04-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Unyeyekevu Wake: Akiwasalimia Watoto Na Kuwapapasa Vichwa Vyao

 

Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

04-Unyenyekevu Wake Akiwasalimia Watoto Na Kuwapapasa Vichwa Vyao

 

www.alhidaaya.com

 

 

Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa mwenye mapenzi na huruma mpaka kwa watoto wake na wasio wake:

 

 

عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ، قَالَ مَا رَأَيْتُ أَحَدًا كَانَ أَرْحَمَ بِالْعِيَالِ مِنْ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم  قَالَ  كَانَ إِبْرَاهِيمُ مُسْتَرْضِعًا لَهُ فِي عَوَالِي الْمَدِينَةِ فَكَانَ يَنْطَلِقُ وَنَحْنُ مَعَهُ فَيَدْخُلُ الْبَيْتَ وَإِنَّهُ لَيُدَّخَنُ وَكَانَ ظِئْرُهُ قَيْنًا فَيَأْخُذُهُ فَيُقَبِّلُهُ ثُمَّ يَرْجِعُ ‏.‏    

 

 

Kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: “Sijapatapo kuona mtu mwenye huruma zaidi na familia yake kama Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Akasema:  Ibrahiym (mwanawe Nabiy Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam( alikuwa akinyonyeshwa na familia moja ya Madiynah. Alipokuwa  anapowatembelea nasi tulikuwa pamoja naye, huingia katika nyumba iliyojaa moshi kwa vile baba yake (Ibraahiym) wa kambo alikuwa ni mhunzi wa chuma. Basi alimbeba Ibraahiym akambusu kisha akimrudisha.  [Muslim]

 

 

Pia,

 

عَنْ أَنَسِ بْنِ مَالِكٍ رضى الله عنه أَنَّهُ مَرَّ عَلَى صِبْيَانٍ فَسَلَّمَ عَلَيْهِمْ وَقَالَ كَانَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم يَفْعَلُهُ‏

 

Kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba aliwapitia Watoto akawasalimia kisha akasema: Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akifanya hivyo: [Al-Bukhaari]

  

Pia,

 

عن أنس بن مالك رضي الله عنه عن النبي صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ : " كَانَ يَزُورُ الأَنْصَارَ وَيُسَلِّمُ عَلَى صِبْيَانِهِمْ ، وَيَمْسَحُ بِرُءُوسِهِمْ "

 

Kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akiwatembelea kina Answaariy na akiwasalimia watoto wao na akiwapapasa vichwa vyao. [Ibn Maajah, ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh Ibn Maajah (459), As-Silsilah Asw-Swahiyhah (5/149)]

 

Share