37-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Kusisitizwa Wajibu wa Zakaah na Kubainisha Fadhila Zake na Mambo Yanayohusiana Nayo

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

 

باب تأكيد وجوب الزكاة وبيان فضلها وَمَا يتعلق بِهَا

37-Mlango Wa Kusisitizwa Wajibu wa Zakaah na Kubainisha Fadhila Zake na Mambo Yanayohusiana Nayo

 

Alhidaaya.com

 

قال الله تَعَالَى :

وَأَقِيمُوا الصَّلَاةَ وَآتُوا الزَّكَاةَ  ﴿٤٣﴾

Na simamisheni Swalaah na toeni Zakaah [Al-Baqarah: 43]

 

وَمَا أُمِرُوا إِلَّا لِيَعْبُدُوا اللَّـهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ حُنَفَاءَ وَيُقِيمُوا الصَّلَاةَ وَيُؤْتُوا الزَّكَاةَۚ وَذَٰلِكَ دِينُ الْقَيِّمَةِ ﴿٥﴾

Na hawakuamrishwa isipokuwa wamwabudu Allaah hali ya kuwa ni wenye kumtakasia Dini, wenye kujiengua na upotofu kuelemea Dini ya haki, na wasimamishe Swalaah na watoe Zakaah. Na hiyo ndiyo Dini iliyosimama imara. [Al-Bayyinah: 5]

 

خُذْ مِنْ أَمْوَالِهِمْ صَدَقَةً تُطَهِّرُهُمْ وَتُزَكِّيهِم بِهَا وَصَلِّ عَلَيْهِمْ ۖ ﴿١٠٣﴾

Chukua (ee Muhammad صلى الله عليه وآله وسلمkatika mali zao Swadaqah, uwatwaharishe na uwatakase kwazo, na waombee Du’aa (na Maghfirah). [At-Tawbah: 103]

 

Hadiyth – 1

وعن ابن عمر رضي الله عنهما : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( بُنِيَ الإسْلاَمُ عَلَى خَمْسٍ : شَهَادَةِ أنْ لاَ إلهَ إِلاَّ اللهُ ، وَأنَّ مُحَمَّداً عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ ، وَإقَامِ الصَّلاَةِ ، وَإيتَاءِ الزَّكَاةِ ، وَحَجِّ البَيْتِ ، وَصَوْمِ رَمَضَانَ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Umejengwa Uislamu juu ya nguzo tano: Kikiri kwa moyo na kubaini kwa ulimi kwamba hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah, na kwamba Muhammad ni Rasuli wa Allaah, na kusimamisha Swalaah, na kutoa Zakaah, na kuhiji na kufunga mwezi wa Ramadhwaan." [Al-Bukhaariy, Muslim, At-Tirmidhiy na An-Nasaaiy]

 

