008-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia: Mavazi Na Mapambo Kwa Wanaume:Vivazi Vilivyokatazwa Kwa Wanaume Kuvivaa: Ni Haramu Kuvaa Nguo Ya Kipekee Ili Kuonekana Tofauti (Vazi La Umashuhuri)

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

 

كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ  وَأَحْكَامُ النَّظَرِ

 

 Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia 

 

 

اللِّبَاسُ وَالزِّيْنَةُ للرِّجَالِ 

Mavazi Na Mapambo Kwa Wanaume 

 

 

Alhidaaya.com 

 

 

 

008-  Mavazi Na Mapambo Kwa Wanaume: Vivazi Vilivyokatazwa Kwa Wanaume Kuvivaa: Ni Haramu Kuvaa Nguo Ya Kipekee Ili Kuonekana Tofauti (Vazi La Umashuhuri):

 

 

 

Ibn ‘Umar amesema:  “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: 

 

"مَنْ لَبِسَ ثَوْبَ شُهْرَةٍ فيٍ الدُّنْيَا أَلْبَسَهُ اللَّهُ ثَوْبَ مَذَلَّةٍ يَوْمَ الْقِيَامَةِ" [ثُمَّ أَلْهَبَ فِيْهِ نَارًا]

 

“Mwenye kuvaa nguo ya kutaka yeye pekee aonekane tofauti na wengine hapa duniani, Allaah Atamvisha nguo ya udhalili Siku ya Qiyaamah [Kisha Atamwashia ndani yake moto].  [Hadiyth Hasan.  Imekharijiwa na Abu Daawuwd (4029), Ibn Maajah (3606) na Ahmad (2/92), iko kwenye Swahiyhul Jaami’i (6526)].

 

Ibn Al-Athiyr amesema:  “Nguo hii, ni nguo ya mtu kutaka umashuhuri kati ya watu, rangi yake iwe tofauti na rangi ya nguo zao (au mshono, kitambaa n.k) kiasi cha kuwafanya watu wanyanyue macho yao kuiangalia huku akitamba kwa kiburi na kujiona yeye ni yeye, hakuna zaidi yake”.

                                                                       

Share