07-Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم): Miujiza Yake: Kuzidi Chakula

 

Fadhila Za Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)

 

07-Miujiza Yake: Kuzidi Chakula

 

Alhidaaya.com

 

Miujiza yake Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) ya kuongezeka chakula na vinywaji imetokea mara kadhaa na katika hali na sehemu tofauti. Kati ya miujiza ya kuongezeka chakula ni kama ilivyothibiti katika Hadiyth zifuatazo:

 

Hadiyth Ya 1:

 

حَدَّثَنَا أَبُو النُّعْمَانِ، قَالَ حَدَّثَنَا مُعْتَمِرُ بْنُ سُلَيْمَانَ، قَالَ حَدَّثَنَا أَبِي، حَدَّثَنَا أَبُو عُثْمَانَ، عَنْ عَبْدِ الرَّحْمَنِ بْنِ أَبِي بَكْرٍ، أَنَّ أَصْحَابَ الصُّفَّةِ، كَانُوا أُنَاسًا فُقَرَاءَ، وَأَنَّ النَّبِيَّ صلى الله عليه وسلم قَالَ ‏ "‏ مَنْ كَانَ عِنْدَهُ طَعَامُ اثْنَيْنِ فَلْيَذْهَبْ بِثَالِثٍ، وَإِنْ أَرْبَعٌ فَخَامِسٌ أَوْ سَادِسٌ ‏"‏‏.‏ وَأَنَّ أَبَا بَكْرٍ جَاءَ بِثَلاَثَةٍ فَانْطَلَقَ النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم بِعَشَرَةٍ، قَالَ فَهْوَ أَنَا وَأَبِي وَأُمِّي، فَلاَ أَدْرِي قَالَ وَامْرَأَتِي وَخَادِمٌ بَيْنَنَا وَبَيْنَ بَيْتِ أَبِي بَكْرٍ‏.‏ وَإِنَّ أَبَا بَكْرٍ تَعَشَّى عِنْدَ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم ثُمَّ لَبِثَ حَيْثُ صُلِّيَتِ الْعِشَاءُ، ثُمَّ رَجَعَ فَلَبِثَ حَتَّى تَعَشَّى النَّبِيُّ صلى الله عليه وسلم فَجَاءَ بَعْدَ مَا مَضَى مِنَ اللَّيْلِ مَا شَاءَ اللَّهُ، قَالَتْ لَهُ امْرَأَتُهُ وَمَا حَبَسَكَ عَنْ أَضْيَافِكَ ـ أَوْ قَالَتْ ضَيْفِكَ ـ قَالَ أَوَمَا عَشَّيْتِيهِمْ قَالَتْ أَبَوْا حَتَّى تَجِيءَ، قَدْ عُرِضُوا فَأَبَوْا‏.‏ قَالَ فَذَهَبْتُ أَنَا فَاخْتَبَأْتُ فَقَالَ يَا غُنْثَرُ، فَجَدَّعَ وَسَبَّ، وَقَالَ كُلُوا لاَ هَنِيئًا‏.‏ فَقَالَ وَاللَّهِ لاَ أَطْعَمُهُ أَبَدًا، وَايْمُ اللَّهِ مَا كُنَّا نَأْخُذُ مِنْ لُقْمَةٍ إِلاَّ رَبَا مِنْ أَسْفَلِهَا أَكْثَرُ مِنْهَا‏.‏ قَالَ يَعْنِي حَتَّى شَبِعُوا وَصَارَتْ أَكْثَرَ مِمَّا كَانَتْ قَبْلَ ذَلِكَ، فَنَظَرَ إِلَيْهَا أَبُو بَكْرٍ فَإِذَا هِيَ كَمَا هِيَ أَوْ أَكْثَرُ مِنْهَا‏.‏ فَقَالَ لاِمْرَأَتِهِ يَا أُخْتَ بَنِي فِرَاسٍ مَا هَذَا قَالَتْ لاَ وَقُرَّةِ عَيْنِي لَهِيَ الآنَ أَكْثَرُ مِنْهَا قَبْلَ ذَلِكَ بِثَلاَثِ مَرَّاتٍ‏.‏ فَأَكَلَ مِنْهَا أَبُو بَكْرٍ وَقَالَ إِنَّمَا كَانَ ذَلِكَ مِنَ الشَّيْطَانِ ـ يَعْنِي يَمِينَهُ ـ ثُمَّ أَكَلَ مِنْهَا لُقْمَةً، ثُمَّ حَمَلَهَا إِلَى النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم فَأَصْبَحَتْ عِنْدَهُ، وَكَانَ بَيْنَنَا وَبَيْنَ قَوْمٍ عَقْدٌ، فَمَضَى الأَجَلُ، فَفَرَّقَنَا اثْنَا عَشَرَ رَجُلاً، مَعَ كُلِّ رَجُلٍ مِنْهُمْ أُنَاسٌ، اللَّهُ أَعْلَمُ كَمْ مَعَ كُلِّ رَجُلٍ فَأَكَلُوا مِنْهَا أَجْمَعُونَ، أَوْ كَمَا قَالَ‏.‏

