21-Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم):Unyenyekevu Wake: Akila Na Kuketi Kama Wanavyokula Na Kuketi Maswahaba

 

Sifa Na Akhlaaq Za Nabiy  (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

21-Unyenyekevu Wake  Akila Na Kuketi Kama Wanavyokula Na Kuketi Maswahaba

 

www.alhidaaya.com

 

 

عَنْ يَحْيَى بْنِ أَبِي كَثِيرٍ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ قَالَ آكُلُ كَمَا يَأْكُلُ الْعَبْدُ وَأَجْلِسُ كَمَا يَجْلِسُ الْعَبْدُ فَإِنَّمَا أَنَا عَبْدٌ

Kutoka kwa Yahya bin Abi Kathiyr kwamba Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) amesema: “Mimi nakula kama anavyokula mja na nakaa kitako kama anavyokaa mja, kwani hakika mim ni mja.”  [Al-Bayhaqiy na ameisahihisha Al-Albaaniy As-Silsilah Asw-Swahiyhah (544)]

 

Katika Riwaayah nyengine:

 

حَدَّثَنَا جَرِيرُ بْنُ حَازِمٍ، قَالَ: سَمِعْتُ الْحَسَنَ، يَقُولُ: إِنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ كَانَ يُؤْتَى بِطَعَامٍ، فَيَأْمُرُ بِهِ فَيُوضَعُ عَلَى الْأَرْضِ، ثُمَّ يَقُولُ: "إِنِّي إِنَّمَا أَنَا عَبْدٌ، آكُلُ كَمَا يَأْكُلُ الْعَبْدُ" ، وَأَحْسَبُهُ قَالَ: وَأَجْلِسُ كَمَا يَجْلِسُ الْعَبْدُز" رواه البيهقي

Jariyr ibn Haazim amehadithia kwamba: Nilimsikia Al-Hasan akisema:  Hakika Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) alikuwa analetewa chakula huamrisha kiwekwe huwekwa chini kisha husema: “Hakika mimi ni mja, nakula kama mnavyokula.” Na nadhani pia amesema: “Na nakaa kitako kama mnavyokaa kitako.”

[Al-Bayhaqiy, As-Silsilah Asw-Swahiyhah (544)]

Share