169-Asbaabun-Nuzuwl: Aal-'Imraan Aayah 169: وَلَا تَحْسَبَنَّ الَّذِينَ قُتِلُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ أَمْوَاتًا ۚ بَلْ أَحْيَاءٌ عِندَ رَبِّهِمْ يُرْزَقُونَ

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

Aal-‘Imraan  169-Na wala usiwadhanie kabisa wale waliouawa katika njia ya Allaah ni wafu….

 

 

وَلَا تَحْسَبَنَّ الَّذِينَ قُتِلُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ أَمْوَاتًا ۚ بَلْ أَحْيَاءٌ عِندَ رَبِّهِمْ يُرْزَقُونَ ﴿١٦٩﴾ 

169. Na wala usiwadhanie kabisa wale waliouawa katika njia ya Allaah ni wafu, bali wahai, kwa Rabb wao wanaruzukiwa.

 

فَرِحِينَ بِمَا آتَاهُمُ اللَّـهُ مِن فَضْلِهِ وَيَسْتَبْشِرُونَ بِالَّذِينَ لَمْ يَلْحَقُوا بِهِم مِّنْ خَلْفِهِمْ أَلَّا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ ﴿١٧٠﴾ 

170. Wanafurahia kwa Aliyowapa Allaah kwa fadhila Zake na wanawashangilia ambao hawajaungana nao, walio nyuma yao, kwamba: “Hakuna khofu juu yao na wala hawatohuzunika.”

 

يَسْتَبْشِرُونَ بِنِعْمَةٍ مِّنَ اللَّـهِ وَفَضْلٍ وَأَنَّ اللَّـهَ لَا يُضِيعُ أَجْرَ الْمُؤْمِنِينَ ﴿١٧١﴾

171. Wanashangilia kwa neema za Allaah na fadhila na kwamba Allaah Hapotezi ujira wa Waumini.

 

 

Sababun-Nuzuwl:

 

Jaabir bin ‘Abdillaah (رضي الله عنه)  amehadithia kwamba: Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alikutana nami siku moja akaniambia: “Ee Jaabir! Una nini nakuona una huzuni?” Nikasema: Ee Rasuli wa Allaah! Baba yangu amekufa shahidi na ameacha nyuma madeni na watoto. Akasema: “Je, nikujulishe kuwa Allaah Hajapata kuongea na mtu yeyote isipokuwa nyuma ya pazia? Lakini Amemhuisha baba yako na Akazungumza naye moja kwa moja. (Allaah) Akamwambia: Tamani (lolote) Nikupe!  Akasema: Yaa Rabb! Nihuishe (nirudi duniani) ili niuliwe tena kwa ajili Yako! Akasema Rabb (تبارك وتعالى): Nimeshatanguliza kauli kwamba wao hawatorudi tena (maisha ya dunia). Akasema: Yaa Rabb! Basi nifikishie khabari kwa niliowaacha nyuma. Kisha Allaah Akateremsha:

 

 وَلَا تَحْسَبَنَّ الَّذِينَ قُتِلُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ أَمْوَاتًا ۚ بَلْ أَحْيَاءٌ عِندَ رَبِّهِمْ يُرْزَقُونَ ﴿١٦٩﴾ 

Na wala usiwadhanie kabisa wale waliouawa katika Njia ya Allaah kuwa ni wafu, bali wahai, wako kwa Rabb wao wanaruzukiwa.

 

فَرِحِينَ بِمَا آتَاهُمُ اللَّـهُ مِن فَضْلِهِ وَيَسْتَبْشِرُونَ بِالَّذِينَ لَمْ يَلْحَقُوا بِهِم مِّنْ خَلْفِهِمْ أَلَّا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ ﴿١٧٠﴾ 

Wanafurahia kwa Aliyowapa Allaah kwa Fadhila Zake na wanawashangilia ambao bado hawajaungana nao, walio nyuma yao, kwamba: Hakuna khofu juu yao na wala hawatohuzunika.

 

يَسْتَبْشِرُونَ بِنِعْمَةٍ مِّنَ اللَّـهِ وَفَضْلٍ وَأَنَّ اللَّـهَ لَا يُضِيعُ أَجْرَ الْمُؤْمِنِينَ ﴿١٧١﴾

Wanashangilia Neema kutoka kwa Allaah na Fadhila na kwamba Allaah Hapotezi ujira wa Waumini. (3:169-171). [At-Tirmidhiy, Ibn Maajah, Swahiyh At-Targhiyb (2276), Swahiyh At-Targhiyb (1361)]

 

 

 

 

Share