032-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Viapo Na Nadhiri: Kafiri Akinadhiria Jambo Jema Kisha Akasilimu

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الأَيْمَانِ وَالنُّذُوْرِ

 

Kitabu Cha Viapo Na Nadhiri

 

032- Kafiri Akinadhiria Jambo Jema Kisha Akasilimu

 

Alhidaaya.com

 

 

 

“Ulamaa wamekhitalifiana kuhusu wajibu wa kutekeleza nadhiri yake baada ya kusilimu katika kauli mbili:  [Al-Muhallaa (8/25) na Naylul Awtwaar (8/286)].

 

Kauli Ya Kwanza:

 

Ni lazima atekeleze nadhiri yake akisilimu.  Ni madhehebu ya Ash-Shaafi’iy, Daawuwd Adh-Dhwaahiriy na Ibn Hazm.  Dalili yao ni:

 

1-  Hadiyth ya Ibn ‘Umar kwamba ‘Umar alisema:

 

"يَا رَسُوْلَ اللهِ، إنِّي نَذَرْتُ أَنْ أَعْتَكِفَ لَيْلَةً فِي الْمَسْجِدِ الْحَرَامِ‏ فِي الْجَاهِلِيَّةِ.‏ قَالَ: ‏"‏أَوْفِ بِنَذْرِكَ ‏".

 

“Mimi niliweka nadhiri wakati wa ujahili ya kukaa ‘itikafu usiku mmoja ndani ya Al-Masjid Al-Haraam”.  Rasuli akamwambia:  Tekeleza nadhiri yako”. [Hadiyth Swahiyh.  Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (2032) na Muslim (1656)].

 

2-  Hadiyth ya ‘Amri bin Shu’ayb toka kwa baba yake toka kwa babu yake kwamba mwanamke mmoja alikuja kwa Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema:

 

"يَا رَسُولَ اللَّهِ، إِنِّي نَذَرْتُ أَنْ أَضْرِبَ عَلَى رَأْسِكَ بِالدُّفِّ ‏.‏ قَالَ ‏:‏ ‏"‏ أَوْفِي بِنَذْرِكِ ‏"‏ ‏.‏ قَالَتْ ‏:‏ إِنِّي نَذَرْتُ أَنْ أَذْبَحَ بِمَكَانِ كَذَا وَكَذَا، مَكَانٌ كَانَ يَذْبَحُ فِيهِ أَهْلُ الْجَاهِلِيَّةِ ‏.‏ قَالَ ‏:‏ ‏"‏ لِصَنَمٍ ‏"‏ ‏.‏ قَالَتْ ‏:‏ لاَ ‏.‏ قَالَ ‏:‏ ‏"‏ لِوَثَنٍ ‏"‏ ‏.‏ قَالَتْ ‏:‏ لاَ ‏.‏ قَالَ ‏:‏ ‏"‏ أَوْفِي بِنَذْرِكِ".

 

“Ee Rasuli wa Allaah!  Mimi niliweka nadhiri nikupigie dufu mbele yako. Akamwambia:  Tekeleza nadhiri yako.  Akasema:  Niliweka nadhiri ya kuchinja mahala fulani na fulani; mahala ambapo watu wa ujahili walikuwa wakichinjia. Akamuuliza:  Kwa ajili ya sanamu (lenye sura)?  Akasema:  Hapana. Akamuuliza:  Kwa ajili ya “wathan” (kiabudiwa kisicho na sura)?  Akasema: Hapana.  Akamwambia:  Tekeleza nadhiri yako”.  [Sanad yake ni Hasan. Imekharijiwa na Abu Daawuwd (3312).  Angalia Al-Irwaa].

 

Kauli Ya Pili:

 

Nadhiri ya kafiri haizingatiwi, na halazimishwi kuitekeleza akisilimu.  Ni madhehebu ya Jumhuwr.  Wametoa dalili kwa:

 

1-  Kauli Yake Ta’aalaa:

 

"لَئِنْ أَشْرَكْتَ لَيَحْبَطَنَّ عَمَلُكَ وَلَتَكُونَنَّ مِنَ الْخَاسِرِينَ"

 

“Ukifanya shirki bila shaka zitaporomoka ‘amali zako”.  [Az Zumar: (39: 65)].

