02-Buluwgh Al-Maraam: Kitabu Cha Vyakula: Mlango Wa Kuchinja Udhw-hiyyah

 

بُلُوغُ الْمَرام

Buluwgh Al-Maraam

 

كِتَاب اَلْأَطْعِمَةِ

Kitabu Cha Vyakula

 

بَاب اَلْأَضَاحِيِّ

02-Mlango Wa Kuchinja Udhw-hiyyah[1]

 

 

 

 

 

1159.

عَنْ أَنَسِ بنِ مَالِكٍ ‏ رضى الله عنه ‏ {أَنَّ اَلنَّبِيَّ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏كَانَ يُضَحِّي بِكَبْشَيْنِ أَمْلَحَيْنِ، أَقْرَنَيْنِ، وَيُسَمِّي، وَيُكَبِّرُ، وَيَضَعُ رِجْلَهُ عَلَى صِفَاحِهِمَا.‏ وَفِي لَفْظٍ: ذَبَحَهُمَا بِيَدِهِ} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ‏ .‏ وَفِي لَفْظِ: {سَمِينَيْنِ}‏ وَلِأَبِي عَوَانَةَ فِي "صَحِيحِهِ" : {ثَمِينَيْنِ} .‏ بِالْمُثَلَّثَةِ بَدَلَ اَلسِّين

وَفِي لَفْظٍ لِمُسْلِمٍ، وَيَقُولُ: {بِسْمِ اَللَّهِ.‏ وَاَللَّهُ أَكْبَرُ}

وَلَهُ: مِنْ حَدِيثِ عَائِشَةَ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهَا، {أَمَرَ بِكَبْشٍ أَقْرَنَ، يَطَأُ فِي سَوَادٍ، وَيَبْرُكُ فِي سَوَادٍ، وَيَنْظُرُ فِي سَوَادٍ، لِيُضَحِّيَ بِهِ، فَقَالَ: "اِشْحَذِي اَلْمُدْيَةَ" ، ثُمَّ أَخَذَهَا، فَأَضْجَعَهُ، ثُمَّ ذَبَحَهُ، وَقَالَ: "بِسْمِ اَللَّهِ، اَللَّهُمَّ تَقَبَّلْ مِنْ مُحَمَّدٍ وَآلِ مُحَمَّدٍ، وَمِنْ أُمّةِ مُحَمَّدٍ"}

Kutoka kwa Anas bin Maalik (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema kuwa: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akichinja kondoo wawili madume wa kijivu walio na pembe. Akipiga BismiLLaah na akipiga Takbiyr, na akiweka mguu wake juu ya pambizo za shingo zao. Katika tamshi lingine: “Aliwachinja kwa mkono wake.” Katika tamshi lingine: “…walionona.” Abuu ‘Awaanah amepokea katika Swahiyh yake: “…wenye thamani kubwa.”

Vile vile katika tamshi lingine la Muslim: “Na alikuwa akisema: BismiLLaah Wa-Allaahu  Akbar.”

Pia Muslim amepokea kutoka kwa Hadiyth ya ‘Aaishah (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهَا): “Ameamrisha kondoo mwenye pembe, mwenye miguu myeusi, mwenye tumbo leusi, na kando ya macho yake ni weusi pia. Akaletewa ili amchinje, akamuambia ‘Aaishah: ‘Ee ‘Aaishah niletee kisu’ kisha akaniambia: ‘Kinoe kwa jiwe’, nikafanya hivyo. Akachukua kisu kile na akamchukua kondoo akamlaza, akamchinja akasema:

بِسْمِ اَللَّهِ، اَللَّهُمَّ تَقَبَّلْ مِنْ مُحَمَّدٍ وَآلِ مُحَمَّدٍ، وَمِنْ أُمّةِ مُحَمَّدٍ

 

“BismiLLaah, Allaahumma taqabbal min Muhammad wa aali Muhammad, wa min ummati Muhammad.” Kisha akamchinja

 

 

 

1160.

وَعَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ ‏ رضى الله عنه ‏ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏{"مَنْ كَانَ لَهُ سَعَةٌ وَلَمْ يُضَحِّ، فَلَا يَقْرَبَنَّ مُصَلَّانَا"} رَوَاهُ أَحْمَدُ، وَابْنُ مَاجَه، وَصَحَّحَهُ اَلْحَاكِمُ، لَكِنْ رَجَّحَ اَلْأَئِمَّةُ غَيْرُهُ وَقْفَهُ

Kutoka kwa Abuu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Mwenye uwezo na hakuchinja basi asikaribie katu Muswallaa[2] wetu.” [Imetolewa na Ahmad na Ibn Maajah na akaisahihisha Al-Haakim. Maimaam wengine wametilia nguvu kuwa ni Mawquwf]

 

 

 

1161.

