044-Asbaabun-Nuzuwl: Ad-Dukhaan Aayah 10-15: ‏فَارْتَقِبْ يَوْمَ تَأْتِي السَّمَاءُ بِدُخَانٍ مُبِينٍ

أسْبابُ النُّزُول

Asbaabun-Nuzuwl

(Sababu Za Kuteremshwa Suwrah Na Aayaat Za Qur-aan)

 

Imekusanywa na: Alhidaaya.com

 

044-Asbaabun-Nuzuwl Ad-Dukhaan Aayah 10 - 15

 

 

 

Kauli Zake Allaah (سبحانه وتعالى):

 

فَارْتَقِبْ يَوْمَ تَأْتِي السَّمَاءُ بِدُخَانٍ مُّبِينٍ﴿١٠﴾ يَغْشَى النَّاسَ ۖ هَـٰذَا عَذَابٌ أَلِيمٌ﴿١١﴾ رَّبَّنَا اكْشِفْ عَنَّا الْعَذَابَ إِنَّا مُؤْمِنُونَ﴿١٢﴾ أَنَّىٰ لَهُمُ الذِّكْرَىٰ وَقَدْ جَاءَهُمْ رَسُولٌ مُّبِينٌ﴿١٣﴾ ثُمَّ تَوَلَّوْا عَنْهُ وَقَالُوا مُعَلَّمٌ مَّجْنُونٌ﴿١٤﴾ إِنَّا كَاشِفُو الْعَذَابِ قَلِيلًا ۚ إِنَّكُمْ عَائِدُونَ﴿١٥﴾

10. Basi ngojea uangaze siku mbingu zitakapoleta moshi bayana. 11. Utawafunika watu. Hii ni adhabu iumizayo. 12. (Watasema): Rabb wetu! Tuondoshee adhabu, hakika sisi wenye kuamini. 13. Kutoka wapi watapata ukumbusho na hali amekwishawajiaRasuli mwenye kubainisha. 14. Kisha wakamkengeuka na wakasema: Amefundishwa na majnuni. 15. Hakika Sisi Tutaiondosha adhabu kidogo, lakini nyinyi hakika mtarudia vile vile. [Ad-Dukhaan (42: 10 – 15]

 

Sababun-Nuzuwl: 

 

حَدَّثَنَا سُلَيْمَانُ بْنُ حَرْبٍ، حَدَّثَنَا جَرِيرُ بْنُ حَازِمٍ، عَنِ الأَعْمَشِ، عَنْ أَبِي الضُّحَى، عَنْ مَسْرُوقٍ، قَالَ دَخَلْتُ عَلَى عَبْدِ اللَّهِ ثُمَّ قَالَ إِنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم لَمَّا دَعَا قُرَيْشًا كَذَّبُوهُ وَاسْتَعْصَوْا عَلَيْهِ فَقَالَ ‏"‏ اللَّهُمَّ أَعِنِّي عَلَيْهِمْ بِسَبْعٍ كَسَبْعِ يُوسُفَ ‏"‏‏.‏ فَأَصَابَتْهُمْ سَنَةٌ حَصَّتْ ـ يَعْنِي ـ كُلَّ شَىْءٍ حَتَّى كَانُوا يَأْكُلُونَ الْمَيْتَةَ فَكَانَ يَقُومُ أَحَدُهُمْ فَكَانَ يَرَى بَيْنَهُ وَبَيْنَ السَّمَاءِ مِثْلَ الدُّخَانِ مِنَ الْجَهْدِ وَالْجُوعِ ثُمَّ قَرَأَ ‏((‏فَارْتَقِبْ يَوْمَ تَأْتِي السَّمَاءُ بِدُخَانٍ مُبِينٍ * يَغْشَى النَّاسَ هَذَا عَذَابٌ أَلِيمٌ‏)) ‏ حَتَّى بَلَغَ ‏((‏إِنَّا كَاشِفُو الْعَذَابِ قَلِيلاً إِنَّكُمْ عَائِدُونَ‏))‏ قَالَ عَبْدُ اللَّهِ أَفَيُكْشَفُ عَنْهُمُ الْعَذَابُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ قَالَ وَالْبَطْشَةُ الْكُبْرَى يَوْمَ بَدْرٍ‏.‏

 