 

2-  Kauli Yake Ta’aalaa:

 

"وَقَدِمْنَا إِلَىٰ مَا عَمِلُوا مِنْ عَمَلٍ فَجَعَلْنَاهُ هَبَاءً مَّنثُورًا"

 

23.  Na Tutayaendea yale waliyoyatenda ya ‘amali yoyote ile, Tutayafanya   chembechembe za vumbi zinazoelea hewani zikitawanyika.  [Al-Furqaan: 25].

 

Ibn Hazm amejibu kuhusu hili akisema kwamba hakuna hujjah yoyote ndani yake, kwa kuwa haya yote yameteremka kumzungumzia mtu ambaye amekufa hali ya kuwa ni kafiri kwa matini ya kila Aayah kati ya Aayah hizi mbili.  Na Allaah Ta’aalaa Amesema:

 

"وَمَن يَرْتَدِدْ مِنكُمْ عَن دِينِهِ فَيَمُتْ وَهُوَ كَافِرٌ فَأُولَـٰئِكَ حَبِطَتْ أَعْمَالُهُمْ"

 

“Na atakayeritadi miongoni mwenu kutoka Dini yake, akafariki hali ya kuwa ni kafiri, basi hao zimeporomoka ‘amali zao”.  [Al-Baqarah: 217].

 

Kisha wao baada ya haya, wanajuzisha mauzo ya kafiri, ndoa yake, akitoacho bure, swadaqah yake na kuacha kwake huru!!

 

Na katika Hadiyth ya Abu Hurayrah –kuhusu kisa cha kusilimu Thumaamah bin Uthaal (Radhwiya Allaah ‘anhu) kwamba alimwambia Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam):

 

"وَإِنَّ خَيْلَكَ أَخَذَتْنِي وَأَنَا أُرِيدُ الْعُمْرَةَ فَمَاذَا تَرَى، فَبَشَّرَهُ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ وَأَمَرَهُ أَنْ يَعْتَمِرَ".

 

“Na askari wako wa farasi waliniteka, na hali mimi nataka kufanya ‘Umrah.  Je, waonaje?  Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akampa khabari njema, na akamwamuru afanye ‘Umrah”.  [Hadiyth Swahiyh. Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (4372) na Muslim (1764)].

 

Na huyu ni kafiri, alitoka hali ya kuwa anataka kufanya ‘Umrah, akasilimu, na Rasuli akamwamuru akamilishe niyyah yake.

 

Ninasema:  “Lenye nguvu ni kwamba inamlazimu atekeleze nadhiri ya twa’a aliyoiweka wakati wa ukafiri wake anaposilimu.  Na Allaah Ndiye Ajuaye zaidi”.

                                                           

·        Kumlipia Maiti Nadhiri Yake Ya Twa’a

 

Mwanadamu akiweka nadhiri ya twa’a katika ambalo inamlazimu kulitekeleza kisha akafariki kabla ya kulitekeleza, basi walii wake atamlipia nadhiri yake. Ikiwa nadhiri ni mali, basi atatoa katika mali ya maiti kabla ya kutoa madeni ya watu kutokana na Kauli Yake Ta’aalaa:

 

"مِن بَعْدِ وَصِيَّةٍ يُوصِي بِهَا أَوْ دَيْنٍ"

 

“baada ya kutoa wasia aliousia (maiti) au kulipa deni”.  [An-Nisaa: (11)].

 

Hapa Allaah Ta’aalaa Amelitaja deni kiujumla, yaani deni lolote lile; la mali au la ‘ibaadah.  Na Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

 

"فَدَيْنُ اللَّهِ أَحَقُّ أَنْ يُقْضَى ‏"‏.

 

“Basi Deni la Allaah lina haki zaidi kulipwa”.  [Hadiyth Swahiyh.  Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (1953) na Muslim (1148)].

