005-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia: Mavazi Na Mapambo Kwa Wanaume:Vivazi Vinavyoruhusiwa Na Vinavyopendeza Zaidi Kuvaliwa Na Wanaume: Inapendeza Kuvaa Kilemba

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

 

كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ  وَأَحْكَامُ النَّظَرِ

 

 Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia 

 

 

اللِّبَاسُ وَالزِّيْنَةُ للرِّجَالِ 

Mavazi Na Mapambo Kwa Wanaume 

 

 

Alhidaaya.com 

 

 

 

005-  Mavazi Na Mapambo Kwa Wanaume: Vivazi Vinavyoruhusiwa Na Vinavyopendeza Zaidi Kuvaliwa Na Wanaume: Inapendeza Kuvaa Kilemba

 

Toka kwa Jaabir:

 

" أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ دَخَلَ مَكَّةَ يَوْمَ الفَتْحِ وَعَلَيْهِ عِمَامَةٌ سَوْداءُ"

 

Kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliingia Makkah Siku ya Ukombozi akiwa amevalia kilemba cheusi”.  [Hadiyth Swahiyh.  Imekharijiwa na Muslim (1358), At-Tirmidhiy (1735), An-Nasaaiy, (2869) Abu Daawuwd (4076) na Ibn Maajah (2822)].

 

Inakuwa vizuri zaidi kilemba kiteremke kati ya mabega mawili.  Na hii ni kwa Hadiyth ya ‘Amri bin Hurayth aliyesema:

 

"كَأَنِّيْ أَنْظُرُ إِلى رَسُوْلِ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ عَلَى المِنْبَرِ وَعَلَيْهِ عِمَامَةٌ سَوْدَاءٌ قَدْ أَرْخَى طَرَفَيْهَا بَيْنَ الكَتِفَيْنِ"

 

“Kana kwamba mimi namwangalia Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akiwa amevaa kilemba cheusi, huku amening’iniza ncha zake mbili baina ya mabega yake mawili”.  [Hadiyth Swahiyh.  Imekharijiwa na Muslim (1359) na Ibn Maajah (2821)].

 

Ibn ‘Umar amesema: 

 

"كَانَ رَسُوْلُ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ إِذَا اعْتَمَّ سَدلَ عِمَامَتَهُ بَيْنَ كَتِفَيْهِ"

 

“Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa anapopiga kilemba, hukiachilia kilemba chake baina ya mabega yake mawili”.  [Hadiyth Hasan Lighayrih.  Imekharijiwa na At-Tirmidhiy (1736), Ibn Hibaan (6397) na At-Twabaraaniy (12/379)]. 

 

An-Nawawiy kasema:  “Inajuzu kuvaa kilemba kwa kuzitupia ncha zake mbili au kwa kutozitupia, na wala hakuna ukaraha wa kimoja kati ya viwili, na hakuna tamshi lolote sahihi lililokataza kutotupia.  Ama kuzitupia kwa kuvuka sana mpaka, hilo litakuwa ni haramu kwa wenye kujiona, na kwa wengine itakuwa ni makruhu”.  [Al-Majmuw’u (4/457)]

 

 

.

Share