Wali Wa Kisomali Wa Kuku

VIPIMO
WALI:
Mchele 3 vikombe
Vitunguu (viliokatwa vidogo vidogo) 2
Mafuta 3 vijiko vya supu
Thomu na tangawizi iliyosagwa 1 kijiko cha chai
Bizari ya pilau 1 kijiko cha supu
Mdalasini 1 kijiti
Hiliki 3 chembe
Pilipili manga nzima chembe chache
Siagi Vijiko 2 vya supu
Chumvi kiasi
KUKU
Kuku kidari (Breast) kata vipande vipande 2 LB
Mafuta 3 vijiko vya supu
Thomu na tangawizi iliyosagwa 1 kijiko cha supu
Pilipili mbichi iliyosagwa 1 kijiko cha supu
Kotmiri iliyokatwa ndogo ndogo kiasi
Bizari ya pilau (cummin au jiyrah) 1 kijiko cha chai
Pilipili kubwa tamu la kijani 1
Pilipili kubwa tamu nyekundu 1
(zikate vipande vipande)
Karoti iliyokunwa 1 – 2
Chumvi Kiasi
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
Wali:
1. Roweka mchele kwa muda fulani kutegemea mchele
2. Katika sufuria tia mafuta na kaanga vitunguu hadi vibadilike rangi kidogo.
3. Tia thomu iliyosagwa, mdalasini, bizari ya pilau, hiliki, pilipili manga na chumvi, kaanga kidogo.
4. Tia mchele kaanga kidogo, kisha tia maji ya moto kiasi kutegemea na aina ya mchele kama kawaida ya kupika wali
5. Tia sigai, funika upikike wali hadi uwive.
Kuku:
1. Mchanganye kuku pamoja na thomu/tangawizi iliyosagwa, chumvi, pilipili mbichi.
2. Katika karai tia mafuta yapate moto vizuri.
3. Mtie kuku, bizari ya pilau (jiyrah) na ukaange, karibu na kuiva tia vitunguu.
4. Tia mapilipili makubwa, kotmiri, na kaanga kwa dakika moja tu uzime moto na epua weka kando.
Kupakua:
1. Pakua wali katika sahani.
2. Pambia karoti iliyokunwa na ukipenda zabibu na wali uko tayari kuliwa
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha



ahsante kwa kutupatia
ahsante kwa kutupatia recipes nzuri .