41-Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi: الرَّزَّاقُ

Sharh Asmaa Allaah Al-Husnaa Wa Swifaatihi

 

(Maelezo Ya Majina Mazuri Ya Allaah Na Swiffah Zake)

 

Alhidaaya.com

 

الرَّزَّاقُ

 

 

 

 

الرَّزَّاقُ

Ar-Razzaaq

Mwingi Wa Kuwaruzuku Viumbe Vyote

 

 

 

Allaah (سبحانه وتعالى) ni Pekee Anayewaruzuku waja Wake wote, hakuna kiumbe duniani isipokuwa Allaah (سبحانه وتعالى) hukipa rizki. Rizki Yake kwa waja Wake ni ya namna mbili:

 

 

i-Rizki ya ujumla ambayo hukunjuka kwa waja wema na watenda dhambi, wa kwanza mpaka wa mwisho. Hii ni rizki inayohitajika mwilini.

 

 

ii-Rizki mahususi. Hii hutolewa kwenye nyoyo, zinastawishwa kwa ‘ilmu na iymaan. Pia rizki ya halaal iliyoteuliwa kwa manufaa ya Dini, na hii ni mahsusi kwa Waumini na hugawanywa kulingana na daraja zao mbalimbali na kile inachokiamuru Hikmah na Rahmah Yake.

 

 

Anasema Allaah (سبحانه وتعالى):

 

قُلْ تَعَالَوْا أَتْلُ مَا حَرَّمَ رَبُّكُمْ عَلَيْكُمْ ۖ أَلَّا تُشْرِكُوا بِهِ شَيْئًا ۖ وَبِالْوَالِدَيْنِ إِحْسَانًا ۖ وَلَا تَقْتُلُوا أَوْلَادَكُم مِّنْ إِمْلَاقٍ ۖ نَّحْنُ نَرْزُقُكُمْ وَإِيَّاهُمْ ۖ وَلَا تَقْرَبُوا الْفَوَاحِشَ مَا ظَهَرَ مِنْهَا وَمَا بَطَنَ ۖ وَلَا تَقْتُلُوا النَّفْسَ الَّتِي حَرَّمَ اللَّـهُ إِلَّا بِالْحَقِّ ۚ ذَٰلِكُمْ وَصَّاكُم بِهِ لَعَلَّكُمْ تَعْقِلُونَ ﴿١٥١﴾

Sema: Njooni nikusomeeni yale Aliyoyaharamisha Rabb wenu kwenu. Kwamba msimshirikishe na chochote, na muwafanyie ihsaan wazazi wawili, na wala msiwaue watoto wenu kutokana na umasikini. Sisi Tunakuruzukuni pamoja nao. Na wala msikaribie machafu yaliyo dhahiri na yaliyofichika. Na wala msiue nafsi ambayo Ameiharamisha Allaah (kuiua) isipokuwa kwa haki (ya shariy’ah). Hivyo ndivyo Alivyokuusieni kwayo mpate kutia akilini. [Al-An’aam (6): 151]

 

 

Na Anasema pia Allaah (سبحانه وتعالى):

وَمَا خَلَقْتُ الْجِنَّ وَالْإِنسَ إِلَّا لِيَعْبُدُونِ ﴿٥٦﴾

Na Sikuumba majini na wana Aadam isipokuwa waniabudu.

 

مَا أُرِيدُ مِنْهُم مِّن رِّزْقٍ وَمَا أُرِيدُ أَن يُطْعِمُونِ ﴿٥٧﴾

Sitaki kutoka kwao riziki yoyote, na wala Sitaki wanilishe.

 

إِنَّ اللَّـهَ هُوَ الرَّزَّاقُ ذُو الْقُوَّةِ الْمَتِينُ ﴿٥٨﴾

Hakika Allaah Ndiye Mwingi wa kuruzuku, Mwenye nguvu Madhubuti.

[Adh-Dhaariyyat (51): 56-58]

 

 

 

 

Share