64-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Majini Wameitika Risala Yake Na Wakalingania Majini Wenzao

Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

64-Majini Wameitika Risala Yake Na Wakalingania Majini Wenzao

 

Alhidaaya.com

 

 

Miongoni mwa fadhila zake Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) ni kwamba hata Majini waliposikiliza Qur-aan waliisifu Qur-aan kuwa ni ya ajabu na wakaiamini. Anasema Allaah (سُبْحانَهُ وَتَعالى):

 

قُلْ أُوحِيَ إِلَيَّ أَنَّهُ اسْتَمَعَ نَفَرٌ مِّنَ الْجِنِّ فَقَالُوا إِنَّا سَمِعْنَا قُرْآنًا عَجَبًا﴿١﴾ يَهْدِي إِلَى الرُّشْدِ فَآمَنَّا بِهِ ۖ وَلَن نُّشْرِكَ بِرَبِّنَا أَحَدًا﴿٢﴾

 

Sema (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلم): Nimefunuliwa Wahy kwamba kundi miongoni mwa majini lilisikiliza; wakasema: ‘Hakika sisi tumeisikia Qur-aan ya ajabu. Inaongoza kwenye uongofu, basi tukaiamini, na wala hatutomshirikisha Rabb   wetu na yeyote. [Al-Jinn: 1 – 2]

 

Bali wakawalingania majini wenzao kwa yafuatayo baada ya wao kwanza kuisikiliza Qur-aan kwa makini:

 

  • Wanyamaze na wasikilize kwa makini.

 

  • Wakasadikisha yaliyokuja kabla ya Qur-aan.

 

  • Wakawalingania waisadiki Qur-aan kwa kuwa inaongoza katika haki (Uislaam) na katika njia iliyonyooka.

 

  • Wamwitikie Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) na waitikie wito wa Allaah.

 

  • Waiamini Qur-aan na wamwamini Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) na wamwamini Allaah (عَزَّ وَجَلَّ).  

 

  • Kisha wakawahamasisha kuwa pindi wakifanya hivyo wataghufuriwa madhambi yao na wataepushwa na adhabu.

 

  • Kisha wakawaonywa majini wenzao kwamba pindi wasipoitikia wito huo wa Allaah na Rasuli Wake (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ), basi hawataweza kuepukana na adhabu ya Allaah (عَزَّ وَجَلَّ) na watabakia kuwa katika upotofu wa dhahiri.

 

Kauli za Allaah (عَزَّ وَجَلَّ):

 

 

وَإِذْ صَرَفْنَا إِلَيْكَ نَفَرًا مِّنَ الْجِنِّ يَسْتَمِعُونَ الْقُرْآنَ فَلَمَّا حَضَرُوهُ قَالُوا أَنصِتُوا ۖ فَلَمَّا قُضِيَ وَلَّوْا إِلَىٰ قَوْمِهِم مُّنذِرِينَ﴿٢٩﴾ قَالُوا يَا قَوْمَنَا إِنَّا سَمِعْنَا كِتَابًا أُنزِلَ مِن بَعْدِ مُوسَىٰ مُصَدِّقًا لِّمَا بَيْنَ يَدَيْهِ يَهْدِي إِلَى الْحَقِّ وَإِلَىٰ طَرِيقٍ مُّسْتَقِيمٍ﴿٣٠﴾ يَا قَوْمَنَا أَجِيبُوا دَاعِيَ اللَّـهِ وَآمِنُوا بِهِ يَغْفِرْ لَكُم مِّن ذُنُوبِكُمْ وَيُجِرْكُم مِّنْ عَذَابٍ أَلِيمٍ﴿٣١﴾ وَمَن لَّا يُجِبْ دَاعِيَ اللَّـهِ فَلَيْسَ بِمُعْجِزٍ فِي الْأَرْضِ وَلَيْسَ لَهُ مِن دُونِهِ أَوْلِيَاءُ ۚأُولَـٰئِكَ فِي ضَلَالٍ مُّبِينٍ﴿٣٢﴾

Na pale Tulipowaelekeza kwako (ee Muhammadصلى الله عليه وآله وسلم) ) kundi miongoni mwa majini wakisikiliza kwa makini Qur-aan; walipoihudhuria, walisema: Bakieni kimya msikilize! Ilipomalizika; waligeuka kurudi kwa kaumu yao wakiwa wenye kuonya. Wakasema: Enyi kaumu yetu! Hakika sisi tumesikia Kitabu kimeteremshwa baada ya Muwsaa, kinachosadikisha yaliyo kabla yake, kinaongoza kwenye haki na kuelekea njia iliyonyooka. Enyi kaumu yetu! Mwitikieni mlinganiaji wa Allaah, na mwaminini!  (Allaah) Atakughufurieni madhambi yenu, na Atakukingeni na adhabu iumizayo. Na yeyote asiyemuitikia mlinganiaji wa Allaah, basi hawezi kushinda kukwepa katika ardhi na hatokuwa na walinzi badala ya Allaah.  Hao wamo katika upotofu bayana. [Al-Ahqaaf (46): 29 – 32]

 

 

Share