Hadiyth – 2

وعن طَلْحَةَ بن عبيد الله رضي الله عنه ، قَالَ : جَاءَ رَجُلٌ إِلَى رسولِ الله صلى الله عليه وسلم مِنْ أَهْلِ نَجْدٍ ثَائِرُ الرَّأسِ نَسْمَعُ دَوِيَّ صَوْتِهِ ، وَلاَ نَفْقَهُ مَا يَقُولُ ، حَتَّى دَنَا مِنْ رسولِ الله صلى الله عليه وسلم ، فَإذا هُوَ يَسألُ عَنِ الإسْلاَم ، فَقَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( خَمْسُ صَلَواتٍ في اليَوْمِ وَاللَّيْلَةِ )) قَالَ : هَلْ عَلَيَّ غَيْرُهُنَّ ؟ قَالَ : (( لاَ ، إِلاَّ أنْ تَطَّوَّعَ )) فَقَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( وَصِيامُ شَهْرِ رَمَضَانَ )) قَالَ : هَلْ عَلَيَّ غَيْرُهُ ؟ قَالَ : (( لاَ ، إِلاَّ أنْ تَطَّوَّعَ )) قَالَ : وَذَكَرَ لَهُ رسول الله صلى الله عليه وسلم الزَّكَاةَ ، فَقَالَ : هَلْ عَلَيَّ غَيْرُهَا ؟ قَالَ : (( لاَ ، إِلاَّ أنْ تَطَّوَّعَ )) فَأدْبَرَ الرَّجُلُ وَهُوَ يَقُولُ : وَاللهِ لاَ أُزِيدُ عَلَى هَذَا وَلاَ أنْقُصُ مِنْهُ ، فَقَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( أفْلَحَ إنْ صَدَقَ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Amesema Twalhah bin 'Ubaydillaah (Radhwiya Allaahu 'anhu): Alikuja mtu kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kutoka Najd, nywele timtim. Tunasikia mvumo wa sauti yake, wala hatuelewi anachosema, mpaka akamkaribia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) tukajua kumbe anauliza kuhusu Uislamu, akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) : "Zipo Swalaah tano mchana na usiku." Akasema: "Je, kuna Swalaah nyingine mbali na hizo?" Akasema: "Hapana, ila za Sunnah." Akasema Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Na funga ya mwezi wa Ramadhwaan." Akauliza: "Je, kuna funga nyingine mbali na hiyo?" Akasema: "Hapana ila funga ya khiari." Akasema Twalhah: "Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alimtajia kuhusu Zakaah." Akauliza yule mtu: "Je, kuna nyingine mbali na hiyo?" Akasema: "Hapana, ila unaweza kutoa swadaqah." Aliondoka yule mtu na huku anasema: "Naapa kwa Allaah sitazidisha juu ya hizi wala sitazipunguza juu ya hizi wala sitazipunguza." Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: "Kama amesema kweli, basi amefanikiwa (yaani ataingizwa Peponi)." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hadiyth – 3

وعن ابن عباس رضي الله عنه : أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلم بعث مُعاذاً رضي الله عنه إِلَى اليَمَنِ ، فَقَالَ : (( ادْعُهُمْ إِلَى شَهَادَةِ أنْ لاَ إلهَ إِلاَّ اللهُ وَأنِّي رسول اللهِ ، فإنْ هُمْ أطَاعُوا لِذلِكَ ، فَأعْلِمْهُمْ أن اللهَ تَعَالَى ، افْتَرَضَ عَلَيْهِمْ خَمْسَ صَلَواتٍ في كُلِّ يَوْمٍ وَلَيْلَةٍ ، فَإنْ هُمْ أطَاعُوا لِذلِكَ ، فَأعْلِمْهُمْ أنَّ اللهَ افْتَرَضَ عَلَيْهِمْ صَدَقَةً تُؤخَذُ مِنْ أغْنِيَائِهِمْ ، وتُرَدُّ عَلَى فُقَرَائِهِمْ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Abbaas (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipomtuma Mu'aadh (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwenda Yemen alimwambia: "Waite katika kushuhudia ya kwamba hapana anayepaswa kuabudiwa isipokuwa Allaah na kuwa mimi ni Rasuli wa Allaah. Wanapokutii katika hilo basi wafahamishe kuwa Allaah Ta'aalaa amewafaridhisha Swalaah tano kwa kila mchana na usiku. Ikiwa watakutii katika hilo basi wajulishe kuwa Allaah amefaradhisha juu yao swadaqah inayochukuliwa kutoka kwa matajiri miongoni mwao na inarejeshwa kwa mafukara wao." [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy na An-Nasaaiy]

 

Hadiyth – 4

وعن ابن عمر رضي الله عنهما ، قَالَ : قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( أُمِرْتُ أنْ أُقَاتِلَ النَّاسَ حَتَّى يَشْهَدُوا أنْ لاَ إلهَ إِلاَّ اللهُ، وَأنَّ مُحَمَّداً رسول الله ، وَيُقِيمُوا الصَّلاةَ ، وَيُؤتُوا الزَّكَاةَ، فَإذَا فَعَلُوا ذَلِكَ عَصَمُوا مِني دِمَاءهُمْ وَأمْوَالَهُمْ ، إِلاَّ بِحَقِّ الإسْلاَمِ ، وَحِسَابُهُم عَلَى الله )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Nimeamrishwa niwapige watu vita mpaka wakiri kwa moyo na watamke kwa ulimi kuwa, 'Hakuna Mola anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Allaah na kuwa Muhammad ni Rasuli wa Allaah, na wadumishe Swalaah na watoe Zakaah na kama watafanya hivyo wamesalimisha damu zao na mali zao isipokuwa kwa haki ya Uislamu na hesabu yao iko kwa Allaah." [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Hadiyth – 5

