al-Hjr (15:9)]

 

[17] Maryam Ni Miongoni Mwa Wanawake Bora Kabisa:

 

Allaah (سبحانه وتعالى) Anamtakasa  na kumsifia Maryam katika Aayah hizi. Na katika Hadiyth ametajwa kuwa ni miongoni mwa wanawake bora kabisa:

 

عَنْ أَبِي مُوسَى الأَشْعَرِيِّ رضى الله عنه قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم: (( كَمَلَ مِنَ الرِّجَالِ كَثِيرٌ، وَلَمْ يَكْمُلْ مِنَ النِّسَاءِ إِلاَّ مَرْيَمُ بِنْتُ عِمْرَانَ، وَآسِيَةُ امْرَأَةُ فِرْعَوْنَ، وَفَضْلُ عَائِشَةَ عَلَى النِّسَاءِ كَفَضْلِ الثَّرِيدِ عَلَى سَائِرِ الطَّعَامِ ))‏

Amesimulia Abuu Muwsaa Al-Ash’ariyy (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Wanaume wengi wamefikia daraja ya ukamilifu lakini hakuna mwanamke aliyefikia daraja hiyo isipokuwa Aasiyah mke wa Firawni, na Maryam bint 'Imraan. Na ubora wa 'Aaishah (رضي الله عنها) kwa wanawake wengine ni kama mfano wa ubora wa thariyd kwa vyakula vingine.” [Al-Bukhaariy na wengineo]

Rejea pia Suwrah Maryam (19-16). Rejea kisa chake kwa urefu na kuhusu kumzaa kwake Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام) katika Suwrah Maryam (19-16-36).

 

[18] Kalamu Zilitupwa Katika Mto Kupiga Kura:

 

Kura ilipigwa baina ya Nabiy Zakariyyaa (عليه السّلام) na Marabi wa Bayt Al-Maqdis kwa sababu kila mmoja alipendelea kumlea Maryam. Basi wakapiga kura kwa kutupa kalamu zao mtoni na kwamba  yeyote kati yao ambaye kalamu yake haitaibuka katika maji, ndiye atayestahiki  kumlea Maryam. Basi walipotupa kalamu zao mtoni, maji yalizamisha kalamu zote  isipokuwa kalamu ya Nabiy Zakariyyaa (عليه السّلام) ilibakia pale pale ikielea.

 

[19] Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام) Alifanya Miujiza Kwa Idhini Ya Allaah Wala Sio Kwa Uwezo Wake Tu:

 

Katika Aayah hii, na ya Suwrah Al-Maaidah (5:110), ni hoja na dalili ya wazi kabisa kwamba Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام) ni mja wa Allaah na kwamba hakuwa na Uwezo wa kipekee katika kuleta miujiza iliyotajwa katika Aayah hizo mbili. Hivyo ni kwa sababu, alikuwa kila anapoleta miujiza hiyo iliyotajwa, alimalizia kwa kusema: “Kwa Idhini ya Allaah.”  Basi hii ni hoja bayana na raddi kwa Manaswara wanaodai kuwa Nabiy Iysaa ni mungu kwa miujiza hii ilhali yote imetokana na Uwezo wa Allaah (سبحانه وتعالى).

 

[20] Allaah (سبحانه وتعالى) Hana Sifa Mbaya Isipokuwa Anarudisha Ubaya (Muqaabalah):

 

Sifa ya makri (njama) huthibitishwa kwa Allaah (سبحانه وتعالى) kwa njia ya muqaabalah, kwa maana: ukipanga mabaya, Naye Ataamiliana nawe kwa ubaya, na ubaya utakurudia wewe mwenyewe. Na ukipanga mazuri, Naye Ataamiliana nawe kwa uzuri, Atakusaidia na Atakulipa mema. Na Sifa hii kama zilivyo zingine, huthibitishwa kwa Allaah kwa maana inayoendana na kulaikiana na Allaah (عزّ وجلّ).   Kwa hiyo, Allaah Anamfanyia makri (njama) yule anayestahiki, na pia yule ambaye anawafanyia makri (njama) waja Wake Waumini.

 

Hali kadhaalika, kumfanyia istihzai Allaah (عزّ وجلّ) au Waja Wake, au kuwadhihaki, au aina yoyote ya shutuma kama kudai kwamba Mkono wa Allaah umefumbwa kama katika Aayah ya Al-Maaidah (5:64) na mengineyo. Haya yote na mengineyo mabaya, Allaah Huwarudishia wahusika wake kwa adhabu za kidunia, au kwa namna ambayo Yeye Allaah Anaona kuwa inanasibiana na makosa yao.

 

[21] Uthibitisho Kuwa Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام) Yu Hai Mbinguni Na Atateremka Duniani Kama Alama Kubwa Za Qiyaamah:

 

Allaah (سبحانه وتعالى) Alimnyanyua Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام) kuelekea mbinguni akiwa hai, na wala hakuuliwa kabla ya hapo. Na atakuja kuteremka duniani zama za mwisho, atamuua Masiyh Ad-Dajjaal, atawaua nguruwe wote, atavunja misalaba yote, ataondosha kodi, hatokubali isipokuwa Uislamu, na atahukumu kwa sharia ya Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم). Dalili ipo katika Suwrat An-Nisaa (4:157-159).

