012-Swahiyh Fiqh As-Sunnah: Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia: Mavazi Na Mapambo Kwa Wanaume:Vivazi Vilivyokatazwa Kwa Wanaume Kuvivaa: Nguo Iliyotengenezwa Kwa Ngozi Ya Wanyama Wakali

 

Swahiyh Fiqh As-Sunnah

 

كِتَابُ اللِّبَاسِ وَالزِّيْنَةِ  وَأَحْكَامُ النَّظَرِ

 

 Kitabu Cha Mavazi Na Mapambo Na Hukmu Za Kuangalia 

 

 

اللِّبَاسُ وَالزِّيْنَةُ للرِّجَالِ 

Mavazi Na Mapambo Kwa Wanaume 

 

 

Alhidaaya.com 

 

 

 

 

012-  Mavazi Na Mapambo Kwa Wanaume: Vivazi Vilivyokatazwa Kwa Wanaume Kuvivaa:  Nguo Iliyotengenezwa Kwa Ngozi Ya Wanyama Wakali:

 

 

 

Ni kama simba, chui, duma na kadhalika.  Ni haramu kuvaa nguo au viatu vilivyotengenezwa kwa ngozi za wanyama hawa kutokana na neno lake Rasuli wa Allaah (Swalla Allaah ‘alayhi wa  aalihi wa sallam):

 

"لَا تَرْكَبُوا الْخَزَّ وَلَا النِّمَارَ"

 

“Msikalie hariri wala ngozi ya chui”.  [Hadiyth Swahiyh.  Imekharijiwa na Abu Daawuwd (4129) na Ibn Maajah (3656)].

 

Rasuli amekataza kutumia vitu hivi kutokana na kuwa ni mapambo, na kuwa vinajenga kiburi kwa mtumiaji, lakini pia ni nguo za watu wasio na asili ya Uarabu (Waajemi).  [‘Awnul Ma’abuwd (11/188)]

 

 

Share