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : لَمَّا تُوُفِّيَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم - وَكَانَ أَبُو بَكْرٍ رضي الله عنه - وَكَفَرَ مَنْ كَفَرَ مِنَ العَرَبِ ، فَقال عُمَرُ رضي الله عنه : كَيْفَ تُقَاتِلُ النَّاسَ وَقَدْ قَالَ رسولُ الله صلى الله عليه وسلم : (( أُمِرْتُ أنْ أُقَاتِلَ النَّاسَ حَتَّى يَقُولوُا لاَ إلهَ إِلاَّ اللهُ ، فَمَنْ قَالَهَا فَقَدْ عَصَمَ مِنِّي مَالَهُ وَنَفْسَهُ إِلاَّ بِحَقِّهِ ، وَحِسَابُهُ عَلَى الله )) فَقَالَ أَبُو بَكْرٍ : وَاللهِ لأُقَاتِلَنَّ مَنْ فَرَّقَ بين الصَّلاَةِ وَالزَّكَاةِ ، فَإنَّ الزَّكَاةَ حَقُّ المَالِ . وَاللهِ لَوْ مَنَعُونِي عِقَالاً كَانُوا يُؤدُّونَهُ إِلَى رسولِ الله صلى الله عليه وسلم ، لَقَاتَلْتُهُمْ عَلَى مَنْعِهِ . قَالَ عُمَرُ رضي الله عنه : فَوَاللهِ مَا هُوَ إِلاَّ أنْ رَأيْتُ اللهَ قَدْ شَرَحَ صَدْرَ أَبي بَكْرٍ لِلقِتَالِ ، فَعَرَفْتُ أنَّهُ الحَقُّ . متفقٌ عَلَيْهِ .

Amesema Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu): Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alipofishwa, na Abu Bakar (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa khalifah, na wakakufuru walio kufuru miongoni mwa Waarabu (Abu Bakar aliamua kuwapiga vita). 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhu) akauliza: "Vipi utawapiga watu vita wakati Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema, 'Nimeamrishwa kuwapiga watu vita mpaka waseme kuwa hakuna Mola anayestahiki kuabudiwa isipokuwa Allaah. Atakayesema hivyo atakuwa amelinda kwangu, mali na nafsi yake, isipokuwa kwa haki yake, na hesabu yake iko kwa Allaah'." Akasema Abu Bakar: "Naapa kwa Allaah! Nitampiga vita aliyetenganisha kati ya Swalaah na Zakaah, hakika Zakaah ni wajibu katika mali. Naapa kwa Allaah! Lau kama wangalininyima mtoto wa mbuzi tu waliyekuwa wanamtoa kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ningewapiga vita." 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhu) Akasema: "Naapa kwa Allaah! haikuwa isipokuwa Allaah Amekikunjua kifua cha Abu Bakar (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwa ajili ya vita, na nikaelewa kuwa hiyo ndiyo haki." [Al-Bukhaariy, Muslim, Abu Daawuwd, At-Tirmidhiy na An-Nassaiy]

 

Hadiyth – 6

وعن أَبي أيُّوب رضي الله عنه : أنّ رَجُلاً قَالَ للنبيِّ صلى الله عليه وسلم : أخْبِرْنِي بعمل يُدْخِلُنِي الجَنَّة ، قَالَ : (( تَعْبُدُ اللهَ ، وَلاَ تُشْرِكُ بِهِ شَيْئاً ، وَتُقِيمُ الصَّلاَةَ ، وَتُؤْتِي الزَّكَاةَ ، وَتَصِلُ الرَّحِمَ )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abu Ayyub (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa mtu mmoja alimuuliza Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam): "Nieleze amali itakayoniingiza Peponi?" Akasema: "Umuabudu Allaah wala usimshirikishe na chochote, udumishe Swalaah, utoe Zakaah na Uunge undugu." [Al-Bukhaariy na Muslim].