 

Aayah hii tukufu ni dalili ya wazi kwa wanaodai kwamba neno la مُتَوَفِّيكَ  lina maana “kukufisha kikamilifu.”  Neno hilo hilo Amelitaja Allaah (سبحانه وتعالى) katika Al-An’aam (6:60) na Az-Zumar (39:42):

 

وَهُوَ الَّذِي يَتَوَفَّاكُم بِاللَّيْلِ وَيَعْلَمُ مَا جَرَحْتُم بِالنَّهَارِ ثُمَّ يَبْعَثُكُمْ فِيهِ لِيُقْضَىٰ أَجَلٌ مُّسَمًّى ۖ

“Naye Ndiye Anayekufisheni usiku (mnapolala) na Anajua yale yote mnayoyafanya mchana, kisha Anakufufueni humo ili utimizwe muda maalumu uliokadiriwa.” [Al-An'aam (6:60)]

 

اللَّـهُ يَتَوَفَّى الْأَنفُسَ حِينَ مَوْتِهَا وَالَّتِي لَمْ تَمُتْ فِي مَنَامِهَا ۖ فَيُمْسِكُ الَّتِي قَضَىٰ عَلَيْهَا الْمَوْتَ وَيُرْسِلُ الْأُخْرَىٰ إِلَىٰ أَجَلٍ مُّسَمًّى ۚ

“Allaah Huzichukua roho wakati wa kufa kwake, na zile zisizokufa katika usingizi wake, kisha Huzizuia ambazo Amezikidhia mauti, na Huzirudisha nyingine mpaka muda maalumu uliokadiriwa.” [Az-Zumar (39:42)]

 

Hapo tunafahamu kwamba, mtu anapolala anachukuliwa au anafishwa usingizini na kurudishwa katika uhai kwa kuwa roho yake inachukuliwa na ndio inayojulikana kuwa ni Al-Mawt As-Sughraa (mauti madogo). Kwa dalili pia kutoka katika mafunzo ya Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) katika nyiradi za kulala; mojawapo ni kusema pindi mtu anapoingia kulala:

بِاسْـمِكَ اللّهُـمَّ أَموتُ وَأَحْـيا

”Kwa Jina Lako Ee Allaah ninakufa na ninakuwa hai”.

 

Na anapoamka aseme:

الحَمْـدُ لِلّهِ الّذي أَحْـيانا بَعْـدَ ما أَماتَـنا وَإليه النُّـشور

”Himdi Anastahiki Allaah Ambaye Ametupa uhai baada ya kutufisha, na Ni Kwake tu kufufuliwa”.

 

Rejea pia Az-Zumar (39:42).

 

[22] Kuumbwa Kwa Nabiy Aadam (عليه السّلام) Na Kuzaliwa Nabiy Iysaa (عليه السّلام):

 

Kuumbwa kwa Nabiy Aadam (عليه السّلام)  ni muujiza mkubwa zaidi kulikoni kuzaliwa kwa Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام) kwa sababu Nabiy Aadam (عليه السّلام)  hakuzaliwa na baba wala mama bali ameumbwa kwa udongo tu! Ama Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام)  amezaliwa na mama bila ya baba. Basi hii ni dalili, ushahidi na hoja ya wazi kabisa na raddi kwa Manaswara wanaodai kuwa Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام) ni mungu kwa sababu ya kuzaliwa kwake kimuujiza.

 

[23] Mubaahalah:

 

Kilugha ni kuomba kwa unyenyekevu na juhudi. Na katika istilahi ni kuomba Laana ya Allaah imfikie mmoja kati ya watu wanaokhitilafiana katika jambo.

 

Wajumbe wa kikanisa wa Najraan, walitumwa waende Madiynah kwa lengo la kubishana na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) kwamba  Nabiy ‘Iysaa (عليه السّلام) ni mwana wa Allaah. Walipofika,  Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), akawataka mubaahalah,  kwamba wakusanyike pande mbili;  wao na familia zao, na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) na familia yake kisha waapize Laana ya Allaah iwaangukie waongo na wakanushaji. Lakini hakuna hata mmoja wao aliyejitokeza  katika mubaahalah huo, kwa sababu walijua vilivyo kuwa Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم) ni mkweli na Risala aliyotumwa nayo na Allaah  ni Risala ya haki. Hivyo basi wakaogopa laana ya Allaah kuwafikia. Hapo basi uongo wao ukadhihirika. Rejea Aayah (61). 

 

[24] Dini Ya Nabiy Ibraahiym (عليه السّلام) Ni Dini Ya Kiislamu:

 