وَعَنْ جُنْدُبِ بْنِ سُفْيَانَ رضى الله عنه ‏ قَالَ: {شَهِدْتُ اَلْأَضْحَى مَعَ رَسُولِ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏فَلَمَّا قَضَى صَلَاتَهُ بِالنَّاسِ، نَظَرَ إِلَى غَنَمٍ قَدْ ذُبِحَتْ، فَقَالَ: "مَنْ ذَبَحَ قَبْلَ اَلصَّلَاةِ فَلْيَذْبَحْ شَاةً مَكَانَهَا، وَمَنْ لَمْ يَكُنْ ذَبَحَ فَلْيَذْبَحْ عَلَى اسْمِ اَللَّهِ"} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

Kutoka kwa Jundub bin Sufyaan (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Nilishuhudia Udhw-hiyyah pamoja na Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alipomaliza kuswalisha watu alitazama mbuzi aliyekuwa amechinjwa, akasema: “Aliyechinja kabla kuswali achinje mnyama mwingine mahala pake na ambaye hajachinja basi achinje kwa Jina la Allaah.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

1162.

وَعَنِ اَلْبَرَاءِ بنِ عَازِبٍ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: قَامَ فِينَا رَسُولُ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏فَقَالَ: {"أَرْبَعٌ لَا تَجُوزُ فِي اَلضَّحَايَا: اَلْعَوْرَاءُ اَلْبَيِّنُ عَوَرُهَا، وَالْمَرِيضَةُ اَلْبَيِّنُ مَرَضُهَا، وَالْعَرْجَاءُ اَلْبَيِّنُ ظَلْعُهَا وَالْكَسِيرَةُ اَلَّتِي لَا تُنْقِي"} رَوَاهُ اَلْخَمْسَةُ ‏.‏ وَصَحَّحَهُ اَلتِّرْمِذِيُّ، وَابْنُ حِبَّانَ

Kutoka kwa Al-Baraa bin ‘Aazib (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alisimama akatuhutubia: “Wanyama aina nne[3] hawafai katika Udhw-hiyyah: mwenye chongo, inayoonekana wazi chongo yake, mgonjwa anayeonekana dhahiri ugonjwa wake, kiwete anayeonekana waz ulemavu wake na mkongwe ambaye hana uboho.” [Imetolewa na Al-Khamsah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah, Ahmad) na akaisahihisha At-Tirmidhiy na Ibn Hibbaan]

 

 

 

1163.

وَعَنْ جَابِرٍ ‏ رضى الله عنه ‏ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏{"لَا تَذْبَحُوا إِلَّا مُسِنَّةً، إِلَّا أَنْ يَعْسُرَ عَلَيْكُمْ فَتَذْبَحُوا جَذَعَةً مِنَ اَلضَّأْنِ"} رَوَاهُ مُسْلِمٌ

Kutoka kwa Jaabir (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) amesema: “Msichinje (Udhw-hiyyah) isipokuwa musinnah,[4] isipokuwa ikiwa uzito kwenu, hapo mtachinja koo la kondoo (mwenye umri wa miezi sita hadi kumi).” [Imetolewa na Muslim]

 

 

 

1164.

وَعَنْ عَلِيٍّ ‏ رضى الله عنه ‏ قَالَ: {أَمَرَنَا رَسُولُ اَللَّهِ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏أَنْ نَسْتَشْرِفَ اَلْعَيْنَ وَالْأُذُنَ، وَلَا نُضَحِّيَ بِعَوْرَاءَ، وَلَا مُقَابَلَةٍ، وَلَا مُدَابَرَةٍ، وَلَا خَرْمَاءَ، وَلَا ثَرْمَاءَ"} أَخْرَجَهُ أَحْمَدُ، وَالْأَرْبَعَةُ.‏ وَصَحَّحَهُ اَلتِّرْمِذِيُّ، وَابْنُ حِبَّانَ، وَالْحَاكِمُ

Kutoka kwa ‘Aliy (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alituamuru kuchunguza macho na masikio, wala tusidhahi mnyama chongo, wala aliyekatwa ncha ya sikio, wala aliyekatwa masikio kwa upana wala asiye na meno ya mbele.”[5] [Imetolewa na Ahmad na Al-Arba’ah (At-Tirmidhiy, An-Nasaaiy, Abuu Daawuwd, Ibn Maajah) na akaisahihisha At-Tirmidhiy, Ibn Hibbaan na Al-Haakim]

 

 

 

1165.

وَعَنْ عَلِيِّ بْنِ أَبِي طَالِبٍ ‏ رضى الله عنه ‏ قَالَ: {أَمَرَنِي اَلنَّبِيُّ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏أَنَّ أَقْوَمَ عَلَى بُدْنِهِ، وَأَنْ أُقَسِّمَ لُحُومَهَا وَجُلُودَهَا وَجِلَالَهَا عَلَى اَلْمَسَاكِينِ، وَلَا أُعْطِيَ فِي جِزَارَتِهَا مِنْهَا شَيْئاً} مُتَّفَقٌ عَلَيْهِ

Kutoka kwa ‘Aliy bin Abiy Twaalib (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) amesema: “Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) aliniamuru nimsimamie ngamia wake (wa Udhw-hiyyah) na nigawe nyama yao, ngozi yake na masaruji yake kwa masikini.[6] Na nisimpe chochote mchinjaji kutokana na ngamia hao.” [Al-Bukhaariy, Muslim]

 

 

 

1166.