 

Na kama nadhiri ni ‘ibaadah kama Hijjah, swawm, ‘itikafu na mfano wa hayo, basi walii wake atamfanyia kwa dalili zifuatazo:

 

1-  Toka kwa Ibn ‘Abbaas:

 

" أَنَّ سَعْدَ بن عبَادَة رَضِي اللهُ عَنْهُم اسْتَفْتَى النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فِي نَذْرٍ كَانَ عَلَى أُمِّهِ فَتُوُفِّيَتْ قَبْلَ أَنْ تَقْضِيَهُ فَأَفْتَاهُ أَنْ يَقْضِيَهُ عَنْهَا".

 

“Kwamba Sa’ad bin ‘Ubaadah (Radhwiya Allaah ‘anhu) alimuuliza Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusu nadhiri ambayo mama yake aliiweka na akafariki kabla hajaitekeleza.  Akamjibu kuwa amlipie mama yake”. Hadiyth Swahiyh.  [Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (2761) na Muslim (1638)].

 

Na katika tamshi jingine alimwambia:

 

"اقْضِهِ عَنْهَا"

 

“Mlipie”.

 

2-  Toka kwa Ibn ‘Abbaas kwamba:

 

جَاءَتِ امْرَأَةٌ إِلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ فَقَالَتْ : يَا رَسُولَ اللَّهِ، إِنَّ أُمِّي مَاتَتْ وَعَلَيْهَا صَوْمُ مِنْ نَذْرٍ، أَفَأَصُومُ عَنْهَا؟ فقَالَ لَهَا النَّبِيُّ صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ‏"‏ أَرَأَيْتِ لَوْ كَانَ عَلَى أُمِّكِ دَيْنٌ فَقَضَيْتِيهِ أَكَانَ يُؤَدِّي ذَلِكِ عَنْهَا؟ ‏"‏ ‏.‏ قَالَتْ نَعَمْ ‏.‏ قَالَ ‏"‏ فَصُومِي عَنْ أُمِّكِ ‏"‏ ‏

 

“Mwanamke mmoja alikuja kwa Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam akasema:  Ee Rasuli wa Allaah!  Hakika mama yangu amekufa naye anadaiwa swawm ya nadhiri.  Je, naweza kumfungia?  Nabiy (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihii wa sallam) akamwambia:  Hebu angalia, je kama mama yako alikuwa na deni halafu wewe ukalilipa, je hilo litakuwa limemlipia deni lake?  Akasema:  Na’am.  Akamwambia:  Basi mfungie mama yako”.  [Hadiyth Swahiyh.  Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (953) na Muslim (1148) na tamshi ni lake].

 

3-  Imeripotiwa toka kwa ‘Aaishah (Radhwiya Allaah ‘anhaa):

 

"أَنَّهَا اعْتَكَفَتْ عَنْ أَخِيْهَا بَعْدَ مَا مَاتَ".

 

“Kwamba alimkalia ‘itikafu kaka yake baada ya kufariki”.  [Isnaad yake ni Dhwa’iyf.  [Imekharijiwa na Sa’iyd bin Mansour (424) na Ibn Abiy Shaybah (2/339)].

 

·        Je, Maiti Hulipiwa Swalaah Aliyoiwekea Nadhiri?

 

Mwelekeo wa Jumhuwr ya ‘Ulamaa ni kuwa mtu hamswalii mwingine, bali Ibn Battwaal amehadithia kufikiwa ‘Ijmaa juu ya hilo!!  Lakini hili linatenguliwa na:

 

"أَنَّ ابْنَ عُمَرَ أَمَرَ امْرَأَةً جَعَلَتْ أُمَّهَا عَلَى نَفْسِهَا صَلاَةً بِقُبَاءَ فَقَالَ: صَلِّيْ عَنْهَا"

 

“Kwamba Ibn ‘Umar alimwamuru mwanamke mmoja ambaye mama yake alijiwekea nadhiri ya kuswali Qubaa kwa kumwambia:  “Swali kwa niaba yake”. [Al-Bukhaariy amesema ni Mu’allaq (11/584) kwa tamko la “Jazm”, na Al-Haafidh hakuifanya Mawsuul katika At-Taghliyq (5/203)].

 

Daawuwd na Ibn Hazm wamewajibisha kulipwa Swalaah iliyowekewa nadhiri na maiti.  [Al-Muhallaa].

 

 

Share