Amesimulia Ibn ’Umar (رضي الله عنهما)  kwamba: Zayd bin ‘Amr bin Nufayl, alitoka kuelekea Sham, akiulizia kuhusu dini ili aifuate. Akakutana na mwanazuoni wa ki-Yahudi, akamuuliza kuhusu dini na akasema: Mimi huenda nikaingia dini yenu, basi nielezee. Akasema: Huwezi kuwa katika dini yetu mpaka uchukue fungu lako katika Ghadhabu za Allaah. Akasema Zayd: Mimi hakuna ninachokikimbia ila Ghadhabu za Allaah, wala sivumilii Ghadhabu za Allaah kwa kitu chochote, na vipi nitaweza! Je, utanielekeza (dini) nyingine? Akasema (mwanachuoni wa ki-Yahudi): Sijui ila dini iliyotakasika, akasema Zayd: Ni (dini) ipi hiyo iliyotakasika? Akasema: Dini ya Ibraahiym, hakuwa Myahudi wala Mnaswara, wala haabudu ila Allaah. Akatoka Zayd akakutana na mwanazuoni wa ki-Naswara, akamuuliza kama vile (alivyomuuliza Myahudi), akasema: Huwezi kuwa katika dini yetu mpaka uchukue fungu lako katika Laana za Allaah. Akasema: Mimi hakuna ninachokimbia ila nakimbia Laana za Allaah, wala sivumilii Laana za Allaah wala Ghadhabu Zake kwa chochote, na vipi nitaweza! Je, utanielekeza (dini) nyingine? Akasema: sijui ila (Dini) iliyotakasika. Akasema: Ni ipi hiyo (dini) iliyotakasika? Akasema: Dini ya Ibraahiym, hakuwa Myahudi wala Mnaswara wala haabudu ila Allaah. Basi Zayd alipoona maneno yao kuhusu Ibraahiym (عليه السّلام)  aliondoka sehemu hiyo, na alipokuwa nje aliinua mikono yake akasema: “Ee Allaah, mimi nashuhudia niko katika Dini ya Ibraahiym.” [Al-Bukhaariy (3827)]

Rejea Al-Baqarah (2:135).

 

[25] Al-Hukma:

 

Ni hukumu, mamlaka, ufakihi wa sharia za Dini n.k.  

 

[26] Maana Ya Rabbaaniyyuwna (Marabi) Na Sifa Zake:

 

Rabbaaniy maana yake ya asili ni mlezi. Na baadhi ya Wafasiri wa Qur-aan wamesema kuwa wanalea watu kwa sifa zao njema na wanawatengenezea mambo yao.

 

Na wengi kati ya Salaf wametaja maana kadhaa zifuatazo:

 

Ni ‘Ulamaa na wenye kumwabudu Allaah (سبحانه وتعالى). Ni wenye ikhlaasw (kumtakasia Allaah Dini). Ni Maimaam (Viongozi) Fuqahaa (wenye ilimu ya hali ya juu kabisa) na wanafanyia kazi ilimu zao. Ni Maimaam (Viongozi) Swalihina wenye taqwa ya hali ya juu. Ni wenye busara na hikmah. Ni wenye zuhd (kuipa mgongo dunia). Ni wanyenyekevu kwa Allaah (سبحانه وتعالى) na kwa watu. Ni wapole mno. Ni wenye kuwafundisha watu mambo mepesi kwanza kabla yaliyo magumu.  

 

Na baadhi ya Sifa zao, Rabbaaniyyuwn wameelezwa katika Qur-aan kuwa ni wenye kuamrisha mema na kukataza maovu [Al-Maaidah (5:63)] Pia, wana uthibati katika Jihaad na subra katika mitihani na dhiki [Aal-‘Imraan (3:146)] pamoja  na sifa njema nyenginezo. Basi kwa sababu ya sifa hizo ndipo Allaah (سبحانه وتعالى) Anawaambia Rusuli Wake wawaamrishe watu wawe Rabbaaniyyuwn kuwafundisha watu ilimu waliyonayo na kukanusha kuwa Rusuli Wake Allaah (سبحانه وتعالى) wametaka waabudiwe na watu au eti wamewaamrisha watu wawaabudu. 

 

[27] Dalili Kuwa Al-Khidhwr Hayuko Hai:

 

Aayah hii ni miongoni mwa dalili za kufariki kwa Khidhwr (عليه السّلام)  na kuwa yeye amekwishakufa na si kama wanavyodai Masufi kuwa Khidhwr yupo hai. Na lau kama angelikuwa yupo hai, basi angesimama kumnusuru Nabiy Muhammad  (صلى الله عليه وآله وسلم)   kwa kauli na matendo.

 

[28] Al-Asbaatw: Rejea Al-Baqarah (2:136).

 

[29] Dini Ya Kiislamu Ni Dini Pekee Anayoiridhia Allaah (سبحانه وتعالى) : Rejea Suwrah hii Aal-’Imraan (3:19-20).

 

[30] Israaiyl Ni Nabiy Ya’quwb  (عليه السّلام) :

Israaiyl ni Nabiy Ya’quwb  (عليه السّلام), na watoto wake na vizazi vyao wametajwa kuwa ni Bani Israaiyl kama katika Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):   

 

  أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ أَنْعَمَ اللَّـهُ عَلَيْهِم مِّنَ النَّبِيِّينَ مِن ذُرِّيَّةِ آدَمَ وَمِمَّنْ حَمَلْنَا مَعَ نُوحٍ وَمِن ذُرِّيَّةِ إِبْرَاهِيمَ وَإِسْرَائِيلَ وَمِمَّنْ هَدَيْنَا وَاجْتَبَيْنَا  

“Hao ndio ambao Allaah Amewaneemesha miongoni mwa Manabii katika uzao wa Aadam, na wale Tuliowapandisha (katika jahazi) pamoja na Nuwh na katika uzao wa Ibraahiym na (uzao wa) Israaiyl (Ya’quwb) na wale Tuliowaongoa na Tukawateua.” [Maryam (19:58)]

 

[31] Fadhila Na Sifa Za Ibraahiym (عليه السّلام): Rejea An-Nahl (16:120).

