Kutub As-Sunnah كُتُبْ السُّنَّة

Kibainisho Muhimu

Maandalizi Ya Ramadhwaan Faida Mbali Mbali - 5

 

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمنِ الرَّحِيم

Kwa Munaasaba wa mwezi mtukufu wa Ramadhwaan, ALHIDAAYA imewakusanyia na kuwaandalia faida mbalimbali za Fiqh ya Ramadhwaan: Yanayohusiana na hukmu za Swiyaam kwa ujumla, Fataawaa Za 'Ulamaa, Maswali Na Majibu, pamoja na faida nyinginezo za kusoma na kusikiliza ili kuwasaidia kwa wepesi katika kutekeleza vizuri kabisa ‘ibaadah zenu katika Ramadhwaan.

 

Hali kadhaalika tumeanza kuwawekea Duruws, Mawaidha na Fataawaa za ‘Ulamaa wakubwa kwa lugha ya Kiarabu. Na in Shaa Allaah tutaendelea kuongeza kila baada ya muda.

 

Bonyeza Hapa Upate Faida Tele:

 

Share

Kipengele Maalumu

Nasiha Za Minasaba

Laylatul-Qadr- Vipi Uweze Kuupata Usiku Huu?

Laylatul-Qadr- Vipi Uweze Kuupata Usiku Huu?

Imekusanywa Na:  Alhidaaya.com

 

 

Tunaingia kumi la mwisho la Ramadhwaan, kumi ambalo ndani yake kuna Laylatul-Qadr. ‘ibaadah yoyote itakayotendwa usiku huo, ni bora kuliko ‘ibaadah ya miezi elfu.

 

Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):

بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ

إِنَّا أَنزَلْنَاهُ فِي لَيْلَةِ الْقَدْرِ ﴿١﴾

Hakika Sisi Tumeiteremsha Qur-aan katika Laylatil-Qadr (usiku wa Qadar).

وَمَا أَدْرَاكَ مَا لَيْلَةُ الْقَدْرِ ﴿٢﴾

Na nini kitakachokujulisha ni nini huo Laylatul-Qadr?

لَيْلَةُ الْقَدْرِ خَيْرٌ مِّنْ أَلْفِ شَهْرٍ ﴿٣﴾

Laylatul-Qadr ni mbora kuliko miezi elfu.

تَنَزَّلُ الْمَلَائِكَةُ وَالرُّوحُ فِيهَا بِإِذْنِ رَبِّهِم مِّن كُلِّ أَمْرٍ ﴿٤﴾

Wanateremka humo Malaika na Ar-Ruwh (Jibriyl) kwa idhini ya Rabb wao kwa kila jambo.

سَلَامٌ هِيَ حَتَّىٰ مَطْلَعِ الْفَجْرِ ﴿٥﴾

Amani mpaka kuchomoza Alfajiri.    [Al-Qadr: 1-5]

 

Hadiyth mbali mbali zimethibiti kuhusu fadhila za usiku huu mtukufu na jinsi Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alivyokuwa katika masiku kumi ya mwisho ya Ramadhwaan.

 

Hesabu ya thawabu za usiku huo ni kama ifuatavyo:

 

Bonyeza Endelea...

 

Share

Tarjama Ya Maana Ya Qur-aan (Translation Of The Meaning Of Al-Qur-aan)

Bonyeza Hapa Kwa Faida Ziada