Skip navigation.
Home kabah

Kuku Wa Karai (Pakistani)


 

 

 
Vipimo 

                        

Kuku aliyekatwa vipande vipande                    5 LB

Mafuta                                                           1 Kikombe cha chai

Nyanya zilizokatwa ndogo ndogo                    5 kubwa

Nyanya ya kopo                                             2 kiijiko vya supu

Thomu na Tangawizi                                       2 vijiko vya supu

Pilipili mbichi (zipasue katikati)                         3 au 5

Bizari ya pilau ya unga (Jeera)                        2 vijiko vya chai

Gilgilani ya unga (Dania)                                 1 kijiko cha chai

Paprika                                                          1 Kijiko cha supu

Bizari ya manjano ya unga                             2 vijiko vya chai

Chumvi                                                          kiasi

 Kotmiri iliyokatwa ndogondogo                     1 kikombe kimoja

Pilipili mboga (kijani)                                       1

Ndimu                                                            2 vijiko vya supu.

 

Namna Ya Kutayarisha Na Kupika

 

1.  Tia mafuta katika karai yashike moto vizuri.

2.  Tia Thomu na tangawizi kaanga kidogo tu.

3.  Tia nyanya, pilipili mbichi, nyanya ya kopo na bizari zote.

4.   Mtie kuku na mkaange katika masala hayo.

5.  Funika karai na wacha moto wa kiasi, kuku atoe maji yake na  apikike.

6.  Karibu na kuwiva kuku tia pilipili mboga iliyokatwa vipande vipande, kotmiri na ndimu.

7.  Funua karai na endelea kukaanga mpaka awe anakaribia kukauka,  muepue na tayari kuliwa.

 

BISMILLAH RAHMAN

BISMILLAH RAHMAN RAHIM:

SHUKRAN KWA WOTE MLIO/MNAOSHIRIKI KATIKA KUTUKUMBUSHA NA KUTUONGOGA KTK MWELEKEO MWEMA.

INSHALLWA MOLA AKUJAALIENI KILA LA KHERI NA AKUWEZESHENI NANYI KUZIKUMBUSHA NAFSI ZENU KTK MUONGOZO MWEMA.

ZAIDI NI KWAMBA MNATUSAIDIA WENGI WETU KUWEZA KUZIPATIA LISHE BORA FAMILIA ZETU. NA HASA KUIMARISHA NDOA ZETU.

KWANI MWANAMKE JIKO ATI.

ALHAMDULILAH RABIL ALAMIN