Amesimulia ‘Abdur-Rahman bin Abiy Bakr (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) :   Hakika watu wa Swuffah walikuwa mafakiri. Na Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) mara moja alisema: “Mwenye chakula cha watu wawili, amchuke wa tatu (yaani amchukue mtu mmoja miongoni mwao), na yeyote mwenye chakula cha kuwatosha watu wane, achukue wa tano au wa sita (au alisema mfano wake).” Abu Bakr alichukua watu watatu ilhali Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) alichukua kumi. Na Abu Bakr pamoja na watu wake watatu wa familia ambao ni mimi, babangu na mamangu. Mpokezi akawa ana shaka kama ‘Abdur-Rahman amesema: “Mke wangu na mtumishi, ambaye alikuwa ni huyo huyo nyumbani kwangu na nyumba ya Abu Bakr.” Abu Bakr alikula chakula cha usiku pamoja na Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) na akabaki huko mpaka akaswali Swalaah ya ‘Ishaa. Alirudi na kubaki na Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) mpaka akala chakula chake cha usiku. Baada ya kupita sehemu fulani ya usiku, alirudi nyumbani kwake. Mkewe akamwambia: “Ni kitu kilichokuzuia na wageni wako?” Akasema: “Je, mmewapatia chakula cha usiku?” Akasema: “Wamekataa kula mpaka uje. Wao (yaani baadhi ya watu wa nyumbani) waliwapelekea chakula lakini walikataa (kula)”. Nilikwenda kujificha, akasema: “Ee Ghunthar!” Akamuomba Allaah Ayafanye masikio yangu kukatwa, naye akanikaripia. Akasema: “Kuleni!” Na akaongeza: “Mimi sitokula chakula”. Akasema: “Naapa kwa Allaah! Kila tulipokuwa tunachukua tonge ya chakula, chakula kilikuwa kikijaa kutoka chini zaidi kuliko tonge hilo mpaka kila mmoja akala na kushiba. Hata ivyo, chakula kilichobakia kilikuwa kingi kuliko kile cha awali. Abu Bakr akakiona chakula kilikuwa zaidi kuliko kile cha mwanzo”. Alimuita mkewe, “Ee dada wa Bani Firaas!” Akajibu, “Ee pozo la macho yangu. Chakula hiki kimeongezeka mara tatu zaidi.” Abu Bakr, alianza kula chakula hicho, na huku anasema: “Hakika hicho (yaani kiapo cha kutokula) ni kwa sababu ya shaytwaan.” Kisha akala tonge kwayo, na kumpelekea chengine Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم). Chakula hicho kikawa kwa Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم). Kulikuwa na sulhu baina yetu na watu fulani, na muda wa sulhu ulipomalizika, alitugawa makundi kumi na mbili, kila kimoja kikiongozwa na mtu. Allaah Ndiye Ajuaye watu wangapi walikuwa chini ya amiri wa kila kikundi. Hata hivyo, Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) alituma amiri kwa kila kikundi. Kisha wote wakala chakula hicho. [Al-Bukhaariy Kitaab Al-Manaaqib]