 

Hadiyth – 7

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه: أنَّ أعْرَابياً أتَى النبيَّ صلى الله عليه وسلم ، فَقَالَ : يَا رسولَ اللهِ، دُلَّنِي عَلَى عَمَلٍ إِذَا عَمِلْتُهُ ، دَخَلْتُ الجَنَّةَ . قَالَ : (( تَعْبُدُ اللهَ لاَ تُشْرِكُ بِهِ شَيْئاً ، وتُقِيمُ الصَّلاَةَ ، وتُؤتِي الزَّكَاةَ المَفْرُوضَةَ ، وَتَصُومُ رَمَضَانَ )) قَالَ : وَالذي نَفْسِي بِيَدِهِ ، لا أزيدُ عَلَى هَذَا ، فَلَمَّا وَلَّى ، قَالَ النبيُّ صلى الله عليه وسلم : (( مَنْ سَرَّهُ أنْ يَنْظُرَ إِلَى رَجُلٍ مِنْ أهْلِ الجَنَّةِ فَلْيَنْظُرْ إِلَى هَذَا )) متفقٌ عَلَيْهِ .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Mbedui mmoja alikuja kwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na kumwambia: "Nielekeze amali nikifanya nitaingia Peponi." Akamjibu: "Muabudu Allaah usimshirikishe na chochote, na dumisha Swalaah na utoe Zakaah za faradhi na ufunge Ramadhwaan." Akasema: "Ninaapa kwa yule ambaye nafsi yangu iko mikononi Mwake, siongezi zaidi ya hivi." Alipoondoka Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alisema: "Anayefurahishwa kumuangalia mtu miongoni mwa watu wa Peponi amuangalie mtu huyu." [Al-Bukhaariy na Muslim].

 

Hadiyth – 8

وعن جرير بن عبد الله رضي الله عنه ، قَالَ : بايَعْتُ النبيَ صلى الله عليه وسلم عَلَى إقَامِ الصَّلاَةِ ، وَإيتَاءِ الزَّكَاةِ ، وَالنُّصْحِ لِكُلِّ مُسْلِمٍ . متفقٌ عَلَيْهِ .

Jariyr bin 'Abdillaah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: "Nilimbai Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) juu ya kusimamisha Swalaah na kutoka Zakaah na kumpa nasaha kila Muislamu." [Al-Bukhaariy na Muslim].

 