 

[32] Nyumba Ya Kwanza Kwa Ajili Ya Ibaadah (Al-Ka’bah): Rejea Al-An’aam (6:92)

 

[33]  Maana Ya Kushikamana Na Kamba Ya Allaah Bila Kufarikiana.

 

Kushikamana na Kamba ya Allaah bila ya kufarikiana imekusudiwa kubakia katika Swiraatw Al-Mustaqiym (njia iliyonyooka). Rejea Tanbihi ya Al-Faatihah (1:6) (6:153). 

 

Na pia Kauli ya Allaah (عزّ وجلّ) :

 

وَأَنَّ هَـٰذَا صِرَاطِي مُسْتَقِيمًا فَاتَّبِعُوهُ ۖ وَلَا تَتَّبِعُوا السُّبُلَ فَتَفَرَّقَ بِكُمْ عَن سَبِيلِهِ ۚ ذَٰلِكُمْ وَصَّاكُم بِهِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ ﴿١٥٣﴾

“Na kwamba hii ndio Njia Yangu iliyonyooka, basi ifuateni. Na wala msifuate njia nyinginezo zitakufarikisheni na Njia Yake. Hivyo ndivyo Alivyokuusieni (Allaah) kwayo mpate kuwa na taqwa.” [Al-An’aam (6:153)]

 

Pia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ametahadharisha mno kuhusu kuthibitika katika Swiraatw Al-Mustaqiym ambayo inamaanisha kutokutoka nje ya mafunzo ya Qur-aan na Sunnah. Miongoni mwa maonyo yake ni Hadiyth ifuatayo:

 

Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Hakika Allaah Anawaridhia mambo matatu na Anachukia kwenu mambo matatu: Anawaridhia mumwabudu Yeye, wala msimshirikishe kwa chochote, na mshikamane nyote na Kamba ya Allaah wala msifarikiane. Na anachukia kwenu uvumi, kuuliza sana na   kupoteza mali.” [Muslim, na katika riwayaah: “Na muwanasihi wenye kuwatawalia mambo yenu.” Swahiyh Adab Al-Mufrad (343)]

 

[34]  Makundi Sabini Na Tatu Yataingia Motoni Isipokuwa Kundi Moja Tu!

 

Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Wamegawanyika Mayahudi katika mapote sabini na moja, na wakagawanyika Manaswara katika mapote sabini na mbili, na ummah wangu utagawanyika mapote sabini na tatu. Yote hayo yataingia motoni ila moja tu.” Swahaba waliuliza: Ni lipi hilo ee Rasuli wa Allaah?  Akasema: “Ni lile nililokuwemo mimi na Swahaba zangu.” [Ahmad, Abuu Daawuwd, At-Tirmidhiy na Ad-Daarimiy]

 

Rejea pia Al-Faatihah (1:6), Aal-‘Imraan (3:31) na Al-An’aam (6:153).

 

[35] Ummah Wa Kiislamu Ni Ummah Bora Kabisa:

 

Hadiyth kadhaa zimetaja fadhila za ummah huu wa Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم). Miongoni mwa fadhila hizo ni:

 

Mu’aawiyah bin Haydah Al-Qash-riyy (رضي الله عنه) amehadithia kutoka kwa baba yake kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Nyinyi mnakamilisha ummah sabini. Nyinyi ndio bora wao na ndio watukufu zaidi mbele ya Allaah (عزّ وجلّ).” [Ahmad, At-Tirmidhiy, Ibn Maajah, Al-Haakim, na wengineo kwa riwaayah tofauti kidogo taz. Swahiyh Al-Jaami’ (2301), Swahiyh At-Tirmidhiy (3001)]

 

Na pia, Abuu Hurayrah (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Sisi (Waislamu) ni wa mwisho (kuja) na (tutakuwa) wa mwisho Siku ya Qiyaamah na wa mwanzo kuingia Jannah…” [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

[36]  Amri Ya Kuamrisha Mema Na Kukataza Maovu:

 

Kuamrisha mema na kukataza maovu ni sifa ya ummah huu wa Kiislamu, nayo imesisitizwa katika Aayah kadhaa za Qur-aan, na pia katika Sunnah imesisitizwa mno. Miongoni mwazo ni Hadiyth zifuatazo:

 

Hudhayfah bin Al-Yamaani (رضي الله عنه) amehadithia kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Naapa kwa Yule Ambaye nafsi yangu imo Mkononi Mwake! Mtaamrisha mema na mtakataza maovu au sivyo Allaah Atakuleteeni adhabu kutoka Kwake, kisha mtamuomba wala Hatokuitikieni.” [Ahmad na At-Tirmidhy - Swahiyh At-Tirmdhiy (2169), Swahiyh Al-Jaami’ (7070)]

 

Pia: Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (رضي الله عنه) amehadithia kwamba: “Nilimsikia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akisema: “Atakayeona munkari (uovu) basi aubadilishe kwa mkono wake, na asipoweza basi kwa ulimi wake, na asipoweza basi kwa moyo wake (achukizwe) na huo ni udhaifu wa imaan.”  [Muslim]

 

Kuamrishana mema na kukatazana maovu ni moja ya sifa za ummah huu wetu wa Kiislamu. Rejea Suwrah hii Aal-‘Imraan (3:110).