Ametuhadithia Sulaymaan ibn Harb, ametuhadithia Jariyr bin Haazim, toka kwa Al-A‘mash, toka kwa Abu Adh-Dheuhaa, toka kwa Masruwq, amesema: Niliingia kwa ‘Abdullaah [bin Mas‘uwd] kisha akasema: Hakika Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) alipowalingania Maquraysh [Uislaam] walimkadhibisha na wakampinga na kumfanyia inadi, naye akasema [kuwaapiza]: Ee Allaah! Nisaidie dhidi yao kwa kuwapiga miaka saba ya njaa na ukame kama miaka saba ya njaa na ukame ya [enzi ya Nabiy] Yuwsuf. Ukawapiga mwaka mmoja wa njaa na ukame ulioteketeza kila kitu mpaka wakaanza kula mizoga. Na mmoja wao anaposimama, alikuwa anaona kitu mithili ya moshi kati yake na kati ya mbingu kutokana na uchovu mkubwa na njaa kali. Kisha akasoma:

 

فَارْتَقِبْ يَوْمَ تَأْتِي السَّمَاءُ بِدُخَانٍ مُّبِينٍ﴿١٠﴾ يَغْشَى النَّاسَ ۖ هَـٰذَا عَذَابٌ أَلِيمٌ﴿١١﴾

Basi ngojea uangaze siku mbingu zitakapoleta moshi bayana • Utawafunika watu. Hii ni adhabu iumizayo….mpaka akafikia:

 

إِنَّا كَاشِفُو الْعَذَابِ قَلِيلًا ۚ إِنَّكُمْ عَائِدُونَ﴿١٥﴾

Hakika Sisi Tutaiondosha adhabu kidogo, lakini nyinyi hakika mtarudia vile vile.

‘Abdullaah akasema: Je, hivi wataondoshewa adhabu Siku ya Qiyaamah?  Akasema [tena]:

الْبَطْشَةَ الْكُبْرَىٰ

Mashambulizi makubwa ni Siku ya Badr. [Al-Bukhaariy Kitaab At-Tafsiyr]

             

 

Faida:

 

‘Abdullaah aliposema: Je, hivi wataondoshewa adhabu Siku ya Qiyaamah? [Swali kanushi hili. Anakusudia kwamba moshi uliotajwa katika Aayah hatuwezi kusema utakuja Siku ya Qiyaamah, kwa kuwa Allaah Amesema:

 

إِنَّا كَاشِفُو الْعَذَابِ قَلِيلًا ۚ إِنَّكُمْ عَائِدُونَ﴿١٥﴾

 

 ((Hakika Sisi Tutaiondosha adhabu kidogo)), na adhabu ya Aakhirah haiondoshwi. Moshi kusudiwa hapa ni ule anaouona Mqurayshi kutokana na njaa kali].                           

 

 

Na pia,

 

