009-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Viapo Na Nadhiri: Mwenye Kuapa Kwa Kusema: لَعَمْرُ الله “Naapa kwa Uhai wa Allaah”

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الأَيْمَانِ وَالنُّذُوْر

Kitabu Cha Viapo Na Nadhiri

 

09- Mwenye Kuapa Kwa Kusema: لَعَمْرُ الله “Naapa kwa Uhai wa Allaah”

 

Alhidaaya.com

 

 

Imekuja katika Hadiyth ya ‘Aaishah (Radhwiya Allaah ‘anhaa): Watu waliomzushia uzushi wa zinaa na wakasema waliyoyasema na Allaah Akamtakasa na uzushi huo, Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihii wa sallam) alisimama na akataka udhuru toka kwa ‘Abdillaah bin Ubayya, na Usayd bin Khudhayr akasimama na kumwambia Sa’ad bin ‘Ubaadah:

 

" لَعَمْرُ الله لَنقْتُلَنَّه "

“Naapa kwa Uhai wa Allaah, lazima tutamuua”. [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (6662)].

 

"العَمْرُ" ina maana ya uhai.  Mwenye kusema "لَعَمْرُ اللهِ" ni kama ameapa kwa Kubakia Milele Allaah, na hili linajuzu kwa ‘Ulamaa wote, na kiapo kinafungika kutokana na Hadiyth iliyotangulia.  Katika Hadiyth hii, Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihii wa sallam) alikikubali kiapo cha Usayd (Radhwiya Allaah ‘anhu) cha "لَعَمْرُ اللهِ"  na wala hakumkataza.

 

Na Allaah Ta’aalaa Amesema:

 

"لَعَمْرُكَ إِنَّهُمْ لَفِي سَكْرَتِهِمْ يَعْمَهُونَ"

 

15.  Naapa kwa uhai wako (ee Muhammad صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَآلِهِ وَسَلَّمَ).  Hakika wao walikuwa katika ulevi wao wanatangatanga kwa upofu.  [Al-Hijr (72)].

 

Ikathibiti kwalo kuwa ni tamko la kisharia.  Kisha kwa kuwa maana yake ni: “Naapa kwa Usalio wa Milele wa Allaah”, au: “Naapa kwa Uhai wa Allaah”.  Kiapo hiki kinakuwa kwa Sifa ya Dhati ya Allaah, hivyo kinakuwa ni chenye kujuzu.

 

 

Share