 

[37] Ghazwat-Uhud: Vita Vitukufu Vya Uhud:

 

Vita vitukufu vya Uhud vimetajwa katika Aayah zifuatazo za Suwrah hii Aal-‘Imraan:

 

(121-128), (139-146), (148), (150), (152-153), (157-158), (166), (168-171). Na Allaah Mjuzi zaidi.

 

Vita vya Uhud ni katika vita vikubwa vya Jihaad. Vilifanyika mwaka mmoja baada ya Vita vya Badr. Waislamu walipigana na makafiri wa Kiquraysh siku ya Jumamosi mnamo mwezi wa Shawwaal mwaka wa tatu baada ya Hijrah.

 

Vimeitwa Uhud kwa sababu vilitokea katika maeneo ya mlima wa Uhud. 

 

Washirikina hawakuwa na raha baada ya kushindwa Vita vya Badr, wakawa na raghba na ghamu kubwa ya kulipiza kisasi kwa yale yaliyowasibu katika Vita vya Badr, kwa kuuliwa wengi wao wakiwemo vigogo vyao. Hivyo basi Maquraysh walikuwa na unyonge, huzuni na ghadhabu kubwa. Basi wakawa wakikutana katika vikao vyao wakipanga namna ya kulipa kisasi dhidi ya Waislamu waweze kuondosha huzuni na ghadhabu zao.

 

Waliokuwa na nashati na hamasa zaidi katika kutayarisha vita hivi upande wa washirikina, ni ‘Ikrimah bin Abiy Jahl, Safwaan bin Umayyah, Abu Sufyaan bin Harb na ‘Abdullaah bin Abi Rabiy’ah.

 

Walikusanya mali nyingi na wakatayarisha jeshi kubwa lililokusanya watu wa makabila maarufu ya Bani Kinaanah na Tihaamah na mabedui wa Ahaabish na makabila mbali mbali ya Kiarabu, waliowajaza chuki nyoyoni mwao. 

 

Al-’Abbaas (رضي الله عنه) ammi yake Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم), baada ya kuona jeshi likiondoka, alimtumia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) ujumbe wa kumjulisha nyendo za washirikina na idadi yao. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)  akashauriana na Swahaba wake kama wapambane na Maquraysh au wabakie Madiynah, basi rai ya wengi ilikuwa ni kutoka kupambana na Maquraysh,   na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)  akakubali rai hiyo.  

 

Idadi ya jeshi la Waislamu ilikuwa ni elfu moja. Imepokewa kwamba wanafiki walijitenga na jeshi la Waislamu kabla ya vita, na idadi yao ilikuwa mia tatu, kwa hivyo walibakia Waislamu mia saba tu waliobaki kukabiliana na Vita vya Uhud. Na katika Suwrah hii wanafiki wamefichuliwa siri zao za dhahiri na siri za kutokutaka kushiriki katika Vita vya Uhud. 

 

Waislamu walipofika kwenye uwanja wa vita, Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) aligawanya jeshi katika vikosi vitatu. Cha kwanza kilikuwa ni kikosi cha Muhajirina, na bendera yake ilibebwa na Musw-ab bin ‘Umayr (رضي الله عنه). Kikosi cha pili kilikuwa ni kikosi cha Al-Aws na kiliongozwa na Usayd bin Hudhwayr (رضي الله عنه). Na kikosi cha tatu kilikuwa ni kikosi cha Khazraj kikiongozwa na Al-Hubbaab bin Mundhir (رضي الله عنه).  Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akawapanga Waislamu hamsini wa kupiga  mishale juu ya mlima. Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akawataka wabakie hapo wasiondoke. Mapigano yalipoanza, ushindi ulikuwa kwanza wa Waislamu, na jeshi la washirikina likaanza kurudi nyuma. Lakini wapiga mishale katika jeshi la Waislamu wakafikiri kwamba vita vimeisha. Wakateremka kutoka mlimani juu ya kwamba waliamrishwa awali wasiondoke, wakikimbilia kuteka ngawira za makafiri  waliokuwa wanakimbilia mbali. Wakamuasi Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) kwa hili.  Wakabakia hapo mlimani waliobakia katika Waumini wa kweli. 

 

Khaalid bin Waliyd ambaye alikuwa miongoni mwa viongozi wa Quraysh, akachukua fursa ya kuwateremkia Waislamu. Akauzunguka mlima ili awazunguke Waislamu kwa nyuma, na kwa vile alikuwa na sifa ya ushujaa wa kupigana, alishambulia kwa ujasiri, na hapo basi wimbi la vita likageuka, Waislamu wengi wakauliwa na ushindi ukawa kwa makafiri.  

 

Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alijeruhiwa katika vita hivi, uso wake ulijaa damu. Swahaba Twalhah Bin ‘Abdillaah (رضي الله عنه) alijiweka karibu na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) akiulinda uso wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) dhidi ya mishale. Twalhah (رضي الله عنه) alipigwa mara mbili kichwani na akapata majeraha mengi mwilini mwake. Aliitwa “Shahidi aliye hai.” Rejea Al-Ahzaab (33:23). Na Abu Bakr (رضي الله عنه) aliita siku hiyo ya Uhud kuwa ni siku ya Twalhah (رضي الله عنه) kwa sababu ya kumhami kwake Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) bila ya kujali kujeruhiwa.

