188-Asbaabun-Nuzuwl: Aal-'Imraan Aayah 188: لَا تَحْسَبَنَّ الَّذِينَ يَفْرَحُونَ بِمَا أَتَوا وَّيُحِبُّونَ أَن يُحْمَدُوا

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

Aal-‘Imraan   188-Usiwadhanie kabisa wale wanaofurahia kwa waliyopewa

 

لَا تَحْسَبَنَّ الَّذِينَ يَفْرَحُونَ بِمَا أَتَوا وَّيُحِبُّونَ أَن يُحْمَدُوا بِمَا لَمْ يَفْعَلُوا فَلَا تَحْسَبَنَّهُم بِمَفَازَةٍ مِّنَ الْعَذَابِ ۖ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿١٨٨﴾ 

188. Usiwadhanie kabisa wale wanaofurahia kwa waliyopewa na wanapenda wasifiwe kwa wasiyoyatenda. Usiwadhanie kabisa kuwa watasalimika na adhabu. Nao watapata adhabu iumizayo.

 

 

Sababun-Nuzuwl:

 

Aayah hii imeteremka kuwazungumzia wanafiki kama alivyohadithia Abuu Sa’iyd Al-Khudriyy (رضي الله عنه) kwamba: “Katika zama za Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم), pale alipokuwa Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم) anatoka kwenda vitani, wanafiki walimkhalifu na kubakia nyuma wasiende vitani, na wakifurahi kwa kubakia kwao nyuma kinyume na (alivyofanya) Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم). Kisha pale alipokuwa anarudi Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) walitoa nyudhuru kwake na wakiapa na wakipenda wasifiwe kwa hayo waliyoyafanya, hapo ikateremka (hii Aayah…).” [Amehadithia Abuu Sai’yd (رضي الله عنه), ameipokea  Al-Bukhaariy na Muslim]  

 

 

Pia, Marwaan alimwambia mlinzi wake, Rafiy’ aende kwa Ibn ‘Abbaas (رضي الله عنهما) kumwambia: “Ingekuwa kila mtu miongoni mwetu anafurahia kwa aliyoyafanya na kupenda kusifiwa kwa ambayo hakuyatenda, basi ataadhibiwa na sisi tutaadhibiwa.” Ibn ‘Abbaas akasema: Mna nini na Aayah hii? Hakika Aayah hii imeteremshwa kuhusu Watu wa Kitabu. kisha akasoma Aayah:

 

وَإِذْ أَخَذَ اللَّـهُ مِيثَاقَ الَّذِينَ أُوتُوا الْكِتَابَ لَتُبَيِّنُنَّهُ لِلنَّاسِ وَلَا تَكْتُمُونَهُ فَنَبَذُوهُ وَرَاءَ ظُهُورِهِمْ وَاشْتَرَوْا بِهِ ثَمَنًا قَلِيلًا ۖ فَبِئْسَ مَا يَشْتَرُونَ ﴿١٨٧﴾

Na pale Alipochukua Allaah fungamano la wale waliopewa Kitabu (Allaah Akawaambia): Bila shaka mtakibainisha kwa watu na wala hamtokificha. Lakini walikitupa nyuma ya migongo yao na wakakibadilisha kwa thamani ndogo. Basi ubaya ulioje kwa yale wanayoyanunua! [Aal-‘Imraan (3:187)]

 

 

Kisha Ibn ‘Abbaas akasoma:

 

لَا تَحْسَبَنَّ الَّذِينَ يَفْرَحُونَ بِمَا أَتَوا وَّيُحِبُّونَ أَن يُحْمَدُوا بِمَا لَمْ يَفْعَلُوا فَلَا تَحْسَبَنَّهُم بِمَفَازَةٍ مِّنَ الْعَذَابِ ۖ وَلَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ ﴿١٨٨﴾ 

Usiwadhanie kabisa wale wanaofurahia (mabaya) waliyoyafanya na wanapenda wasifiwe kwa (mazuri) wasiyoyatenda. Usiwadhanie kabisa kuwa watasalimika na adhabu. Nao watapata adhabu iumizayo. [Aal-‘Imraan (3:187)]

 

 Kisha akasema: “Waliulizwa jambo (waliokuwa na ujuzi nalo) na Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) lakini walimficha kulijua na wakamuambia kinyume cha uhalisia wa jambo hilo, kisha wakaondoka wakifurahia kuwa wamemuongopea wakataka wasifiwe kwa hayo waliyoyaficha.” [Muslim]  

 

 

 

Share