Zakaatul-Fitwr: Anafanya Kazi; Je, Alipe Mwenyewe Zakaatul-Fitwr Au Wazazi Wake Wamlipie?

 

Anafanya Kazi; Je, Alipe Mwenyewe Zakaatul-Fitwr Au Wazazi Wake Wamlipie?

 

Alhidaaya.com

 

 

 

SWALI:

 

Naswali moja kuhusu Zakaa ya Fitr. Ikiwa naishi na wazazi wangu nyumba moja na nafanya kazi kwa maana ya kuwa (nimeajiliwa). Je mzazi anapota Zakaatul-Fitr kwa watu wa nyumbani pamoja na mimi inakubalika au na mimi pia natakiwa kuchangia au kujitolea mwenyewe.

 

Shukran.

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah Himdi Anastahiki Allaah Rabb wa walimwengu Swalaah na salamu zimshukie kipenzi chetu Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Ikiwa unapata kipato fulani inakuwa umeshawajibika kutoa Zakaatul-Fitwr kwa sababu hiyo ni fardhi iliyofaridhishwa kwa kila Muislamu hata mtumwa mwenye uwezo fulani amewajibika, seuze aliye huru? Dalili kama ilivyo katika usimulizi ufuatao:

 

عَن ْابْنِ عُمَرَ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَاقَالَ: "فَرَضَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ زَكَاةَ الْفِطْر  صَاعًا مِنْتَمْرٍ أَوْ صَاعًا مِنْ شَعِيرٍ عَلَى الْعَبْدِ وَالْحُرِّوَالذَّكَرِ وَالأنْثَى وَالصَّغِيرِ وَالْكَبِيرِ مِنْ الْمُسْلِمِينَ". البخاري

 

Kutoka kwa bin 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhuma): "Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ameifanya Zakaatul-Fitwr ni fardhi kwa mtumwa na aliye huru, mwanamume na mwanamke, mdogo na mkubwa miongoni mwa Waislamu kwa kutoa swaa' moja ya tende kavu au swaa' moja ya shayiri" [Al-Bukhaariy] 

 

*swaa' (pishi) moja = kilo mbili na nusu (mteko) viganja viwili vya mkono vya mtu wa wastani vilivyojaa mara nne.

 

 

Tafadhali  bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo na faidi zaid:

 

Fataawaa: Za Zakaatul-Fitwr

Fataawaa: Mukhtasari Wa Fataawaa Za Zakaatul-Fitwr

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

Share