 

Swahaba sabiini waliuawa kama Shahidi, akiwemo Hamzah bin ‘Abdil-Muttwalib (رضي الله عنه)  ambaye ni ammi yake Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):

Amesimulia Al-Baraa Bin ‘Aazib (رضي الله عنه): Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alimchagua ‘Abdullaah bin Jubayr (رضي الله عنه) kuwa jemadari wa kikosi cha miguu (warusha mishale) ambao walikuwa hamsini siku ya Vita vya Uhud. Akawaagizia: “Bakieni mahali penu, na msiondoke hata mkiona ndege wakitunyakua, mpaka niwatumie (mjumbe). Na mkiona tumewashinda kaumu na kuwafanya kukimbia, hata hivyo msiondoke mpaka niwatumie (mjumbe).” Kisha tukawashinda. Wa-Allaahi niliwaona wanawake wakikimbia na huku wamenyanyua nguo zao, hivyo vikuku vya miguu kuonekana na miundi yao. Wakasema Swahaba wa ‘Abdullaah bin Jubayr (رضي الله عنه): “Ngawira! Enyi watu, ngawira! Swahaba zenu wameshinda, mnasubiri nini?” ‘Abdullaah bin Jubayr akasema: “Je, mmesahau aliyowaambia Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)?” Wakasema: “Wa-Allaahi, tutakwenda kwa watu (yaani maadui) tukusanye sehemu yetu ya ngawira!” Walipokwenda kwao, walilazimishwa kugeuka na huku wameshindwa. Wakati huo Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa nyuma yao akiwaita. Wanaume kumi na mbili (12) tu ndio walobakia pamoja na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)  na wakauliwa sabiini miongoni mwetu. [Al-Bukhaariy – Kitaab Al-Jihaad]

 

Hayo ni matokeo ya kumuasi Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم). Anataja Allaah (سبحانه وتعالى)  katika Aayah: (152-153).

 

Baadhi Ya Ghazwah (Vita Vitukufu Vya Jihaad) Vilivyotajwa Katika Qur-aan:

 

Ghazwat-Uhud: Suwrah hii ya Aal-‘Imraan (3). 

 

Ghazwat-Badr: Suwrah hii ya Aal-‘Imraan (3) na Al-Anfaal (8).

 

Ghazwat-Khandaq au Al-Ahzaab (33).     

 

Ghazwat-Tabuwk:  At-Tawbah: (9).

 

Ghazwat-Hudaybiyah:  Al-Fat-h (48).

 

Ghazwat-Khaybar:  Al-Fat-h (48)

 

Ghazwat-Hunayn: At-Tawbah (9).

 

Na vita vinginevyo, ambavyo vimetajwa katika Suwrah nyenginezo. kama vita dhidi ya Bani Nadhwiyr ambavyo vimetajwa katika Suwrah Al-Hashr (59). Na pia Fat-h Makkah (Ufunguzi wa Makkah) ambavyo vimetajwa katika Suwrah An-Naswr (110). Na kuna Hadiyth kadhaa pia zilizotaja kuhusu vita vitukufu vyote hivyo.

 

[38]  Maana Ya Badr:

 

‘Ulamaa wametofautiana kuhusu maana ya ‘Badr’. Baadhi yao wamesema ni jina la mtu, na wengine wamesema ni jina la kisima. Sehemu hiyo iko baina ya Makkah na Madiynah, na umbali kati yake na Madiynah ni kilometa mia na khamsini. Na Allaah Ndiye Mjuzi zaidi. Rejea pia Al-Anfaal (8:7) kuna maelezo bayana kuhusu Vita hivi vitukufu.

 

[39]  Haramisho La Riba Na Matahadharisho: Rejea Al-Baqarah: (2:275–279).

 

[40]  Kuomba Maghfirah Na Kutubia Baada Ya Kutenda Maasi:

 

Rejea An-Nisaa (4:110) na At-Tahriym (66:8).

 

[41]  Waumini Kuliwazwa Katika Vita Vya Jihaad Kwamba Watembee Katika Ardhi Wakaone Hatima Ya Waliokadhibisha Na Nusra Kuwa Ya Waumini, Na Hii Ndio Desturi Ya Allaah (سبحانه وتعالى):

 

Aayah hii na zinazofuatia zinaendelea kutaja kuhusu Vita Vitukufu vya Uhud pale Waumini walipokuwa katika shida, dhiki na mtihani wa kujeruhiwa vitani na baadhi yao kuuliwa. Hivyo Allaah (عزّ وجلّ) Anawaliwaza Waja Wake Waumini na kuwaambia watembee katika sehemu ambapo kuna athari za Adhabu za Allaah (سبحانه وتعالى) kwa makafiri wa nyumati za nyuma. Na kwamba vizazi na nyumati nyingi zilizopita kabla yao, walitahiniwa na kujaribiwa. Walijaribiwa kwa kupigana na makafiri, wakaendelea kumahanika na kuhangaika mpaka Allaah (عزّ وجلّ) Akawaletea Nusra yake na mwisho mwema, na ushindi ukawa wa Waja Wake wema. Na kwamba makafiri waliangamizwa pamoja na majumba yao, wakala khasara na wakahizika! Basi hiyo ndiyo Desturi ya Allaah (سبحانه وتعالى) ya kuwaadhibu makafiri na badala yake kuwajaalia Nusra na ushindi Waumini. Hivyo basi, Waumini katika Vita vya Uhud wanapaswa wayajue hayo, wapate nguvu, wathibiti katika imaan yao, na watambue kwamba hali yao ni kama hali za wenzao wa nyuma, lakini mwisho mwema ni wao; ima wapate ushindi au walipwe malipo mema Aakhirah.   