Hadiyth – 9

وعن أَبي هريرة رضي الله عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( مَا مِنْ صَاحِبِ ذَهَبٍ ، وَلاَ فِضَّةٍ ، لا يُؤَدِّي مِنْهَا حَقَّهَا إِلاَّ إِذَا كَانَ يَومُ القِيَامَةِ صُفِّحَتْ لَهُ صَفَائِحُ مِنْ نَارٍ، فَأُحْمِيَ عَلَيْهَا في نَارِ جَهَنَّمَ ، فَيُكْوَى بِهَا جَنْبُهُ، وَجَبِينُهُ ، وَظَهْرُهُ، كُلَّمَا بَرَدَتْ أُعِيدَتْ لَهُ في يَومٍ كَانَ مِقْدَارُهُ خَمْسِينَ ألْفَ سَنَةٍ ، حَتَّى يُقْضَى بَيْنَ العِبَادِ فَيَرَى سَبيلَهُ ، إمَّا إِلَى الجَنَّةِ ، وَإمَّا إِلَى النَّارِ )) قيل : يَا رسولَ الله ، فالإبلُ ؟ قَالَ : (( وَلاَ صَاحِبِ إبلٍ لا يُؤَدِّي مِنْهَا حَقَّهَا ، وَمِنْ حَقِّهَا حَلْبُهَا يَومَ وِرْدِهَا ، إِلاَّ إِذَا كَانَ يَومُ القِيَامَةِ بُطِحَ لَهَا بِقَاعٍ قَرْقَرٍ أوْفَرَ مَا كَانَتْ ، لاَ يَفْقِدُ مِنْهَا فَصيلاً وَاحِداً ، تَطَؤُهُ بِأخْفَافِهَا ، وَتَعَضُّهُ بِأفْوَاهِهَا ، كُلَّمَا مَرَّ عَلَيْهِ أُولاَهَا ، رُدَّ عَلَيْهِ أُخْرَاهَا ، في يَوْمٍ كَانَ مِقْدَارُهُ خَمْسِينَ ألْفَ سَنَةٍ ، حَتَّى يُقْضى بَيْنَ العِبَادِ ، فَيَرَى سَبِيلَهُ ، إمَّا إِلَى الجَنَّةِ ، وَإمَّا إِلَى النَّارِ )) قِيلَ : يَا رَسولَ اللهِ ، فَالبَقَرُ وَالغَنَمُ ؟ قَالَ : (( وَلاَ صَاحِبِ بَقَرٍ وَلاَ غَنَمٍ لاَ يُؤَدِّي مِنْهَا حَقَّهَا ، إِلاَّ إِذَا كَانَ يَوْمُ القِيَامَةِ ، بُطِحَ لَهَا بقَاعٍ قَرْقَرٍ ، لاَ يَفْقِدُ مِنْهَا شَيْئاً ، لَيْسَ فِيهَا عَقْصَاءُ ، وَلاَ جَلْحَاءُ ، وَلاَ عَضْبَاءُ ، تَنْطَحُهُ بقُرُونها ، وَتَطَؤُهُ بِأظْلاَفِهَا ، كُلَّمَا مرَّ عَلَيْهِ أُولاَهَا ، رُدَّ عَلَيْهِ أُخْرَاهَا ، في يَومٍ كَانَ مِقْدَارُهُ خَمْسِينَ ألْفَ سَنَة حَتَّى يُقْضى بَيْنَ العِبَادِ ، فَيَرى سَبيِلَهُ ، إمَّا إِلَى الجَنَّةِ ، وَإمَّا إِلَى النَّارِ )) قيل : يَا رسول الله فالخَيْلُ ؟ قَالَ : (( الخَيلُ ثَلاَثَةٌ : هِيَ لِرَجُلٍ وِزْرٌ ، وَهِيَ لِرَجُلٍ سِتْرٌ ، وَهِيَ لِرَجُلٍ أجْرٌ . فَأمَّا الَّتي هي لَهُ وِزْرٌ فَرَجُلٌ ربطها رِيَاءً وَفَخْراً وَنِوَاءً عَلَى أهْلِ الإسْلاَمِ ، فَهِيَ لَهُ وِزْرٌ ، وَأمَّا الَّتي هي لَهُ سِتْرٌ ، فَرَجُلٌ رَبَطَهَا في سَبيلِ الله ، ثُمَّ لَمْ يَنْسَ حَقَّ اللهِ في ظُهُورِهَا ، وَلاَ رِقَابِهَا ، فَهِيَ لَهُ سِتْرٌ ، وَأمَّا الَّتي هي لَهُ أجْرٌ ، فَرَجُلٌ رَبَطَهَا في سَبيلِ الله لأهْلِ الإسْلاَمِ في مَرْجٍ ، أَوْ رَوْضَةٍ فَمَا أكَلَتْ مِنْ ذَلِكَ المَرْجِ أَوْ الرَّوْضَةِ مِنْ شَيْءٍ إِلاَّ كُتِبَ لَهُ عَدَدَ مَا أَكَلَتْ حَسَنَات وكُتِبَ لَهُ عَدَدَ أرْوَاثِهَا وَأبْوَالِهَا حَسَنَات ، وَلاَ تَقْطَعُ طِوَلَهَا فَاسْتَنَّتْ شَرَفاً أَوْ شَرَفَيْنِ إِلاَّ كَتَبَ اللهُ لَهُ عَدَدَ آثَارِهَا ، وَأرْوَاثِهَا حَسَنَاتٍ ، وَلاَ مَرَّ بِهَا صَاحِبُهَا عَلَى نَهْرٍ ، فَشَرِبَتْ مِنْهُ ، وَلاَ يُرِيدُ أنْ يَسْقِيهَا إِلاَّ كَتَبَ اللهُ لَهُ عَدَدَ مَا شَرِبَتْ حَسَنَاتٍ )) قِيلَ : يَا رسولَ اللهِ فالحُمُرُ ؟ قَالَ : (( مَا أُنْزِلَ عَلَيَّ في الحُمُرِ شَيْءٌ إِلاَّ هذِهِ الآية الفَاذَّةُ الجَامِعَةُ : [ فَمَنْ يَعْمَلْ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ خَيْراً يَرَهُ وَمَنْ يَعْمَلْ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ شَرّاً يَرَهُ ] )) متفقٌ عَلَيْهِ ، وهذا لفظ مسلم 

Kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema: Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakuna mwenye dhahabu na fedha, na hatoi haki yake, ila Siku ya Qiyaamah ataviringishwa mabamba ya moto. Atachomwa navyo ubavu wake, paji lake la uso na mgongo wake. kila yakipoa yatarudishwa katika siku kiasi chake ni miaka elfu hamsini, mpaka ihukumiwe baina ya waja, Waonyeshwe njia yao ima ya Peponi au ya Motoni. Pakasemwa: "Ee Rasuli wa Allaah! Je, ngamia?" , Akasema: "Hata mwenye ngamia hatoi haki yake, na haki yake ni maziwa tangu siku ilipoanza kunywa maji. Vingenevyo atachomwa kwa uso wake Siku ya Qiyaamah katika wangwa mpana kuliko, Nagamia wake watakuwa wengi kama walivyokuwa na wamenona, Hakosekani hata mmoja, watamkanyanga kwa miguu yao na watamng'ata kwa meno yao. Wa mwisho akimaliza wa kwanza anaanza. Katika siku kiasi chake ni miaka hamsini elfu, hadi ihukumiwe baina ya waja, Ataona njia yake, ima ya Peponi au ya Motoni." Pakasemwa: "Ee Rasuli wa Allaah! Je, ng'ombe na mbuzi?" Akasema: "Hata mwenye ng'ombe na mbuzi, hatoi haki zake, Siku ya Qiyaamah ni atarushwa kwa uso wake katika wangwa mpana kuliko, hakosekani hata mmoja, hakuna asiye na pembe. Watamrarua kwa pembe zao, kila wakimaliza wa kwanza wa mwisho atarudishwa, katika siku kiasi chake ni miaka elfu hamsini, mpaka ihukumiwe baina ya waja, na akaona njia yake ima ya Peponi au Motoni." Akaulizwa: "Ee Rasuli wa Allaah! Je, mwenye farasi?" Akasema: "Farasi anafugwa kwa moja katika mambo matatu: Wao kwa baadhi ya watu ni njia ya kupata dhambi, na kwa wengine ni sitara na kwa wengine ni njia ya malipo. Ama ambaye anapata dhambi ni kwa yule mtu aliyemfunga kwa ajili ya kujionyesha na fakhari na kwa uadui kwa Waislamu, basi ufugaji huo ni dhambi kwake. Na ama ambaye kwake ni kwa sitara ni mtu aliyemfunga kwa ajili ya kupigania Dini ya Allaah, kisha asisahau haki ya Allaah kwa migongo yao na shingo zao, basi kwa ufugaji huo atapata maisha yake. Na ama ambaye atapata malipo (thawabu) ni mtu aliyemfunga farasi wake katika njia ya Allaah kwa sababu ya Waislamu, akafika katika malisho au bustani. Kwa hivyo anachokula katika malisho au bustani chochote ila huandikiwa idadi ya alichokula mema na pia huandikiwa idadi ya kinyesi chake na alama za kwato zake pia ni mema. Na wala hatakata kamba yaek ndefu na akaruka hatua moja au mbili isipokuwa Allaah humuandikia idadi ya hatua zake na kinyesi chake kuwa ni mema. Na wala hatakwenda naye katika mto na akanywa ndani yake na hakutaka kumnywesha basi kwa hilo Allaah humuandikia mema kwa idadi ya alicho kunywa. Akaulizwa: "Ee Rasuli wa Allaah! Je, mwenye punda?" Akasema: "Kuhusu punda sikuteremshiwa isipokuwa ayah hii yenye kukusanya aina yake: 'Basi yule atakayetenda kheri uzito wa chembe ataiona Na yule atakayetenda shari uzito wa chembe ataiona'." [Al-Zalzalah: 7-8] [Al-Bukhaariy na Muslim, na hii ni lafdhi ya Muslim].

 
 

 

 

Share