18-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Unyeyekevu Wake: Hakuwa Mwenye Kiburi Bali Amekataza Kutakabari

 

Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

18-Unyeyekevu Wake Hakuwa Mwenye Kiburi Bali Amekataza Kutakabari

www.alhidaaya.com

 

 

 عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ مَسْعُودٍ  (رضي الله عنه) عَنْ النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ: ((لاَ يَدْخُلُ الْجَنَّةَ مَنْ كَانَ فِي قَلْبِهِ مِثْقَالُ ذَرَّةٍ مِنْ كِبْر))  قَالَ رَجُلٌ: إِنَّ الرَّجُلَ يُحِبُّ أَنْ يَكُونَ ثَوْبُهُ حَسَنًا وَنَعْلُهُ حَسَنَةً.  قَالَ:  ((إِنَّ اللَّهَ جَمِيلٌ يُحِبُّ الْجَمَالَ،  الْكِبْرُ بَطَرُ الْحَقِّ وَغَمْطُ النَّاسِ)) مسلم

 

Imepokelewa kutoka kwa ‘Abdullaah bin Mas’uwd (رضي الله عنه) kwamba Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: ((Hatoingia Jannah ambaye moyoni mwake mna kiburi uzito wa chembe (au sisimizi)). Mtu mmoja akauliza: “Mtu hupenda nguo yake iwe nzuri na viatu vyake viwe vizuri [itakuwaje?]” Akasema: ((Hakika Allaah ni Mzuri Anapenda Uzuri. Kiburi ni kukataa haki na kudharau watu)).  [Muslim]

 

 

Share