Juisi Ya Embe

VIPIMO
Maembe yaliyoiva 2
Mtindi (yogurt) 2 Vikombe vya chai
Maziwa 1 Kikombe cha chai
Asali au Sukari ¼ Kikombe cha chai
Maji ya ndimu ½ Kipande
Barafu 12 vipande
Kungumanga ya unga kidogo
NAMNA YA KUTAYARISHA
-
Ambua maembe kisha ukate kate vipande.
-
Weka vipimo vyote isipokuwa kungumanga, kwenye mashine ya kusagia (blender).
-
Saga hadi ilainike.
-
Mimina kwenye gilasi na unyunyize ile kungumanga na itakuwa tayari.
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