 

Rejea Faatwir (35:43-44), Al-An’aam (6:11), Yuwsuf (12:109), Al-Kahf (18:55), Al-Hajj (22:46) na Ghaafir (40:21) (40:82), (40:85).

 

[42] Shuhadaa Rejea Aayah (3:169).

 

[43] Fadhila Na Upole Wa Nabiy Muhammad (صلى الله عليه وآله وسلم):

 

Fadhila na sifa zake imetajwa mara tele katika Qur-aan na Sunnah. Rejea At-Tawbah (9:128).

 

[44]  Shuhadaa: Waliofariki Katika Vita Vitukufu Vya Jihaad Wako Hai Peponi. Rejea An-Nisaa (4:69). 

 

Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) amehadithia: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  amesema: “Pale walipopatwa na msiba ndugu zenu wa Uhud, Allaah Alijaalia roho zao kuwa katika maumbile ya ndege wa kijani ambao wanakunywa katika mito ya Jannah. na wanakula katika matunda ya Jannah, na hurukia na hustarehe kwenye kandili ya dhahabu chini ya kivuli cha ‘Arshi ya Allaah. Kisha roho hizo zilipopatwa na utamu wa kunywa na kula katika neema za humo ndani ya Jannah, na uzuri wa makazi, na marejeo yao wakasema: Laiti wangelifahamu ndugu zetu yale Allaah Aliyotufanyia sisi ili wasipuuze jambo la Jihaad na wala wasirejee na kuogopa vita. Basi hapo Allaah Akasema: “Mimi Ninayafikisha hayo kutoka kwenu!” Ndipo Allaah (سبحانه وتعالى)  Akateremsha:

وَلَا تَحْسَبَنَّ الَّذِينَ قُتِلُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ أَمْوَاتًا ۚ بَلْ أَحْيَاءٌ عِندَ رَبِّهِمْ يُرْزَقُونَ ﴿١٦٩﴾ 

“Na wala usiwadhanie kabisa wale waliouawa katika Njia ya Allaah kuwa ni wafu, bali wahai, wako kwa Rabb wao wanaruzukiwa…” [Aal-‘Imraan (3:169) mpaka Aayah (171) - Imaam Ahmad]

 

 

[45]Aliyoyasema Nabiy ‘Ibraahiym (عليه السّلام) Alipoingizwa Katika Moto Na Makafiri:

 

Amesimulia Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما): Kauli ya mwisho ya Ibraahiym wakati alipoingizwa katika moto (na makafiri) ilikuwa ni:

حَسْبِيَ اللَّهُ ونِعْمَ الوَكِيلُ

Hasbiya-Allaahu wa Ni’mal-Wakiyl

(Allaah Ananitosheleza na Mzuri Alioje Mtegemewa) [Al-Bukhaariy]

 

Al-Wakiyl: Rejea Faharasa Ya Majina Mazuri Kabisa Ya Allaah Na Sifa Zake.

 

[46] Tahadharisho Na Adhabu Ya Kutokutoa Zakaah:

 

Amesimulia Abuu Hurayrah (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Yeyote yule ambaye Allaah Amemruzuku mali kisha asiitolee Zakaah yake, basi (Siku ya Qiyaamah) mali yake itakuwa kama nyoka dume kipara aliye na madoto mawili juu ya macho yake. Atamvingirita shingoni na kumuuma mashavu yake huku akisema: Mimi mali yako! Mimi hazina yako!” [Al-Bukhaariy]

 

[47] Mayahudi Kumfanyia Allaah (سبحانه وتعالى) Utovu Wa Adabu Mkubwa, Ufidhuli Na Dhulma Ya Kuvuka Mipaka:

 

‘Ulamaa wametaja kwamba Aayah hii iliteremkwa kuhusu kundi la Mayahudi waliotaja hayo. Wakataja kuwa katika hao, ni Fanhaasw Bin ‘Aazuwraa ambaye ni miongoni mwa wanachuoni wakuu wa ki-Yahudi waliokuwa Madiynah. Na kwamba waliposikia Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

مَّن ذَا الَّذِي يُقْرِضُ اللَّـهَ قَرْضًا

“Ni nani atakayemkopesha Allaah karadha nzuri kisha (Allaah).” [Al-Baqarah (2:245)]

 

Na:

وَأَقْرَضُوا اللَّـهَ قَرْضًا حَسَنًا

“Na wakamkopesha Allaah karadha mzuri.” [Al-Hadiyd (57:18)]  

 

Akasema kwa kiburi chake kikubwa mno kauli hiyo. [Tafsiyr As-Sa’diy]

Na Sa’iyd bin Jubayr Amesimulia kutoka kwa Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) kwamba ilipoteremka:

 

مَّن ذَا الَّذِي يُقْرِضُ اللَّـهَ قَرْضًا حَسَنًا فَيُضَاعِفَهُ لَهُ أَضْعَافًا كَثِيرَةً ۚ

