06-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Unyenyekevu Wake: Hakujiona Yeye Ni Bora Kuliko Maswahaba Wake

 

Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

06-Unyenyekevu Wake: Hakujiona Yeye Ni Bora Kuliko Maswahaba Wake

 

www.alhidaaya.com

 

 

عن أنس بن مالك رضي الله عنه أنَّ رجلًا قال: يا محمدُ: أيا سيَّدَنا وابنَ سيِّدِنا! وخيرَنا وابنَ خيرِنا! فقال رسولُ اللهِ صلَّى اللهُ عليهِ وسلَّمَ: ((يا أيها الناسُ عليكم بتقواكم، ولا يستهوينَّكم الشيطانُ، أنا محمدُ بنُ عبدِ اللهِ، أنا عبدُ اللهِ ورسولِه، ما أحبُّ أن ترفعوني فوقَ منزلَتي التي أنزلَنيها اللهُ))

Kutoka kwa Anas bin Maalik (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba mtu mmoja aliita: “Ee Muhammad! Ee Bwana wetu, mwana wa Bwana wetu! Mbora wetu, mwana wa mbora wetu!”  Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Enyi watu! Shikameni na taqwa yenu! Msimwache shaytwaan akuchezeeni! Mimi ni Muhammad bin ‘Abdillaah, mja wa Allaah na Rasuli Wake. Sipendi mnipandishe zaidi ya daraja ambayo Ameniteremshia Allaah)) [Ahmad, An-Nasaaiy na ameisahihisha Al-Albaaniy katika As-Silsilah Asw-Swahiyhah (4/101)]

 

Na pia:

 

عنْ أَبِي مَسْعُودٍ، قَالَ أَتَى النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم ـ رَجُلٌ فَكَلَّمَهُ فَجَعَلَ تُرْعَدُ فَرَائِصُهُ فَقَالَ لَهُ: ((هَوِّنْ عَلَيْكَ فَإِنِّي لَسْتُ بِمَلِكٍ إِنَّمَا أَنَا ابْنُ امْرَأَةٍ تَأْكُلُ الْقَدِيدَ))   

Kutoka kwa Abuu Mas‘uwd amesema: Alikuja mtu kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akamsemesha basi akawa anatetemeka kwa sababu ya kumwogopa. Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Jitulize, kwani mimi si mfalme, hakika mimi ni mwana ambaye mama yake alikula nyama kavu)) [Ibn Maajah na ameisahihisha Al-Albaaniy katika Swahiyh Ibn Maajah (2693)]

 

Share