حَدَّثَنَا أَبُو بَكْرِ بْنُ أَبِي شَيْبَةَ، حَدَّثَنَا أَبُو مُعَاوِيَةَ، وَوَكِيعٌ، ح وَحَدَّثَنِي أَبُو سَعِيدٍ، الأَشَجُّ أَخْبَرَنَا وَكِيعٌ، ح وَحَدَّثَنَا عُثْمَانُ بْنُ أَبِي شَيْبَةَ، حَدَّثَنَا جَرِيرٌ، كُلُّهُمْ عَنِ الأَعْمَشِ، ح وَحَدَّثَنَا يَحْيَى بْنُ يَحْيَى، وَأَبُو كُرَيْبٍ - وَاللَّفْظُ لِيَحْيَى - قَالاَ حَدَّثَنَا أَبُو مُعَاوِيَةَ، عَنِ الأَعْمَشِ، عَنْ مُسْلِمِ بْنِ صُبَيْحٍ، عَنْ مَسْرُوقٍ، قَالَ جَاءَ إِلَى عَبْدِ اللَّهِ رَجُلٌ فَقَالَ تَرَكْتُ فِي الْمَسْجِدِ رَجُلاً يُفَسِّرُ الْقُرْآنَ بِرَأْيِهِ يُفَسِّرُ هَذِهِ الآيَةَ ‏ ((يَوْمَ تَأْتِي السَّمَاءُ بِدُخَانٍ مُبِينٍ‏))‏ قَالَ يَأْتِي النَّاسَ يَوْمَ الْقِيَامَةِ دُخَانٌ فَيَأْخُذُ بِأَنْفَاسِهِمْ حَتَّى يَأْخُذَهُمْ مِنْهُ كَهَيْئَةِ الزُّكَامِ ‏.‏ فَقَالَ عَبْدُ اللَّهِ مَنْ عَلِمَ عِلْمًا فَلْيَقُلْ بِهِ وَمَنْ لَمْ يَعْلَمْ فَلْيَقُلِ اللَّهُ أَعْلَمُ فَإِنَّ مِنْ فِقْهِ الرَّجُلِ أَنْ يَقُولَ لِمَا لاَ عِلْمَ لَهُ بِهِ اللَّهُ أَعْلَمُ ‏.‏ إِنَّمَا كَانَ هَذَا أَنَّ قُرَيْشًا لَمَّا اسْتَعْصَتْ عَلَى النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم دَعَا عَلَيْهِمْ بِسِنِينَ كَسِنِي يُوسُفَ فَأَصَابَهُمْ قَحْطٌ وَجَهْدٌ حَتَّى جَعَلَ الرَّجُلُ يَنْظُرُ إِلَى السَّمَاءِ فَيَرَى بَيْنَهُ وَبَيْنَهَا كَهَيْئَةِ الدُّخَانِ مِنَ الْجَهْدِ وَحَتَّى أَكَلُوا الْعِظَامَ فَأَتَى النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم رَجُلٌ فَقَالَ يَا رَسُولَ اللَّهِ اسْتَغْفِرِ اللَّهَ لِمُضَرَ فَإِنَّهُمْ قَدْ هَلَكُوا فَقَالَ ‏"‏ لِمُضَرَ إِنَّكَ لَجَرِيءٌ ‏"‏ ‏.‏ قَالَ فَدَعَا اللَّهَ لَهُمْ فَأَنْزَلَ اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ ‏((‏إِنَّا كَاشِفُو الْعَذَابِ قَلِيلاً إِنَّكُمْ عَائِدُونَ‏)) ‏ قَالَ فَمُطِرُوا فَلَمَّا أَصَابَتْهُمُ الرَّفَاهِيَةُ - قَالَ - عَادُوا إِلَى مَا كَانُوا عَلَيْهِ - قَالَ - فَأَنْزَلَ اللَّهُ عَزَّ وَجَلَّ: ((فَارْتَقِبْ يَوْمَ تَأْتِي السَّمَاءُ بِدُخَانٍ مُبِينٍ * يَغْشَى النَّاسَ هَذَا عَذَابٌ أَلِيمٌ)) ((يَوْمَ نَبْطِشُ الْبَطْشَةَ الْكُبْرَى إِنَّا مُنْتَقِمُونَ))قَالَ يَعْنِي يَوْمَ بَدْرٍ ‏.‏

Ametuhadithia Abu Bakr bin Abiy Shaybah, wametuhadithia Abu Mu’aawiyah na Waqiy’u [mpaka mwisho wa Isnaad]. Amenihadithia Abu Sa’iyd, Al-Ashajju, ametueleza Wakiy’u [mpaka mwisho wa Isnaad]. Ametuhadithia ‘Uthmaan bin Abu Shaybah, ametuhadithia Jariyr, na wote toka kwa Al A‘amash [mpaka mwisho wa Isnaad]. Na Yahyaa bin Yahyaa pamoja na Abu Kurayb wametuhadithia –na tamko ni la Yahyaa- wamesema: Ametuhadithia Abu Mu’aawiyah, toka kwa Al A‘amash, toka kwa Muslim bin Swubayh, toka kwa Masruwq, amesema: Mtu mmoja alikuja kwa ‘Abdullaah [Ibn Mas‘uwd] akamwambia: Nimemwacha mtu Msikitini akiifasiri Qur-aan kwa rai yake,  anaifasiri Aayah hii:

يَوْمَ تَأْتِي السَّمَاءُ بِدُخَانٍ مُّبِينٍ

Siku mbingu zitakapoleta moshi bayana…. akisema: Utawajia watu moshi Siku ya Qiyaamah uzizuie pumzi zao na kuwafanya kama waliopatwa na mafua. ‘Abdullaah akasema: Aliyeijua elimu basi na aizungumze, na ambaye hajui basi aseme tu “Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi.” Kwani usomi wa kweli wa mtu, ni pale anaposema “Allaah Ndiye Mjuzi Zaidi.” kwa lile asilolijua. Na ukweli wa khabari [ya Aayah hii] ni kuwa, Maquraysh walipompinga  Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم) na kumfanyia inadi, aliwaapizia iwapige miaka ya njaa na ukame sawa na miaka ya ukame na njaa ya Yuwsuf. Ukame na uchovu mkali ukawashambulia kiasi cha kumfanya mtu anapoangalia juu aone mfano wa moshi kati yake na mbingu kutokana na uchovu, na hata wakala mifupa. Mtu mmoja akamjia Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)   akamwambia: Ee Rasuli wa Allaah! Waombee Mudhwar maghfirah kwa Allaah, hakika wao wamehiliki. Akamwambia:  Niwaombee Mudhwar, hakika wewe ni jasiri mno! [Wa kunitaka niwaombee pamoja na maasia waliyonayo na ushirikina wao]. [Rasuli] akawaombea, na Allaah (عز وجل)    Akateremsha:

