01-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kutembelea Mgonjwa Kufuata Jeneza, Kumswalia Maiti, Kuhudhuria Mazishi Yake na Kukaa Kwenye Kaburi Lake Kwa Muda

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب عيَادة المريض وَتشييع المَيّت

والصّلاة عليه وَحضور دَفنهِ وَالمكث عِنْدَ قبرهِ بَعدَ دَفنه

01-Mlango Wa Kutembelea Mgonjwa Kufuata Jeneza, Kumswalia Maiti, Kuhudhuria Mazishi Yake na Kukaa Kwenye Kaburi Lake Kwa Muda

 

Alhidaaya.com

 

 

Hadiyth – 1

عن البَرَاءِ بن عازِبٍ رضي الله عنهما ، قَالَ : أمَرَنَا رسولُ الله صلى الله عليه وسلم بعِيَادَةِ الْمَريضِ ، وَاتِّبَاعِ الجَنَازَةِ ، وَتَشْمِيتِ العَاطِسِ ، وَإبْرَارِ الْمُقْسِمِ ، وَنَصْرِ المَظْلُومِ ، وَإجَابَةِ الدَّاعِي ، وَإفْشَاءِ السَّلاَمِ . متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Al-Baraa' bin 'Aazib (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) amesema: "Ametuamuru sisi Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kuzuru wagonjwa, kufuata jeneza, kumwombea dua anapochemua mtu, kutekeleza viapo, kumnusuru aliyedhulumiwa, kuitikia mwaliko na kueneza salamu za amani." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 2

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( حَقُّ المُسْلِمِ عَلَى المُسْلِمِ خَمْسٌ : رَدُّ السَّلاَمِ ، وَعِيَادَةُ المَرِيضِ ، وَاتِّبَاعُ الجَنَائِزِ ، وَإجَابَةُ الدَّعْوَةِ ، وَتَشْمِيتُ العَاطِسِ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kwa Abuu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Haki ya Muislamu kwa Muislamu mwenziwe ni Tano: Kurudisha salamu (anapokusalimia kwa Assalaamu 'Alaykum), kumzuru mgonjwa, kufuata jeneza, kuitikia mwaliko na kumwombea dua anapochemua mmoja wenu." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

 

Hadiyth – 3

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه قَالَ : قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( إنَّ اللهَ عز وجل يَقُولُ يَومَ القِيَامَةِ : يَا ابْنَ آدَمَ ، مَرِضْتُ فَلَمْ تَعُدنِي ! قَالَ : يَا رَبِّ ، كَيْفَ أعُودُكَ وَأنْتَ رَبُّ العَالَمِينَ ؟! قَالَ : أمَا عَلِمْتَ أنَّ عَبْدِي فُلاَناً مَرِضَ فَلَمْ تَعُدْهُ ! أمَا عَلِمْتَ أنَّكَ لَوْ عُدْتَهُ لَوَجَدْتَني عِنْدَهُ ! يَا ابْنَ آدَمَ ، اسْتَطْعَمْتُكَ فَلَمْ تُطْعِمنِي ! قَالَ : يَا رَبِّ ، كَيْفَ أطْعِمُكَ وَأنْتَ رَبُّ العَالَمِينَ ؟! قَالَ : أمَا عَلِمْتَ أنَّهُ اسْتَطْعَمَكَ عَبْدِي فُلانٌ فَلَمْ تُطْعِمْهُ ! أمَا عَلِمْتَ أنَّكَ لَوْ أطْعَمْتَهُ لَوَجَدْتَ ذَلِكَ عِنْدِي ! يَا ابْنَ آدَمَ ، اسْتَسْقَيْتُكَ فَلَمْ تَسْقِنِي ! قَالَ : يَا رَبِّ ، كَيْفَ أسْقِيكَ وَأنْتَ رَبُّ العَالَمينَ ؟! قَالَ : اسْتَسْقَاكَ عَبْدِي فُلاَنٌ فَلَمْ تَسْقِهِ ! أمَا عَلِمْتَ أنَّكَ لَوْ سَقَيْتَهُ لَوَجَدْتَ ذَلِكَ عِنْدِي ! )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abuu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba  Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika Allaah 'Azza wa Jalla Atasema Siku ya Qiyaamah: "Ee mwanadamu! Nimeumwa hukunizuru." Atasema: "Ee Rabb wangu! Vipi nitakuzuru nawe ni Rabb wa viumbe vyote?" Atasema: "Je, hukujua kuwa mja wangu fulani ameumwa hukumzuru?, Hukujua lau ungemzuru ungenikuta kwake?, Ee mwanadamu! Nilikuomba chakula hukunilisha." Akasema: "Ee Rabb wangu! Vipi natakulisha nawe ni Rabb wa viumbe?", Atasema: "Hukujua mja wangu fulani alikuomba chakula hukumlisha?, Hukujua lau ungemlisha ungepata hilo kwangu?, Ee mwanadamu! Nilikuomba maji hukunipa." Atasema: "Ee Rabb wangu! Vipi nitakunywesha Nawe ni Rabb wa viumbe?", Allaah atasema: "Mja wangu fulani alikuomba maji hukumpa. Hukujua lau ungempa ungepata ujira wako Kwangu?" [Muslim].