 

 

Hadiyth Ya 2:

 

حَدَّثَنَا أَبُو بَكْرِ بْنُ النَّضْرِ بْنِ أَبِي النَّضْرِ، قَالَ حَدَّثَنِي أَبُو النَّضْرِ، هَاشِمُ بْنُ الْقَاسِمِ حَدَّثَنَا عُبَيْدُ اللَّهِ الأَشْجَعِيُّ، عَنْ مَالِكِ بْنِ مِغْوَلٍ، عَنْ طَلْحَةَ بْنِ مُصَرِّفٍ، عَنْ أَبِي صَالِحٍ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ، قَالَ كُنَّا مَعَ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم فِي مَسِيرٍ - قَالَ - فَنَفِدَتْ أَزْوَادُ الْقَوْمِ قَالَ حَتَّى هَمَّ بِنَحْرِ بَعْضِ حَمَائِلِهِمْ - قَالَ - فَقَالَ عُمَرُ يَا رَسُولَ اللَّهِ لَوْ جَمَعْتَ مَا بَقِيَ مِنْ أَزْوَادِ الْقَوْمِ فَدَعَوْتَ اللَّهَ عَلَيْهَا ‏.‏ قَالَ فَفَعَلَ - قَالَ - فَجَاءَ ذُو الْبُرِّ بِبُرِّهِ وَذُو التَّمْرِ بِتَمْرِهِ - قَالَ وَقَالَ مُجَاهِدٌ وَذُو النَّوَاةِ بِنَوَاهُ - قُلْتُ وَمَا كَانُوا يَصْنَعُونَ بِالنَّوَى قَالَ كَانُوا يَمُصُّونَهُ وَيَشْرَبُونَ عَلَيْهِ الْمَاءَ ‏.‏ قَالَ فَدَعَا عَلَيْهَا - قَالَ - حَتَّى مَلأَ الْقَوْمُ أَزْوِدَتَهُمْ - قَالَ - فَقَالَ عِنْدَ ذَلِكَ ‏ "‏ أَشْهَدُ أَنْ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَأَنِّي رَسُولُ اللَّهِ لاَ يَلْقَى اللَّهَ بِهِمَا عَبْدٌ غَيْرَ شَاكٍّ فِيهِمَا إِلاَّ دَخَلَ الْجَنَّةَ ‏"‏ ‏.‏

 

 

Amesimulia Abu Hurayrah (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ):

Tulikuwa tukiongozana na Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) katika safari ya (kuelekea Tabuwk). Yeye (msimulizi) alisema: “Vitu na watu vilikuwa karibu vimepungua. Yeye (msimulizi) alisema: (Na hali ikawa mbaya sana) hadi kwamba (wanajeshi) waliamua kuchinja ngamia zao.” Yeye (msimulizi) akasema: Juu ya jambo hili ‘Umar alisema: “Ee Rasuli wa Allaah, laiti kama ungejumuisha  pamoja yale yaliyoachwa kwenye vifungu na watu na kisha muombe Allaah (Alete Barakah Zake) juu yake.” Yeye (msimulizi) alisema: “Yeye (Nabiy صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) alifanya hivyo.:  Yeye (msimulizi) akasema: “Yule aliyekuwa na ngano katika mali yake alikuja pale na ngano. Aliyekuwa na tende naye alikuja pale na tende. Na Mujahid akasema: “Aliyekuwa na kokwa za tende alikuja pale na kokwa.” Mimi (msimulizi) nikasema: “Walifanya nini na kokwa za tende?” Wakasema: “Wao (watu) walikuwa wakizifonza kuzikamua (mdomoni) na kisha wakanywa maji yake.” Yeye (msimulizi alisema): “Yeye (Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) Akaziombea (Baraka za Allaah)  juu yake (hizo rizki).” Yeye (msimulizi) alisema: “Na kulikuwa na ongezeko la muujiza katika rizki) hadi kwamba watu walijaza chakula chao kikamilifu.” Yeye (msimulizi) akasema: Wakati huo yeye (Nabiy (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) alisema:

