Mwanafunzi Nchi Za Nje Atoe Zakaatul-Fitwr Au Wazazi Wake Wamtolee?

SWALI:
 
assalam aleykum warahmatullah wabarakat......
 mi kijana ambaye siichi na wazazi wangu kutokana na usoma malaysia, sasa swali langu ni kuwa tunaamnbiwa tutowe fitri baada ya kumaliza kufunga sasa swali langu ni kuwa inatakiwa mie nitowe hiyo fitri au wazazi wangu wakinitolea inafaa.. naomba mnifafanulie kuhusu hili jambo.
 
 
JIBU:
 
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho. 
 
 
Ikiwa wazazi wako ndio wenye kukuhudumia wewe kwa kukulipia hayo masomo na matumizi yako yote huko uliko, basi ni wajibu wao kukulipia Zakaatul-Fitwr na watakulipia huko waliko wao.
 
 
Lakini kama wewe mwenyewe unacho kipato basi inakupasa ulipe Zakaatul-Ftiwr mwenyewe huko uliko.
 
 
Lililo bora zaidi kufanya ni kwamba, ikiwa hali yako ni zaidi ya kujitosheleza huko uliko japokuwa ni wazazi wako ndio wanaokuhudumia na japokuwa wao watakutolea Zakaatul-Fitwr waliko wao, basi ukitoa Zakaatul-Fitwr huko uliko ni kheri zaidi. Hii ni kwa sababu; kwanza si pesa nyingi za kukulafisha bila shaka kiwango chake ni takriban kilo mbili na nusu ambayo haitokukalifu pesa nyingi. Pili itakuwa ni kama sadaka yako unayoitoa izidi kukuongezea mema.
 
 
Tafadhali soma Fataawa katika viungo vifuatavyo:
 
 
 
Na Allaah Anajua zaidi
 
 
Share