“Ni nani atakayemkopesha Allaah karadha nzuri kisha (Allaah) Amzidishie mzidisho mwingi.” [Al-Baqarah (2:245)]

 

Yahudi akasema: “Ee Muhammad! Je, kwani Rabb wako Amekuwa faqiri hata anaomba karadha kutoka kwa Waje Wake?” Hapo ikateremka kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

 

لَّقَدْ سَمِعَ اللَّـهُ قَوْلَ الَّذِينَ قَالُوا إِنَّ اللَّـهَ فَقِيرٌ وَنَحْنُ أَغْنِيَاءُ ۘ سَنَكْتُبُ مَا قَالُوا وَقَتْلَهُمُ الْأَنبِيَاءَ بِغَيْرِ حَقٍّ وَنَقُولُ ذُوقُوا عَذَابَ الْحَرِيقِ ﴿١٨١﴾

“Kwa yakini Allaah Ameisikia kauli ya wale (Mayahudi) waliosema: Hakika Allaah ni fakiri na sisi ni matajiri. Tutayaandika waliyoyasema na kuua kwao Manabii pasi na haki na Tutasema: Onjeni adhabu ya kuunguza!” [Aal-‘Imraan (3:181), Tafsiyr ibn Kathiyr]

 

[48] Ni Sunnah Kusoma Aayah Za Mwisho Za Suwrah Aal-‘Imraan (190-200) Anapoamka Mtu Usiku Kuswali (Tahajjud):

 

Ibn ‘Umar (رضي الله عنهما) alimuuliza Mama wa Waumini ‘Aaishah (رضي الله عنها) : Tueleze jambo la ajabu zaidi uliloliona kwa  Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم).  Anasema: (Mama wa Waumini ‘Aaishah) akanyamaza (kukumbuka moja kati ya mambo hayo) kisha akasema: Ulipokuwa usiku mmoja kati ya nyusiku, Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)  alisema: “Ee ‘Aaishah! Niruhusu nifanye ibaada usiku huu kwa ajili ya Rabb wangu.”  Nikamwambia:  Wa-Allaahi, mimi napenda kuwa nawe karibu, na ninapenda linalokufurahisha. Akaenda kujitwaharisha, kisha akasimama na kuanza kuswali.  (Akalia), na hakuacha kuendelea kulia mpaka akailowesha nguo yake. Alikuwa amekaa, na akaendelea kulia mpaka akazitotesha ndevu zake.  Kisha akalia, na akaendelea kulia mpaka akailowesha sakafu. Halafu Bilaal akaja kumjulisha kuwadia wakati wa Swalaah. Alipomwona analia alimwambia:  Ee Rasuli wa Allaah! Kwa nini unalia nailhali wewe umeshasamehewa madhambi yako yaliyopita na yajayo?! Akamwambia: “Kwa nini nisiwe mja mwingi wa kushukuru! Hakika zimeniteremkia usiku huu Aayah hizi.  Basi ole wake atakayezisoma na asiyataamuli yaliyomo humo.” Akasoma:

 

إِنَّ فِي خَلْقِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَاخْتِلَافِ اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ لَآيَاتٍ لِّأُولِي الْأَلْبَابِ ﴿١٩٠﴾ 

“Hakika katika kuumbwa mbingu na ardhi, na mabadiliko ya mfuatano wa usiku na mchana, bila shaka ni Aayaat (Ishara, Dalili, Mazingatio) kwa wenye akili…” (mpaka mwisho wa Suwrah).  [Imesimuliwa na Ibn Hibaan katika Swahiyh yake.  Al-Albaaniy kasema: Isnaad yake ni nzuri. Kuna Riwaaya nyengine kama hiyo katika Al-Bukhaariy na Muslim]

 

[49]  Baadhi Ya Maana Ya Ribaatw (رِبَاطٌ) Na Fadhila Zake:

 

Kwanza: Kubakia, kusimama imara katika kuchunga na kulinda mipaka katika Jihaad fiy SabiliLLaah.

 

Pili:  Kubakia katika ibaada baina ya Swalaah Na Swalaah ya pili.

 

Fadhila za Ribaatw:

Amesimulia Sahl bin Sa’ad (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Ar-Ribaatw (kusimama imara katika kulinda mipaka kwenye vita vya Jihaad) ya siku moja kwa ajili ya Allaah, ni bora kuliko dunia na vilivyomo. Na sehemu ndogo katika Jannah (Peponi), kiasi cha ukubwa wa fimbo ya mmoja wenu, ni bora kuliko dunia na yaliyomo ndani yake. Na safari ya asubuhi au ya jioni anayosafiri mja katika Njia ya Allaah, ni bora kuliko dunia na vilivyomo.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

Pia: Amesimulia Salmaan (رضي الله عنه): Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Ribaatw (kusimama imara katika kulinda mipaka kwenye vita vya Jihaad) ya siku moja na usiku wake, ni bora (katika malipo) kuliko Swiyaam ya mwezi mzima na Qiyaam (kisimamo cha kuswali usiku) chake. Na mtu akifariki (akiwa katika ribaatw), amali zake zitaendelea kuandikwa, na riziki yake ataendelea kuipata, na atasalimika na fitnah (za kaburi).”  [Muslim]

 

 

Share