122-Asbaabun-Nuzuwl: Aal-'Imraan Aayah 122: إِذْ هَمَّت طَّائِفَتَانِ مِنكُمْ أَن تَفْشَلَا وَاللَّـهُ وَلِيُّهُمَا ۗ

 

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

Kauli ya Allaah (سبحانه وتعالى):

 

إِذْ هَمَّت طَّائِفَتَانِ مِنكُمْ أَن تَفْشَلَا وَاللَّـهُ وَلِيُّهُمَا ۗ وَعَلَى اللَّـهِ فَلْيَتَوَكَّلِ الْمُؤْمِنُونَ ﴿١٢٢﴾

Pale makundi mawili miongoni mwenu walipofanya wasiwasi kwamba watashindwa nailhali Allaah Ndiye Mlinzi na Msaidizi wao.  Basi kwa Allaah Pekee Waumini watawakali. [Aal-‘Imraan (3:122)]

 

 

Sababun-Nuzuwl:

Aayah hii imeteremka ikiwazungumzia Banuw Salamah na Banuw Haarithah kama alivyohadhithia Jaabir (رضي الله عنه) kwamba: Aayah hii imeteremshwa kuhusu sisi. Tulikuwa ni makabila mawili; Banuw Haarithah na Banuw Salamah. Tusingelipenda (kama isingeteremshwa). Sufyaan kasema: Tusingefurahi kama isingeteremshwa na hali Allaah Anasema:

 

وَاللَّـهُ وَلِيُّهُمَا

“Na Allaah Ndiye Mlinzi na Msaidizi wao.” [Amehadithia Jaabir (رضي الله عنه) na imepokelewa na Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

 

 

Share