01-Riyaadhw Asw-Swaalihiyn: Mlango Wa Fadhila za Kuhimidi na Kushukuru

 

Riyaadhw Asw-Swaalihiyn

باب فضل الحَمْدُ والشكر

01-Mlango Wa Fadhila za Kuhimidi na Kushukuru

 

Alhidaaya.com

 

قال الله تَعَالَى :

فَاذْكُرُونِي أَذْكُرْكُمْ وَاشْكُرُوا لِي وَلَا تَكْفُرُونِ﴿١٥٢﴾

Basi nidhukuruni na Mimi Nitakukumbukeni, na nishukuruni wala msinikufuru. [Al-Baqarah: 102]

لَئِن شَكَرْتُمْ لَأَزِيدَنَّكُمْ ۖ ﴿٧﴾

Ikiwa mtashukuru, bila shaka Nitakuzidishieni (Neema Zangu) [Ibraahiym: 7]

وَقُلِ الْحَمْدُ لِلَّـهِ ﴿١١١﴾

Na sema: AlhamduliLLaah (Himidi Anastahiki Allaah) [Al-Israa: 111]

وَآخِرُ دَعْوَاهُمْ أَنِ الْحَمْدُ لِلَّـهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ﴿١٠﴾

Na wito wao wa mwisho ni AlhamduliLLaah (Himdi Anastahiki Allaah), Rabb wa walimwengu. [Yuwnus: 10]

 

Hadiyth – 1

وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه : أنَّ النبيَّ صلى الله عليه وسلم ، أُتِيَ لَيْلَةَ أُسْرِيَ بِهِ بِقَدَحَيْنِ مِنْ خَمْرٍ وَلَبَنٍ ، فَنَظَرَ إِلَيْهمَا فَأَخَذَ اللَّبَنَ . فَقَالَ جِبريل : الحَمْدُ للهِ الَّذِي هَدَاكَ لِلفِطْرَةِ لَوْ أخَذْتَ الخَمْرَ غَوَتْ أُمَّتُكَ . رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kuwa Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) aliletewa vikombe viwili vya vinywaji usiku wa Israa', kimoja cha pombe na chengine cha maziwa. Akaviangalia, kisha akachukua cha maziwa. Hapo Jibriyl akamwambia: "Sifa zote njema anastahiki Allaah ambaye kwamba amekuongoza katika maumbile. Lau ungechagua kikombe cha pombe, Ummah wako ungepotea." [Muslim]

 

Hadiyth – 2

وعن أَبي هريرة رضي اللهُ عنه ، عن رسول الله صلى الله عليه وسلم قَالَ : (( كُلُّ أمْرٍ ذِي بَالٍ لاَ يُبْدأُ فِيهِ بِالحَمْدُ للهِ فَهُوَ أقْطَعُ )) . حديث حسن ، رواه أَبُو داود وغيره .

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraiyrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Kila jambo muhimu halikuanza kwa kumsifu Allaah litakuwa ni lenye kasoro (kukatika)." [Abu Daawud, Ibn Maajah na Ahmad]

 

Hadiyth – 3

وعن أَبي موسى الأشعري رضي اللهُ عنه : أنَّ رسول الله صلى الله عليه وسلم ، قَالَ : (( إِذَا مَاتَ وَلَدُ العَبْدِ قَالَ اللهُ تَعَالَى لِمَلائِكَتِهِ : قَبَضْتُمْ وَلَدَ عَبْدي ؟ فَيقولون : نَعَمْ ، فيقول : قَبَضْتُمْ ثَمَرَةَ فُؤادِهِ ؟ فيقولون : نَعَمْ ، فيقول : ماذا قَالَ عَبْدِي ؟ فَيقولون : حَمدَكَ وَاسْتَرْجَعَ ، فيقُولُ اللهُ تَعَالَى : ابْنُوا لِعَبْدي بَيتاً في الجَنَّةِ ، وَسَمُّوهُ بَيْتَ الحَمْدِ )) . رواه الترمذي ، وقال : (( حديث حسن )) .

Imepokewa kutoka kwa Abu Muwsaa Al-Ash'ariy (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Anapokufa mtoto wa mja, Allaah anawauliza Malaaikah: 'Mumechukua mtoto wa mja wangu?' Wanasema: 'Ndio.' Atauliza tena: 'Mumechukua tunda la moyo wake?' Watasema: 'Ndio.' Atauliza tena: 'Mja wangu amesema nini?' Watasema: 'Amekushukuru (na kukusifu) na akayakinisha kuwa atarudi Kwako (kwa kusema Innaa liLLaahi wa innaa ilayhi raaji'uwn).' Atasema: Allaah Ta'aalaa: 'Mjengeeni mja wangu nyumba Peponi na muiite Nyumba ya Kushukuriwa." [At-Tirmidhiy, na akasema ni Hadiyth Hasan] 

 

Hadiyth – 4

وعن أنس رضي اللهُ عنه ، قَالَ : قَالَ رسول الله صلى الله عليه وسلم : (( إنَّ الله لَيرْضَى عَنِ العَبْدِ يَأكُلُ الأَكْلَةَ ، فَيَحْمَدُهُ عَلَيْهَا ، وَيَشْرَبُ الشَّرْبَة ، فَيَحْمَدُهُ عَلَيْهَا )) رواه مسلم .

Imepokewa kutoka kwa Anas (Radhwiya Allaahu 'anhu) ya kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: "Hakika inampendeza Allaah kwa mja anayekula chakula kisha akamshukuru juu yake au anayekunywa kinywaji kisha akamshukuru juu yake." [Muslim]

 

Share