 

 

Hadiyth – 4

وعن أَبي موسى رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( عُودُوا المَريضَ ، وَأطْعِمُوا الجَائِعَ ، وَفُكُّوا العَانِي )) رواه البخاري

Imepokewa kwa Abu Muwsaa Al-'Ash'ariy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Mtembeleeni mgonjwa, na mlisheni mwenye njaa msameheni mwenye makosa mateka." [Al-Bukhaariy] 

 

 

Hadiyth – 5

وعن ثوبان رضي الله عنه ، عن النبي صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( إنَّ المُسْلِمَ إِذَا عَادَ أخَاهُ المُسْلِمَ ، لَمْ يَزَلْ في خُرْفَةِ الْجَنَّةِ حَتَّى يَرْجِعَ )) قِيلَ : يَا رَسولَ الله ، وَمَا خُرْفَةُ الجَنَّةِ ؟ قَالَ : (( جَنَاهَا )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Thawbaan (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika Muislamu anapomzuru nduguye Muislamu aliye mgonjwa huwa miongoni pamoja na Khurfah ya Peponi mpaka arudipo." Pakasemwa: "Ee Rasuli wa Allaah! Na Khurfah ya Peponi ni nini?" Akasema: "Matunda yake." [Muslim]

 

 

Hadiyth – 6

وعن عليّ رضي الله عنه ، قَالَ : سَمِعْتُ رسولَ الله صلى الله عليه وسلم ، يَقُولُ : (( مَا مِنْ مُسْلِم يَعُودُ مُسْلِماً غُدْوة إِلاَّ صَلَّى عَلَيْهِ سَبْعُونَ ألْفَ مَلَكٍ حَتَّى يُمْسِي ، وَإنْ عَادَهُ عَشِيَّةً إِلاَّ صَلَّى عَلَيْهِ سَبْعُونَ ألْفَ مَلَكٍ حَتَّى يُصْبحَ ، وَكَانَ لَهُ خَرِيفٌ في الْجَنَّةِ )) رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .

Kutoka kwa 'Aliy (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Nimemsikia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: "Hakuna Muislamu anayemtembelea Muislamu mwenziwe aliye mgonjwa baina ya Swalaah ya Alfajiri na kuchomoza jua isipokuwa wanamuombea yeye Malaika elfu sabiini mpaka kuingie jioni. Na akimtembelea mwisho wa mchana huwa wanamuombea yeye Malaika elfu sabiini mpaka kupambazuke. Na anapatiwa bustani la matunda Peponi." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan]

 

 

Hadiyth – 7

وعن أنسٍ رضي الله عنه ، قَالَ : كَانَ غُلاَمٌ يَهُودِيٌّ يَخْدُمُ النَّبيَّ صلى الله عليه وسلم ، فَمَرِضَ ، فَأتَاهُ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم يَعُودُهُ ، فَقَعَدَ عِنْدَ رَأسِهِ ، فَقَالَ لَهُ : (( أسْلِمْ )) فَنَظَرَ إِلَى أبِيهِ وَهُوَ عِنْدَهُ ؟ فَقَالَ : أَطِعْ أَبَا القَاسِمِ ، فَأسْلَمَ ، فَخَرَجَ النَّبيُّ صلى الله عليه وسلم ، وَهُوَ يَقُولُ : (( الحَمْدُ للهِ الَّذِي أنْقَذَهُ منَ النَّارِ )) رواه البخاري .

Amesema Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu): Kulikuwa na kijana wa kiyahudi aliyekuwa akimtumikia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Alishikwa na ugonjwa na hivyo Nabiy alimzuru na akakaa karibu na kichwa chake na akamwambia: "Silimu." Kijana alimtizama babake aliye naye. Babake Akamwambia: "Mtii Abul Qaasim (yaani Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Kijana alisilimu, naye Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alitoka nyumbani kwao na huku anasema: "Sifa zote anastahiki Allaah aliyemuepusha na moto." [Al-Bukhaariy].

 

 

 

Share