060-Asbaabun-Nuzuwl: Al Mumtahinah Aayah 04-05: قَدْ كَانَتْ لَكُمْ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ فِي إِبْرَاهِيمَ وَالَّذِينَ مَعَهُ

 أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

Sababu Za Kuteremshwa (Baadhi Ya  Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

060-Al-Mumtahinah Aayah 4-5

 

Kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa:)

 

قَدْ كَانَتْ لَكُمْ أُسْوَةٌ حَسَنَةٌ فِي إِبْرَاهِيمَ وَالَّذِينَ مَعَهُ إِذْ قَالُوا لِقَوْمِهِمْ إِنَّا بُرَءَآؤُاْ مِنكُمْ وَمِمَّا تَعْبُدُونَ مِن دُونِ اللَّـهِ كَفَرْنَا بِكُمْ وَبَدَا بَيْنَنَا وَبَيْنَكُمُ الْعَدَاوَةُ وَالْبَغْضَاءُ أَبَدًا حَتَّىٰ تُؤْمِنُوا بِاللَّـهِ وَحْدَهُ إِلَّا قَوْلَ إِبْرَاهِيمَ لِأَبِيهِ لَأَسْتَغْفِرَنَّ لَكَ وَمَا أَمْلِكُ لَكَ مِنَ اللَّـهِ مِن شَيْءٍ ۖ رَّبَّنَا عَلَيْكَ تَوَكَّلْنَا وَإِلَيْكَ أَنَبْنَا وَإِلَيْكَ الْمَصِيرُ﴿٤﴾

4. Kwa yakini mna kigezo kizuri kwa Ibraahiym na wale walio pamoja naye, walipowaambia watu wao: Hakika sisi tumejitenga nanyi na yale mnayoyaabudu badala ya Allaah, tunakukanusheni, na umedhihirika baina yetu na baina yenu uadui na bughudha abadi mpaka mumuamini Allaah Pekee. Isipokuwa kauli ya Ibraahiym kwa baba yake: Nitakuombea maghfirah, na wala sikumilikii chochote kile mbele ya Allaah. Rabb wetu! Tumetawakali Kwako, na Kwako Tunarudia kutubia, na Kwako ni mahali pa kuishia.

 

رَبَّنَا لَا تَجْعَلْنَا فِتْنَةً لِّلَّذِينَ كَفَرُوا وَاغْفِرْ لَنَا رَبَّنَا ۖ إِنَّكَ أَنتَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ﴿٥﴾

5. Rabb wetu! Usitujaalie kuwa mtihani kwa wale waliokufuru, na Tughufurie Rabb wetu; hakika Wewe ni Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote.

 

 

 وقوله: ((إِلَّا قَوْلَ إِبْرَاهِيمَ لِأَبِيهِ)) نهوا أن يتأسوا باستغفار إبراهيم لأبيه فيستغفروا للمشركين. وقوله تعالى ((رَبَّنَا لا تَجْعَلْنَا فِتْنَةً لِلَّذِينَ كَفَرُوا)) لا تعذبنا بأيديهم ولا بعذاب من عندك، فيقولون: لو كان هؤلاء على الحق ما أصابهم.

 

Na Kauli Yake Ta’aalaa:

إِلَّا قَوْلَ إِبْرَاهِيمَ  

 Isipokuwa kauli ya Ibraahiym..

  

Wamekatazwa kuiga kitendo cha Ibraahiym cha kumwombea maghfirah baba yake nao wakawaombea washirikina.

 

Na Neno Lake Ta’aalaa:

رَبَّنَا لَا تَجْعَلْنَا فِتْنَةً لِّلَّذِينَ كَفَرُوا  

5. Rabb wetu! Usitujaalie kuwa mtihani kwa wale waliokufuru,  

 

 

Usituadhibu kwa mikono yao, wala kwa adhabu itokayo Kwako wapate kusema: Lau kama hawa wako juu ya haki, basi yasingeliwapata haya.

[Hadiyth hii ni Swahiyh kwa masharti ya Al-Bukhaariy na Muslim lakini hawakuikhariji, na imekubaliwa na Adh-dhahabiy].

 

Share