154-Asbaabun-Nuzuwl: Aal-'Imraan Aayah 154: ثُمَّ أَنزَلَ عَلَيْكُم مِّن بَعْدِ الْغَمِّ أَمَنَةً نُّعَاسًا يَغْشَىٰ طَائِفَةً مِّنكُمْ

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

Aal-‘Imraan  154-Kisha Akakuteremshieni amani baada ya dhiki; usingizi unaofunika...

 

 

ثُمَّ أَنزَلَ عَلَيْكُم مِّن بَعْدِ الْغَمِّ أَمَنَةً نُّعَاسًا يَغْشَىٰ طَائِفَةً مِّنكُمْ ۖ وَطَائِفَةٌ قَدْ أَهَمَّتْهُمْ أَنفُسُهُمْ يَظُنُّونَ بِاللَّـهِ غَيْرَ الْحَقِّ ظَنَّ الْجَاهِلِيَّةِ ۖ يَقُولُونَ هَل لَّنَا مِنَ الْأَمْرِ مِن شَيْءٍ ۗ قُلْ إِنَّ الْأَمْرَ كُلَّهُ لِلَّـهِ ۗ يُخْفُونَ فِي أَنفُسِهِم مَّا لَا يُبْدُونَ لَكَ ۖ يَقُولُونَ لَوْ كَانَ لَنَا مِنَ الْأَمْرِ شَيْءٌ مَّا قُتِلْنَا هَاهُنَا ۗ قُل لَّوْ كُنتُمْ فِي بُيُوتِكُمْ لَبَرَزَ الَّذِينَ كُتِبَ عَلَيْهِمُ الْقَتْلُ إِلَىٰ مَضَاجِعِهِمْ ۖ وَلِيَبْتَلِيَ اللَّـهُ مَا فِي صُدُورِكُمْ وَلِيُمَحِّصَ مَا فِي قُلُوبِكُمْ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُورِ ﴿١٥٤﴾

154. Kisha Akakuteremshieni amani baada ya dhiki; usingizi unaofunika kundi miongoni mwenu na kundi likawashughulisha nafsi zao wakamdhania Allaah pasi na haki dhana ya kijahili; wanasema: “Je, tuna amri yoyote sisi katika jambo hili?” Sema: “Hakika amri yote ni ya Allaah.” Wanaficha katika nafsi zao yale wasiyokubainishia. Wanasema: “Lau tungelikuwa tuna amri yoyote katika jambo basi tusingeliuliwa hapa.” Sema: “Lau mngelikuwa majumbani mwenu, bila shaka wangejitokeza wale walioandikiwa kuuawa kwenye mahali pa kuangukia wafe.” Ili Allaah Ayajaribu yale yaliyomo katika vifua vyenu na Atakase yale yaliyomo katika nyoyo zenu. Na Allaah ni Mjuzi kwa yaliyomo vifuani.

 

Sababun-Nuzuwl:

 

Aayah hii imeteremka kama alivyohadithia Abuu Twalhah (رضي الله عنه): “Niliinua kichwa changu siku ya Uhud nikawa ninatazama. Sikuona yeyote katika wao siku hiyo isipokuwa kila mtu alikuwa amesinzia, kila mmoja ameinama chini ya silaha yake ya kujilinda na kujihami katika vita. Na hiyo ndiyo Kauli ya Allaah:

 

 

ثُمَّ أَنزَلَ عَلَيْكُم مِّن بَعْدِ الْغَمِّ أَمَنَةً نُّعَاسًا يَغْشَىٰ طَائِفَةً مِّنكُمْ ۖ  

Kisha Akakuteremshieni amani baada ya dhiki; usingizi unaofunika kundi miongoni mwenu. [At-Tirmidhiy]  

 

Pia Az-Zubayr amehadithia kwamba: Nilikuwa pamoja na Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) wakati khofu ilizidi mno (katika vita vya Uhud) na Allaah Akatupa usingizi. Basi hapakuweko mtu ila alikuwa akisinzia (isipokuwa wanafiki). Wa-Allaahi! Kama kwenye ndoto nilisikia maneno ya Mu’attib bin Qushayr akisema:

 

لَوْ كَانَ لَنَا مِنَ الْأَمْرِ شَيْءٌ مَّا قُتِلْنَا هَاهُنَا ۗ

Lau tungelikuwa tuna amri yoyote katika jambo basi tusingeliuliwa hapa.

 

 Basi nikayahifadhi, kisha Allaah (تعالى)  Akateremsha:

 

ثُمَّ أَنزَلَ عَلَيْكُم مِّن بَعْدِ الْغَمِّ أَمَنَةً نُّعَاسًا يَغْشَىٰ طَائِفَةً مِّنكُمْ ۖ  

Kisha Akakuteremshieni amani baada ya dhiki; usingizi unaofunika kundi miongoni mwenu.

 

 mpaka Kauli Yake: tusingeliuliwa hapa.”

 

Kutokana na kauli ya Mu’attib bin Qushayr:

 

قُل لَّوْ كُنتُمْ فِي بُيُوتِكُمْ لَبَرَزَ الَّذِينَ كُتِبَ عَلَيْهِمُ الْقَتْلُ إِلَىٰ مَضَاجِعِهِمْ ۖ وَلِيَبْتَلِيَ اللَّـهُ مَا فِي صُدُورِكُمْ وَلِيُمَحِّصَ مَا فِي قُلُوبِكُمْ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ بِذَاتِ الصُّدُورِ ﴿١٥٤﴾

Sema: Lau mngelikuwa majumbani mwenu, bila shaka wangejitokeza wale walioandikiwa kuuawa kwenye mahali pa kuangukia wafe. Ili Allaah Ayajaribu yale yaliyomo katika vifua vyenu na Atakase yale yaliyomo katika nyoyo zenu. Na Allaah Anayajua vyema yaliyomo vifuani.

 

 [Ameipokea Ibn Raahwayh katika Al-Matwaalib Al-‘Aaliyah, (4/219)] 

 

 

 

 

Share