أَشْهَدُ أَنْ لاَ إِلَهَ إِلاَّ اللَّهُ وَأَنِّي رَسُولُ اللَّهِ لاَ يَلْقَى اللَّهَ بِهِمَا عَبْدٌ غَيْرَ شَاكٍّ فِيهِمَا إِلاَّ دَخَلَ الْجَنَّةَ ‏"

Ash-hadu an laa ilaaha illa Allaah wa anniy Rasuwlu-Allaah.

Nashuhudia kwamba hapana mwabudiwa wa haki ila Allaah na kwamba mimi ni Rasuli wa Allaah.

Hakuna mja atakayekutana na Allaah kwazo Shahada mbili hizi, bila ya kutilia  shaka ndani yake, isipokuwa ataingia Jannah.” [Muslim Kitaab Al-Iymaan]

 

Hadiyth Ya 3:

 

حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ يُوسُفَ، أَخْبَرَنَا مَالِكٌ، عَنْ إِسْحَاقَ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ أَبِي طَلْحَةَ، أَنَّهُ سَمِعَ أَنَسَ بْنَ مَالِكٍ، يَقُولُ قَالَ أَبُو طَلْحَةَ لأُمِّ سُلَيْمٍ لَقَدْ سَمِعْتُ صَوْتَ، رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ضَعِيفًا، أَعْرِفُ فِيهِ الْجُوعَ فَهَلْ عِنْدَكِ مِنْ شَىْءٍ قَالَتْ نَعَمْ‏.‏ فَأَخْرَجَتْ أَقْرَاصًا مِنْ شَعِيرٍ، ثُمَّ أَخْرَجَتْ خِمَارًا لَهَا فَلَفَّتِ الْخُبْزَ بِبَعْضِهِ، ثُمَّ دَسَّتْهُ تَحْتَ يَدِي وَلاَثَتْنِي بِبَعْضِهِ، ثُمَّ أَرْسَلَتْنِي إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ فَذَهَبْتُ بِهِ، فَوَجَدْتُ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فِي الْمَسْجِدِ وَمَعَهُ النَّاسُ، فَقُمْتُ عَلَيْهِمْ فَقَالَ لِي رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏"‏ آرْسَلَكَ أَبُو طَلْحَةَ ‏"‏‏.‏ فَقُلْتُ نَعَمْ‏.‏ قَالَ بِطَعَامٍ‏.‏ فَقُلْتُ نَعَمْ‏.‏ فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم لِمَنْ مَعَهُ ‏"‏ قُومُوا ‏"‏‏.‏ فَانْطَلَقَ وَانْطَلَقْتُ بَيْنَ أَيْدِيهِمْ حَتَّى جِئْتُ أَبَا طَلْحَةَ فَأَخْبَرْتُهُ‏.‏ فَقَالَ أَبُو طَلْحَةَ يَا أُمَّ سُلَيْمٍ، قَدْ جَاءَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم بِالنَّاسِ، وَلَيْسَ عِنْدَنَا مَا نُطْعِمُهُمْ‏.‏ فَقَالَتِ اللَّهُ وَرَسُولُهُ أَعْلَمُ‏.‏ فَانْطَلَقَ أَبُو طَلْحَةَ حَتَّى لَقِيَ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم، فَأَقْبَلَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم وَأَبُو طَلْحَةَ مَعَهُ، فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم ‏"‏ هَلُمِّي يَا أُمَّ سُلَيْمٍ مَا عِنْدَكِ ‏"‏‏.‏ فَأَتَتْ بِذَلِكَ الْخُبْزِ، فَأَمَرَ بِهِ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فَفُتَّ، وَعَصَرَتْ أُمُّ سُلَيْمٍ عُكَّةً فَأَدَمَتْهُ، ثُمَّ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم فِيهِ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ يَقُولَ، ثُمَّ قَالَ ‏"‏ ائْذَنْ لِعَشَرَةٍ ‏"‏‏.‏ فَأَذِنَ لَهُمْ، فَأَكَلُوا حَتَّى شَبِعُوا ثُمَّ خَرَجُوا، ثُمَّ قَالَ ‏"‏ ائْذَنْ لِعَشَرَةٍ ‏"‏‏.‏ فَأَذِنَ لَهُمْ، فَأَكَلُوا حَتَّى شَبِعُوا ثُمَّ خَرَجُوا، ثُمَّ قَالَ ‏"‏ ائْذَنْ لِعَشَرَةٍ ‏"‏‏.‏ فَأَذِنَ لَهُمْ، فَأَكَلُوا حَتَّى شَبِعُوا ثُمَّ خَرَجُوا ثُمَّ قَالَ ‏"‏ ائْذَنْ لِعَشَرَةٍ ‏"‏‏.‏ فَأَكَلَ الْقَوْمُ كُلُّهُمْ وَشَبِعُوا، وَالْقَوْمُ سَبْعُونَ ـ أَوْ ثَمَانُونَ ـ رَجُلاً‏.‏

