216-Aayah Na Mafunzo: Muumini Khasa Ni Mwenye Kuamini Majaaliwa Ya Khayr Na Shari

Aayah Na Mafunzo

Al-Baqarah

Muumini Khasa Ni Mwenye Kuamini Majaaliwa Ya Khayr Na Shari

www.alhidaaya.com

 

 

 كُتِبَ عَلَيْكُمُ الْقِتَالُ وَهُوَ كُرْهٌ لَّكُمْ ۖ وَعَسَىٰ أَن تَكْرَهُوا شَيْئًا وَهُوَ خَيْرٌ لَّكُمْ ۖ وَعَسَىٰ أَن تُحِبُّوا شَيْئًا وَهُوَ شَرٌّ لَّكُمْ ۗ وَاللَّـهُ يَعْلَمُ وَأَنتُمْ لَا تَعْلَمُونَ ﴿٢١٦﴾

216. Mmeandikiwa shariy’ah kupigana vita nako kunachukiza mno kwenu. Na asaa mkachukia jambo na hali lenyewe ni khayr kwenu. Na asaa mkapenda jambo na hali lenyewe ni la shari kwenu. Na Allaah Anajua na nyinyi hamjui.

 

Mafunzo:

 

قال رسولُ اللهِ صلى الله عليه وسلم:" عَجَبًا لأمرِ المؤمنِ إِنَّ أمْرَه كُلَّهُ لهُ خَيرٌ وليسَ ذلكَ لأحَدٍ إلا للمُؤْمنِ إِنْ أصَابتهُ سَرَّاءُ شَكَرَ فكانتْ خَيرًا لهُ وإنْ أصَابتهُ ضَرَّاءُ صَبرَ فكانتْ خَيرًا لهُ ". رواهُ مُسْلِمٌ.

Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Ajabu ya hali ya Muumini kuwa mambo yake yote ni khayr; anapofikwa na furaha hushukuru na huwa khayr kwake, na anapofikwa na matatizo husubiri na huwa ni khayr kwake, na haiwi hivyo (sifa hiyo) ila kwa Muumini)) [Muslim]

Share

128-Asbaabun-Nuzuwl: Na ikiwa mke atakhofia kutoka kwa mumewe uonevu wa ndoa...

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

 

An-Nisaa  128-Na ikiwa mke atakhofia kutoka kwa mumewe uonevu wa ndoa

 

وَإِنِ امْرَأَةٌ خَافَتْ مِن بَعْلِهَا نُشُوزًا أَوْ إِعْرَاضًا فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِمَا أَن يُصْلِحَا بَيْنَهُمَا صُلْحًا ۚ وَالصُّلْحُ خَيْرٌ ۗ وَأُحْضِرَتِ الْأَنفُسُ الشُّحَّ ۚ وَإِن تُحْسِنُوا وَتَتَّقُوا فَإِنَّ اللَّـهَ كَانَ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرًا ﴿١٢٨﴾

128. Na ikiwa mke atakhofia kutoka kwa mumewe uonevu wa ndoa au kutengwa, basi si vibaya juu yake wakisikilizana baina yao kwa sulhu Na sulhu ni bora. Na nafsi zimewekewa uchoyo. Na mkifanya ihsaan na mkawa na taqwa, basi hakika Allaah daima ni Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika kwa yale myatendayo.

 

Sababun-Nuzuwl:

 

Aayah hii imeteremshwa kuhusu bwana mmoja aliyekuwa na mke lakini hakuwa akimuonyesha mahaba wala hamkithirishii katika mahaba na wala hamuonyeshi mwenendo uliokuwa mzuri. Huyo bwana hakutaka kuendelea (kuwa katika ndoa naye), na alishazaa naye mtoto, lakini huyo mke hakupenda apewe talaka. Basi akamwambia mumewe: “Nakuruhusu uishi na mke mwengine” [Al-Bukhaariy na Muslim]. Katika riwaaya nyengine mwanamke huyo alisema: “Naachilia mbali haki zangu, lakini usinitaliki.” Hapo ikateremka Aayah hii: “Na ikiwa mke atakhofia kutoka kwa mumewe nushuwzaa (uonevu wa ndoa) au kutengwa…” (4: 120).

Share

Pages

Subscribe to Alhidaaya.com RSS