Sharbati Ya Stroberi (Strawberry Shake)

VIPIMO
Ndizi 2 Kiasi
Stroberi (strawberries) 2 Vikombe vya chai
Vipande vya barafu 1 Kikombe cha chai
Maziwa ¾ − 1 Kikombe cha chai
Juisi ya machungwa 1 Kikombe cha chai
Asali 2 Vijiko vya supu
NAMNA YA KUTAYARISHA
1. Kata kata ndizi na stroberi na uweke kwenye mashine (blender) pamoja na vipimo vyote vilivyobaki.
2. Saga hadi ilainike vizuri.
3. Mimina kwenye gilasi na ni vizuri kunywiwa hapo hapo.
- Login or register to post comments
- Email this page
- Chapisha