 

Amesimulia Anas bin Maalik (رَضِيَ اللهُ عَنْهُ) kuwa Abu Twalhah alimwambia Umm Sulaym (رَضِيَ اللهُ عَنْهُمَا)  “Nimesikia sauti ya Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم)  ikiwa dhaifu, nikagundua kuwa ana njaa. Je, unacho chakula?” Umm Sulaym akajibu: “Ndiyo.” Akatoa mikate ya shayiri, kisha akatoa ushungi wake na kuifunga mikate, kisha akauingiza mkononi mwangu na kuizungusha sehemu ya ushingi kwangu. Kisha akanituma niende kwa Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم).  Nikaenda na mikate niliyoibeba na nikamkuta Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) akiwa Msikitini pamoja na watu. Niliposimama mbele yake Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) akaniuliza: “Je, amekutuma Abu Twalhah?” Nikasema: “Ndiyo.” Akaniuliza: “Na chakula?” Nikasema: “Ndiyo.” Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم)  akawaambia waliokuwa pamoja naye, “Amkeni, njooni!” Akaondoka (akifuatana na wale watu) nami nikaondoka upesi nikiwa mbele yao hata nikafika kwa Abu Twalhah nikamueleza kilicho tokea. Abu Twalhah akasema kumwambia Umm Sulaym: “Ee Umm Sulaym! Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم)  anakuja pamoja na watu nasi hatuna cha kuwalisha.” Umm Sulaym akajibu kwa kusema: “Allaah na Rasuli Wake wanajua zaidi.” Abu Twalhah akaondoka kwenda kumpokea Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم), akaja Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم) akifuatana na Abu Twalhah. Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم)  akasema: “Umm Sulaym lete ulicho nacho”. Akauleta ule mkate, Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم)  akaamuru ukakatwa katwa, na Umm Sulaym akawaletea samli ikawa ndiyo siagi yao. Kisha Rasuli wa Allaah (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّم)  akasoma alichoweza kukisoma humo, kisha akasema: “Waruhusu watu kumi.” Akawaruhusu wakala mpaka wakashiba na wakatoka. Kisha akasema tena:  “Waruhusuni kumi wengine.” Akawaruhusu watu wote wakala na wakashiba na akawa anasema hivyo na wakala wote hadi wakaisha waliokuwepo. Jumla ya watu walikuwa kati ya sabiini na themanini. [Al-Bukhaariy Kitaab Al-Manaaqib]

 

Share