 

إِنَّا كَاشِفُو الْعَذَابِ قَلِيلًا ۚ إِنَّكُمْ عَائِدُونَ

Hakika Sisi Tutaiondosha adhabu kidogo, lakini nyinyi hakika mtarudia vile vile.

 

Anasema: Wakapata mvua, na maisha yao yalipoboreka na kustawi, walirudi katika hali yao ya kwanza [ya kupinga na kufanya inadi], na Allaah (عز وجل)    Akateremsha:

 

فَارْتَقِبْ يَوْمَ تَأْتِي السَّمَاءُ بِدُخَانٍ مُّبِينٍ  • يَغْشَى النَّاسَ ۖ هَـٰذَا عَذَابٌ أَلِيمٌ  • يَوْمَ نَبْطِشُ الْبَطْشَةَ الْكُبْرَىٰ إِنَّا مُنتَقِمُونَ

Basi ngojea uangaze siku mbingu zitakapoleta moshi bayana • Utawafunika watu. Hii ni adhabu iumizayo • Siku Tutakayoshambulia mashambulio makubwa hakika Sisi ni Wenye kulipiza…akasema: Yaani, Siku ya Badr.

 

[Muslim - Kitaabu Swifatil Qiyaamati wal Jannati wan Naar (Chuo Cha Sifa Za Qiyaamah, Pepo na Moto) Mlango Wa Moshi]

 

 

Na pia,

 

Ametuhadithia Yahyaa, ametuhadithia Abu Mu’aawiyah, toka kwa Al- A‘amash, toka kwa Muslim, toka kwa Masruwq amesema: Amesema ‘Abdullaah: Hakika hili lilikuwa, kwa kuwa Maquraysh walipompinga Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم)   na kumfanyia inadi, aliwaapizia iwapige miaka ya njaa na ukame kama miaka ya ukame na njaa ya Yuwsuf. Ukame na uchovu mkali ukawapiga mpaka wakala mifupa, na mtu akawa anapoangalia juu, anaona kati yake na kati ya mbingu mfano wa moshi kutokana na uchovu mkali. Na hapo Allaah Ta’aalaa Akateremsha:

فَارْتَقِبْ يَوْمَ تَأْتِي السَّمَاءُ بِدُخَانٍ مُّبِينٍ  • يَغْشَى النَّاسَ ۖ هَـٰذَا عَذَابٌ أَلِيمٌ

Basi ngojea uangaze siku mbingu zitakapoleta moshi bayana • Utawafunika watu. Hii ni adhabu iumizayo.

 

Mtu mmoja akamwendea Rasuli wa Allaah (صلى الله عليه وآله وسلم) akamwambia: Ee Rasuli wa Allaah: Mwombe Allaah Awateremshie mvua Mudhwar, hakika wameangamia. [Rasuli] akamwambia: Niwaombee Mudhwar, hakika wewe ni jasiri mno! [Wa kunitaka niwaombee pamoja na maasia waliyonayo na ushirikina wao]. Rasuli akaomba mvua, na Mudhwar wakapata mvua. Na hapo ikateremka:

 

إِنَّكُمْ عَائِدُونَ

Lakini nyinyi hakika mtarudia vile vile… Maisha yao yalipoboreka na kuwa ya raha, walirudi tena katika hali yao. Na hapo Allaah (عز وجل)  Akateremsha:

يَوْمَ نَبْطِشُ الْبَطْشَةَ الْكُبْرَىٰ إِنَّا مُنتَقِمُونَ

Siku Tutakayoshambulia mashambulio makubwa hakika Sisi ni Wenye kulipiza…

 

akasema: Yaani, Siku ya Badr.”

 

[Al-Bukhaariy katika Mujallad wa Kwanza ukurasa wa 192]

 

 

 

Share