وَعَنْ جَابِرِ بنِ عَبْدِ اَللَّهِ رَضِيَ اَللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: {نَحَرْنَا مَعَ اَلنَّبِيِّ ‏ صلى الله عليه وسلم ‏عَامَ اَلْحُدَيْبِيَةِ: اَلْبَدَنَةَ عَنْ سَبْعَةٍ، وَالْبَقَرَةَ عَنْ سَبْعَةٍ} رَوَاهُ مُسْلِمٌ

Kutoka kwa Jaabir bin ‘Abdillaah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا) amesema: “Tulichinja pamoja na Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) mwaka wa Vita Vya Hudaybiyah watu saba kwa kuchinja ngamia mmoja na watu saba wakishirikiana kwa kuchinja ng’ombe mmoja.”[7] [Imetolewa na Muslim]

 

 

[1] Kuchinja ni aina mbili: Ya kwanza ni Hady na ya pili ni Udhw-hiyyah. Hady ni ile inayotolewa na Hujaji Minaa. Ama Udhw-hiyyah ni ile inayotolewa na Waislamu maeneo mengine ulimwenguni wakati wa ‘Iydul Adhw-haa au wakati wa Tashriyq. Kulingana na Wanazuoni wengi, kutoa Udhw-hiyyah ni Sunnah, kwa Wanazuoni wengine ni waajib. ‘Ibaadah hii inaitwa udhw-hiyyah kwa sababu inafanyika wakati wa dhwuha.

[2] Baadhi ya Wanazuoni wanahitimisha katika Hadiyth hii kuwa swala la kuchinja udhw-hiyyah ni la waajib. Hata hivyo Wanazuoni wengi wanaona kuwa ni Sunnah Muakkada. (Sunnah iliyosisitizwa).

[3] Mgonjwa, kiguru, chongo na dhaifu hawaruhusiwi kuchinjwa kwa ajili ya Udhw-hiyyah. Wanazuoni wanaona kuwa hukumu hii inahusu pia magonjwa mengine mwilini.

[4] Katika lugha ya Kiarabu Musinnah ni mnyama ambaye meno yake ya mwanzo yameshaondoka na kuanguka na kubadilishwa kwa meno mengine ya kawaida. Kila mnyama ana muda wake wa kutoka kwa meno. Mbuzi, kondoo na kondoo dume aliyehasiwa wanapokuwa mwaka wa kwanza na kuingia mwaka wa pili wanakuwa musinnah. Ng’ombe na jamusi wanakuwa katika hali hii wanapoingia mwaka wa tatu wa umri wao. Ngamia anakuwa anakuwa katika hali hiyo anapoingia mwaka wa sita wa umri wake.

[5] Mnyama ambaye amekatwa sikio au hata kukaruzwa, au aliyekatwa pembe haruhusiwi kuchinjwa. Hukumu inayohusu sikio na pembe ni ikiwa nusu ya viungo hivi kama vimekatwa basi hairuhusiwi kuchinjwa. Lakini ikiwa zaidi ya nusu ya viungo hivi vikiwa katika hali nzuri basi wanyama hawa wanafaa kuchinjwa. Ikiwa mnyama atakuwa amezaliwa bila ya pembe haizingatiwi kama ni ila, hata hivyo ikiwa pembe yenyewe imekatika baada ya kuzaliwa itakuwa ni ila.

 

[6] Ngozi, sufi na nyama ya mnyama inabidi itolewe kama Swadaqah. Mtu anayetoa Udhw-hiyyah anaruhusiwa kula nyama ile na anaweza kutumia ngozi yake. Kumpa mchinjaji nyama kama ujira wake ni jambo lenye kukatazwa. Watu wengine hawawalipi wachinjaji ujira wao, ambalo ni jambo lisilopendeza. Katika hali ambayo mchinjaji hachukui ujira wake kwa mapenzi yake basi inaruhusiwa.

[7] Udhw-hiyyah wa kondoo mmoja inatosheleza hata kwa watu ishirini wa nyumba moja. Ama udhw-hiyyah wa ng’ombe, jamusi na ngamia mmoja wanashirikiana watu saba kwa maana hiyo nyumba saba zitafaidika na udhw-hiyyah hiyo. Ikiwa udhw-hiyyah hiyo ni ya Sunnah au ni ya waajib, yote ni sawa hakuna tofauti. Siyo lazima ikawa kwa watu saba hata mtu mmoja anaweza kufanya hivyo.

Share