Mbaazi

Vipimo
Mbaazi za kopo (pigeon peas) 40 fl oz (vikopo viwili) (Vikombe vitatu)
Ikiwa mbaazi kavu 3 Vikombe
Tui la nazi zito 1 Kikombe
Kitunguu 1
Chumvi kiasi
Pilipili mbichi 2
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
1. Ikiwa ni mbaazi kavu, roweka katika maji kwa muda wa masaa kisha chemsha hadi ziwive.
2. Ikiwa ni mbaazi za kopo, mwaga maji yake ya kopo umimine katika sufuria.
3. Kata vitunguu na utie katika mbaazi.
4. Tia tui, chumvi, pililipili mbichi upike hadi kwa muda mdogo tu hadi tui lipunguke kidogo, zitakuwa tayari kuliwa.
Maandazi - Tazama Vipimo Vyake kwenye 'Mikate '
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


