A-Majina Ya Swahaba: Maana, Wasifu Wao Kwa Mukhtasari: ‘Abdullaah bin Mas’uwd

 

A-Majina Ya Swahaba: Maana, Wasifu Wao Kwa Mukhtasari

 

‘Abdullaah bin Mas’uwd (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ)

 

 

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

Jina lake:

 

‘Abdullaah bin Mas’uwd

 

(Al-Qurayshiyy)

عبد الله ابن مسعود

 

 

Maana Yake: Mja wa Allaah

 

 

 

Wasifu Wake:

 

 

‘Abdullaah bin Mas’uwd (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) alitoka kwenye mazingira ya kimaskini.

 

Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alikuwa akimpenda sana na akipenda sana usomaji wake wa Qur-aan. 

 

 

Ni Swahaba wa kwanza aliyesimama mbele ya ma-Quraysh bila uwoga na kusoma Qur-aan kwa sauti kubwa.  

 

 

‘Abdullaah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) alikua ni mtunzaji siri za Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ).

 

 

Na ni Swahaba ambaye daiman alikua akimbebea Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) viatu vyake.

 

 

Alikua ni Swahaba mwembamba na mwenye miguu membamba sana. Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمْ) alisema kuwa miguu ya ‘Abdullaah itakuwa mizito katika Miyzaan Siku ya Qiyaamah kuliko Jabal Uhud.

 

 

‘Abdullaah (رضي الله عنه) alikua ni hakimu wa Kufa na pia muweka hazina katika ukhalifa wa ‘Umar na mwanzo wa ukhalifa wa ‘Uthmaan, kisha akahamia Madiynah.

 

 

 

Kufariki Kwake:

 

 

‘Abdullaah bin Mas-‘uwd (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) alifariki Madiynah mwaka 32AH alipofika umri wa miaka 70 na alizikwa Al-Baaqiy.

 

 

 

 

Share