15-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kuharakisha Jeneza

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب الإسراع بالجنازة

15-Mlango Wa Kuharakisha Jeneza

 

Alhidaaya.com

 

 

Hadiyth – 1

عن أَبي هريرة رضي الله عنه ، عن النبيِّ صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( أسْرِعُوا بالجَنَازَةِ ، فَإنْ تَكُ صَالِحَةً ، فَخَيرٌ تُقَدِّمُونَهَا إِلَيْهِ ، وَإنْ تَكُ سِوَى ذَلِكَ ، فَشَرٌّ تَضَعُونَهُ عَنْ رِقَابِكُمْ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

وفي روايةٍ لمسلمٍ : (( فَخَيْرٌ تُقَدِّمُونَهَا عَلَيْهِ )) .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Liharakisheni jeneza (lipelekeni haraka), kama litakuwa la mwema basi mnalipeleka kwenye kheri na kama halikuwa hivyo basi mnajiodoshea mwovu shingoni mwenu." [Al-Bukhaariy, Muslim, Maalik, Abuu Daawuwd, At-Tirmidhiy na An-Nasaai]

 

 

Hadiyth – 2

وعن أَبي سعيد الخدري رضي الله عنه ، قَالَ : كَانَ النبي صلى الله عليه وسلم ، يقُولُ : (( إِذَا وُضِعَت الجَنَازَةُ ، فَاحْتَمَلَهَا الرِّجَالُ عَلَى أعنَاقِهمْ ، فَإنْ كَانَتْ صَالِحَةً ، قالتْ : قَدِّمُونِي ، وَإنْ كَانَتْ غَيْرَ صَالِحَةٍ ، قَالَتْ لأَهْلِهَا : يَا وَيْلَهَا أَيْنَ تَذْهَبُونَ بِهَا ؟ يَسْمَعُ صَوْتَهَا كُلُّ شَيْءٍ إِلاَّ الإنْسَانَ ، وَلَوْ سَمِعَ الإنسَانُ لَصَعِقَ )) رواه البخاري .

Amesema Abu Sa'iyd Al-Khudriy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Itakapokuwa tayari jeneza na ikabebwa na watu juu ya mabega yao, akiwa ni mtu mwema atasema: 'Nipelekeni mbele, nipelekeni mbele (yaani nifikisheni haraka katika kaburi langu). Na ikiwa si mwema atasema: 'Ee, ole wake! Munaipeleka wapi?' Sauti yake inasikika na kila kitu isipokuwa mwanadamu na lau angesikia (mwanadamu) basi angezimia." [Al-Bukhaariy]

 

 

 

Share