03-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji: Chinjo La Kisharia: Masharti Ya Kuchinja:

 

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ الأَطْعِمَةِ وَالأَشْرِبةِ وَمَا يَتَعَلَّقُ بِهِمَا

 

 Kitabu Cha Vyakula Na Vinywaji Na Yanayohusiana Na Viwili Hivi

 

التَّذْكِيَةُ الشَّرْعِيَّةُ

 

Chinjo La Kisharia

 

 

Alhidaaya.com 

 

 

03-Chinjo La Kisharia: Masharti Ya Kuchinja:

 

Kuna masharti kadhaa ambayo ni lazima yawepo ili mnyama anayechinjwa awe halali kuliwa.  Baadhi yake yanahusiana na mnyama mwenyewe, mengine yanahusiana na mchinjaji, na baadhi nyingine kwa zana ya kuchinjia.

 

Masharti Ya Mnyama Anayechinjwa

 

1-  Awe hai wakati anapochinjwa.  Mnyama mfu hachinjwi.

 

2-  Kuchinjwa kwake kuwe ndio sababu ya kutoka roho yake, na si kutokana na sababu nyingine.

 

3-  Asiwe amewindwa eneo la Al-Haram.  Hili limeelezwa katika Kitabu cha Hijja kwamba ni marufuku kuwinda eneo la Al-Haram.  Na Rasuli (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema kuhusiana na Makkah:

 

"فَلَا يُنَفَّرُ صَيْدُهَا"

 

“Wanyama wake hawasumbuliwi (wala kuwindwa)”. [Hadiyth Swahiyh.  Imekharijiwa na Al-Bukhaariy (1349) na Muslim (1355)].

                                                                         

 

Share